Nkwesa Makambo
JF-Expert Member
- Aug 26, 2011
- 4,763
- 1,321
Come on,usikimbilie kukopy nakupaste ,ni moja ya vitu nisivyovipenda.em tumia akili kidogo mkuu.ukiniita vyovyote haitanipunguzia chochote.jenga hoja acha kukopy
Hata kupata sehemu ya kucopy na namna ya kupaste tunatumia akili,Mwanasayansi wa ukweli hutoa maelezo akijiamini kujibu kila anachoulizwa kwa kuweka ushahidi inapobidi, Pseudoscientist kama wewe hujiita mwanasayansi ambaye akiulizwa swali hawezi kujibu kwa kuogopa kunasa kwenye maelezo yake, sana sana ku buy time naye anauliza swali. kujua tu kwamba wewe ni pseudoscientist ni Akili.
Sikuiti Pseudoscientist ili nikupunguzie kitu,lah ni kutaka wale wasomao na wanaokulaumu kwa kutojibu maswali yao wajue wewe ni mtu wa aina hiyo na watu wa aina hiyo huwa hawawezi kujibu maswali,isipokuwa wanaweza kuuliza maswali tu.
Kwa nini unafikiri ujuzi kwamba Mungu ndiye aliyeumba Ulimwengu na vyote vijazavyo na ndiye archtecture , designer,Engineer, Artist, na mathematician aliyeweka Constant zote ni kutokana na UOGA ? UOGA wa jambo gani ? natishwa na NANI ? kweli kauli kama hizi hazitokani na kukariri ?
Mwanadam pale anapofikiri/anapowaza kushindwa ndo anapomuumba mungu.,nilishasema katika uz flan kwamba HAKUNA USHAHIDI WA KUTOSHA KUONESHA UWEPO WA MUNGU,NA MIMI NAJUA HAYUPO,so kama we unaamini yupo lete ushahidi kithibitisha hapa
Hujielewi, unapimaje kwamba ushahidi kuhusu kitu fulani ni wa kutosha au lah ? unahitaji aina gani ya ushahidi ? huwezi kujibu swali hili kama ilivyokawaida yako,japo nina hakika hujielewi.
Angalia hoja uliyo quote hapo juu ? umezungumzia kuhusu Uoga na unazungumzia mara nyingi,umeulizwa Uoga utokane na nini,na Uoga uwe ni kwa jambo gani ? badala ya kujibu kama ulivyoulizwa umekuja na kushusha kariri zako, Pseudoscientist hujielewi tu...
Ungejielewa usingekuwa unauliza maswali na kutaka ujibiwe kama unavotaka.huku hutaki kusema unachodhan n sahihi.we ndo hujielewi na hujui kama hujielewi.,waweza niita vyovyote lakini haibadilishi ukwel
Unanihukumu sivyo,mi sijakwepa swali.Mapungufu yako unanihamishia mimi???
Mkuu kwanza asante mkuu kwa kuniweka sawa hapa.Mkanganyiko na sio kidogo Mkuu, ni watu wengi ikiwemo hata mimi kwa kipindi kirefu niliamini kwamba Lucifer ina muwakilisha IBILISI, Lakini baada ya kupitia maandiko mbalimbali na maelezo mengi ya namna kuisoma Biblia na Kuelewa ndiyo nilipoweza nami kupata ufahamu wa kwamba kumbe ni makosa ya kifasiri tu,Chanzo cha Mkanganyiko ni maandiko yaliyomo kwenye Kitabu cha Isaya 14:12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! (KJV)
Kweli Ibilisi ndiye Nyota ya asubuhi ?
Tukiyachunguza maandiko vizuri tutaona kwenye ufunuo 22:16 ''Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi''
Hivyo Bwana Yesu Mwenyewe alijitambulisha kwamba yeye ndiye Nyota yenye Kung'aa ya asubuhi.
Yapo maandiko mengine ambayo yanathibitisha kwamba Yesu Kristo ndiye Nyota ya asubuhi.
2 Petro 1:19 19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Ufunuo wa Yohana 2:28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.
Ni wazi kwamba Nyota ya asubuhi ni sifa ambayo ni ya kipekee kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kamwe haiwezi kuwa ni sifa ya Shetani/Ibilisi.
Kiini cha mkanganyiko.
Mkanganyiko umetokana na maelezo yanayopatikana katika tafsiri ya Biblia ya KJV Isaya 14:12 (Hasa katika Kiingereza ambapo limetumike neno LUCIFER) kama ilivyoelezwa hapo juu, Neno Lucifer limetumika kama utambulisho wa nyota ya asubuhi,ikiwa ni katika maelezo ambayo ukiyasoma kwa haraka unaweza fikiri yanamzungumzia IBILISI na kumpa sifa ya Nyota ya asubuhi. Hasa ukisoma Isaya14:12 kama ulivyo.
Isaya 14:12-15
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
Ukiisoma maandiko haya kwa makini utagundua si kweli kwamba shetani anapewa sifa na ukuu wa kwamba yeye ni Nyota ya Asubuhi bali ni lugha ya ''Kebehi'' dhidi ya majikwezo ya IBILISI,na kujipa sifa kwamba yeye ni LUCIFER (Nyota ya Asubuhi) na inaonyesha jinsi ambavyo kujikweza kwake kumedhiriwa hadi kushushwa chini mpaka kuzimu,wakati alijinasibu kuwa yeye atapaa kupita vipimo vya mawingu na kuwa sawa na aliye juu!
