Nikiacha Pikipiki kwa muda mrefu bila kuiwasha itapata shida?

KAGAMEE

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
3,889
4,522
Habari zenu wanajamvi.

Nina pikipiki yangu aina ya SANLG huwa naitumia tu katika mizunguko yangu ya hapa na pale ila sasa nina dharula nitakaa nje ya hapa home kama mwezi na wiki mbili hivi.

Najiulza nikiipaki ndani haiwezi kuharibika kwa sababu ya kutoendeshwa muda mrefu?

Naombeni elimu juu ya hili.

Asanteni
 
Kama kilometa za service zimefika Ukirudi utamwaga oil tu mzeebaba haina shida, ifungie tu
 
Kwa Huo Muda Hakuna Tatizo Isipokuwa Battery Ndiyo Kama Haiko Sawa Sawa Mpe Mtu Aitumie Hadi Utakaporudi
 
Mwezi mmoja ni mfupi sana kwa pkpk we ifungie sepa zako ila hakikisha unafungua terminal za betry na ikiwezekana mafuta yafunge tu
 
Iwashe kwanza na baada ya kuunguruma kwa muda mfupi ifunge mafuta , lakini uiache ikiunguruma mpaka mafuta yaishe kwenye kabureta na itazima , unafanya hivyo kwa sababu mafuta yakiwapo kwenye kabureta yatasababisha jet za mafuta kuziba. Baada ya hapo fungua terminal ya -ve ya battery ya pikipiki yako. Ukirudi unga hiyo terminal fungulia mafuta washa pikipiki . Hii ni kwa uzoefu wangu wa kutumia pikipiki muda mrefu.
 
Back
Top Bottom