Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Wakuu, kwanza poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima ya leo. Ndugu yenu nataka kufanya maamuzi ila sitaki nionekane nimedhulumu haki ya mtu.

Miezi 3 iliyopita kuna jamaa ambao sifahamiani nao; walikuwa wanasafirisha magendo kwa gari binafsi kutoka point "X" kwenda point "Y". Wakakamatwa na polisi njiani wakawekwa ndani. Gari nayo (Spacio) ikazuiliwa kama kielelezo.

Sijui walielewana nini na askari, wakawa wana shida na mill 3. Nikapigiwa simu na mwanangu mmoja ambaye ndio anafahamiana na hao watuhumiwa, akaniomba niwakopeshe hiyo hela kwasababu anawafahamu, ila akakataa kuwadhamini.

Na mimi nikashtuka. Ili kuepuka kugombana na jamaa yangu nikakataa kutoa pesa kwa mali kauli. Mmoja wa watuhumiwa akaomba aagize gari yake itoke mkoani ije iwekwe bond kwangu ili niwape pesa. Gari ikaja.

Nikatoa pesa, jamaa wakatoka mahabusu, tukaandika makubaliano, nikakabidhiwa gari (Toyota crown athlete mpya kabisa) na kadi yake. Mwisho wa wao kunirudishia pesa yangu ilikuwa ni juzi tar 12/08/2023. Makubaliano yanasema wakishindwa kurudisha hiyo pesa kwa wakati bila taarifa yoyote rasmi, basi gari itakuwa mali yangu. Cha ajabu ni kwamba, hadi hiyo tarehe 12 inakaribia hakuna hata mmoja kati ya wale watuhumiwa amenipigia simu! Wote wako kimya na hawapatikani! Ninayewasiliana nae ni huyu jamaa yangu tu ambaye naishi nae huku niliko, na yeye hajui kilichowasibu!

Sasa ningeweza kuwasikilizia ila hela yangu iko kwenye mzunguko, natakiwa niitumbukize mahali niongeze faida. Hapa nafanyaje wakuu? Nikijihamishia umiliki wa hii gari sitaonekana nimedhulumu? Manake wanadamu kwa nongwa hatujambo!

Naombeni ushauri.
Kimkataba ukoo sahihi kabisaa KWA upande wangu woga wako tuu......ila kibinadamu(Kiafrika) tutasema unatamaa,,huna uvumilivu n.k
Hivo kupanga ni kuchagua utakaloona ww sahihi Fanya tu
 
Honouring a contract and time sio culture ya mtu mweusi. Kila kitu kinaweza kuwa upande wako, lakini kwa kuwa nimesema hapo mtu mweusi hana utamaduni wa kuheshimu maandishi usishangae wanakufanyia tukio kwa back door.

From the beginning hukupaswa jiingiza kwa hayo mambo kabisa unless ni ndugu yako.
Duh! Kazi ipo..
 
Hapa duniani ukichagua njia ya huruma na kusaidia watu matatizo yao mwisho mwingi huwa naonaga n mbaya,n heri uchague kuwa mgumu na maisha yako waseme wanayoweza kusema kuhusu wewe ila maisha ya sasa hayana mtu mwema wengi ni wema nyusoni sio mioyoni "hata ndugu"
 
Sasa mbona wamepotea tu hewani ghaflaaa???? Hata jamaa ako hajui walipoo hakuna anaeweza acha Crown apotee hewani kisa mil 3..
Jamaa naye anadai hana clue yoyote ya whereabouts zao! Unless kama kuna kitu ananificha.
 
Hao wahuni wanasubiria uanze mchakato wa kujimilikisha ndio wakushukukie kama mwewe..

Tulia acha papara.

Jambo la msingi hapo ni kurudi kwenye makubaliano kwamba wakichelewa kurudisha hela kuwe na riba. Faida yako uipate kwenye riba. Tofauti na hapo subiri kesi itakayo kuvuruga sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kitu kama hiki niliwahi kukutana nacho. Jamaa ninayemfahamu alimleta jamaa yake aweke bond pikpik ni miaka ya 2014 hivi, mwanzoni nilikataa lakini baada ya kunushawishi kwamba anashida sana na ukiangalia nami nilitamani nipate pikipiki ya kujifunzia kuendesha nikajiingiza nikawaambia leteni kadi original na mkataba wa mauziano..

Baada ya siku mbili wakarudi tena safari hii wanamkataba wa kimchongo (haukufuata utaratibu) na kadi ya pikpiki imefanyiwa lamination,ikabidi niendelee na utaratibu tukaenda kwa mwenyekiti wa mtaa tukaandikishana nikampa laki nne awe amerudisha baada ya wiki mbili vinginevyo baada ya hapo atarudisha riba ya elfu 50 kila wiki itakayoongezeka...

Siku zikaenda wiki zikakata simuoni mtu nikaona hapa tayari pikpiki yangu hii, siku moja nakumbuka ilikuwa 24 dec 2014 nikaona nipeleke pikpik kwa fundi arekebishe kidogo na service.. simu ikaita nikaipokea, kumbe ni police wamefika nyumbani kwangu na wananituhumu kwa kumiliki pikpik ya wizi nikawaambia soon nakuja.