Ukitambua kwamba Lugha ilikuwa si kumsifia Ibilisi bali kubeza kujikweza kwake na kujipa sifa asizokuwa nazo utagundua kwamba bado matumizi ya neno LUCIFER kwamba ni Ibilisi yanakinzana na ukweli, kwamba alijiita LUCIFER kujikweza tu,lakini kiukweli hana sifa hizo hata chembe.
asante mkuu kwa kuniweka sawa hapa.Big up
Mkuu hawa jamaa hutoa kafara hata binadamu mkuu! Unaukumbuka ushuhuda uliotolewa na yule mchungaji baada ya Kanumba kufariki? Pia nina ushuda wa binti aliyekuwa akituumikia Freemason kwa kipindi kirefu? Kama unatumia whtsap nipe namba umsikilize huyu afu uniambie kwanini unadai freemason hawahusiki na utoaji kafara wa binadamu je nikweli
Hahahahahaaa! Mkuu post yangu umeifasiri literaly!
Naamini fremansory wanatoa kafara za watu!
In short fremanson ni wachawi kama wachawi wengine tu (wanga) tofauti yao ni kwamba fremanson wamemodify kidogo!
Ninaposema nimetumia akili yangu ninamaana nile nnachofikiria mimi(mimi kama mimi),maana yake kwamba haya mawazo ni huru sijakopy kilichowahi kusemwa mahala ama maandishi haya sio ya kukopy na kupaste.ni jinsi nionavyo mimi.
Tutaamini je uwongo?Nikikwambia hakuna Freemason East Africa utaamini??
Mkuu kule kama jeshini tu! Ukiwa kuruta kazi yako lindo but ukiwa na manyota mbona sheria nyingi hazitokufunga!!!Hakuna kafara ya Watu inayotolewa na Masonic,
Hiyo sina uhakika nayo hadi sasa! Mwenye uhakika na athibitishe!na wala KANUMBA hakuwa masons .usipagawe na stor za vijiweni
Thibitisha
Worryout Free ideas! Nakuibukia kesho!
Uwe na usiku mwema!
Free Mason ama wajenzi huru,ni jamiii ama kikundi ambacho kina misingi toka zaman sana enzi za mfalme solomon.kwa jinsi nnavojua mimi kilianzaa kama umoja wa wajenzi waliokuwa maarufu sana wakati ule hasa katika mambo.ya ramani na usanifu majengo,kikundi hiki kilikuwa namisingi yake mashariki yakati.wakati kinaanza hawakuwa na nia yoyote mbaya kama inavyosemekana sasa.
Nimetoa maelezo ya neno LUCIFER kuandikwa mara moja tena kwenye Biblia ya KJV na chanzo cha kutumiwa neno hilo nimeeleza Mkuu.
Mkuu we jua tu kuwa unapokuta mahali pameandikwa "mwenye nuru" au aliyepewa nuru" jua ni lucifer tuAma kuhusu Shetani kuitwa Lucifer nje ya mkanganyiko wa matumizi ya neno Lucifer kwenye Isaya 14:12 nakiri kwako kwamba sijui na sijawahi kusoma popote.
Mkuu wale watawala wote ambao walikua wakijikweza walikuwa wakichukua sifa za shetani kwasababu ndani yao aliyekuwa anafanya hiyo kazi ni huyo shetani,hivyo kusema aliyekuwa anaambiwa ni shetani sio kosa kwakuwa ndie aliyekuwa anafanya kazi na sio huyo mtawalaKwa kadri ya uchunguzi,pamoja na kujulikana kupitia Isaya 14:12 kwamba Shetani aliitwa Lucifer kutokana na kujisifu kuwa ni mkuu hana aliye mkuu chini hata juu,japo kwa kurejea Isaya 14:4, tunaona Isaya allitumwa kutengeneza Methali kwa ajili ya Mtawala wa Babeli aliyekuwa na majivuno na kiburi dhidi ya Mungu. Hivyo yawezekana sana kwamba Lucifer aliyekuwa anazungumziwa na kukebehiwa kwa mafumbo na Nabii Isaya ni Mtawala wala Babeli,binadam mwenye mwili na si Shetani.
Mkuu hapo pia kuna jamboYah, Mkuu kwa kutafsiri neno Morning,kiswahili unaweza kusema Alfajiri au asubuhi na ukawa sahihi kwa tafsiri zote.
Nikweli ngoja nikaangalie kwenye kumbukumbu zangu na nitakuja kukuhabarisha mkuu!Mkuu nashauri tuendelee kuchunguza maandiko, ili tujue ukweli usio na mawaa, lakini kumbuka nimeeleza hapo juu kwamba Neno Lucifer limeandikwa mara moja tu ndani ya Biblia,tena kwenye Biblia tafsiri ya KJV kwenye Isaya 14:12 tu. Labda kama kuna sehemu nyingine ambayo unajua Ibilisi au Shetani ameitwa Lucifer nitafurahi kujifunza...