Nafika home nakuta defender ya police inanguruma tu ikinisubiria pamoja na noah yenye wamiliki wa pikpiki. Wenye chombo walivyoona walifurahi sana wakisema ndiyo yenyewe, ndiyo yenyewe.

Police wakaniambia pikpiki umeitoa wapi nikaambia wenye wameeka bondi.. nikaulizwa umeandikisha wapi kwa Mwenyekiti wa mtaa mkataba upo wapi nakawaletea na ile kadi pia nikaileta wakati huo yule aliyeweka bondi yupo kwenye noah na pingu ..

Nilichoka baada ya kuonyeshwa kadi ya pikpik original kumbe ile ilikuwa nifeki... kilichoniokoa ni mkataba uliomhusisha mwenyekiti wa mtaa.

Nikapelekwa central police nikawekewa mdhamana baadae..
Kesi iliendelea ila haikufika mbali bali iliishia kwenye stage ya mediation.

Nimekoma na mambo ya bondi
 
Achana na maliza watu gar ya milion 15 ndio uchukue kwa million tatu hv unajipenda kweli
 
Hao wahuni wanasubiria uanze mchakato wa kujimilikisha ndio wakushukukie kama mwewe..

Tulia acha papara.

Jambo la msingi hapo ni kurudi kwenye makubaliano kwamba wakichelewa kurudisha hela kuwe na riba. Faida yako uipate kwenye riba. Tofauti na hapo subiri kesi itakayo kuvuruga sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikienda kwenye swala la riba ndio nitaharibu zaidi kwani kwenye mkataba riba haijazungumziwa.

Hata hivyo mimi sio Taasisi ya fedha iliyosajili na kulipa kodi; hivyo siwezi kukopesha kwa riba.
 
Mkuu kitu kama hiki niliwahi kukutana nacho. Jamaa ninayemfahamu alimleta jamaa yake aweke bond pikpik ni miaka ya 2014 hivi, mwanzoni nilikataa lakini baada ya kunushawishi kwamba anashida sana na ukiangalia nami nilitamani nipate pikipiki ya kujifunzia kuendesha nikajiingiza nikawaambia leteni kadi original na mkataba wa mauziano..

Baada ya siku mbili wakarudi tena safari hii wanamkataba wa kimchongo (haukufuata utaratibu) na kadi ya pikpiki imefanyiwa lamination,ikabidi niendelee na utaratibu tukaenda kwa mwenyekiti wa mtaa tukaandikishana nikampa laki nne awe amerudisha baada ya wiki mbili vinginevyo baada ya hapo atarudisha riba ya elfu 50 kila wiki itakayoongezeka...

Siku zikaenda wiki zikakata simuoni mtu nikaona hapa tayari pikpiki yangu hii, siku moja nakumbuka ilikuwa 24 dec 2014 nikaona nipeleke pikpik kwa fundi arekebishe kidogo na service.. simu ikaita nikaipokea, kumbe ni police wamefika nyumbani kwangu na wananituhumu kwa kumiliki pikpik ya wizi nikawaambia soon nakuja.

Nafika home nakuta defender ya police inanguruma tu ikinisubiria pamoja na noah yenye wamiliki wa pikpiki. Wenye chombo walivyoona walifurahi sana wakisema ndiyo yenyewe, ndiyo yenyewe.

Police wakaniambia pikpiki umeitoa wapi nikaambia wenye wameeka bondi.. nikaulizwa umeandikisha wapi kwa Mwenyekiti wa mtaa mkataba upo wapi nakawaletea na ile kadi pia nikaileta wakati huo yule aliyeweka bondi yupo kwenye noah na pingu ..

Nilichoka baada ya kuonyeshwa kadi ya pikpik original kumbe ile ilikuwa nifeki... kilichoniokoa ni mkataba uliomhusisha mwenyekiti wa mtaa.

Nikapelekwa central police nikawekewa mdhamana baadae..
Kesi iliendelea ila haikufika mbali bali iliishia kwenye stage ya mediation.

Nimekoma na mambo ya bondi
Dah! So sad, pole sana mkuu.

Asante pia kwa ku-share experience yako. Nimejifunza pakubwa sana.
 
Walisharudi kuchukua mali yao?? Tuoe mrejesho
 
Kujimilikisha naweza kwasababu nina makubaliano (mkataba) ambao niliandikishiana nao kwa Wakili. Kitaalamu, kule TRA wakati wa transfer of ownership, badala ya mkataba wa mauziano, unawekwa huu mkataba wangu wa kukopeshana fedha kwa dhamana.

Mimi kukamatwa haiwezekani kwani nina mkataba ambao unaonyesha mmiliki halali ndio amenikabidhi gari lake kama dhamana yeye mwenyewe kwa hiari yake.

Wewe ni mjuaji sana, una leseni ya biashara ya kujope
Nikienda kwenye swala la riba ndio nitaharibu zaidi kwani kwenye mkataba riba haijazungumziwa.

Hata hivyo mimi sio Taasisi ya fedha iliyosajili na kulipa kodi; hivyo siwezi kukopesha kwa riba.

Then umeshika gari ya watu kwa sababu zipi?
 
Inaonekana un tamaa na hiyo tamaa itakudondosha ulishindwa nini kusema hauna hela ungeacha wakae huko mahabusu kwa kuwa wamejitakia wenyewe kuna misaada huwa inageuka mateso
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom