Poleee, ID/Account umefungua usiku saa tatu, Huu uzi umeuandika usiku huu saa tisa kamili, ngoja tukusubr mpk asubu ukanushe au laaa.... pengne unaota au n haya masimu ya tecno umelilalia limeshafungua ID lenyewe likacopy mavitu kutoka FB au kweny Msg za kawaida likaingia Jf likapest lika post, maana inaonesha umepost tu n kama lijisaa limepita hukurud tena hewan, Au ndo umepata usingz? M mwenyewe sidaiwi wala sina stress zozote lakn nimekosa ka usingz sembuse mtu anaefikiria kufaaa?
Kama n kweli, Pole sanaaa kwan huna assets zozote zinazofka hio 25M Au kukaribia? Mda wa kulipa deni kwa hiari walikupa na umeshapita? umejarb kuongea nao kwa busara ukawaeleza nia yako ya kulipa? huwez huko huko bank ukafanya kaz bure kwa mda utakaofidia hilo deni?
M25 si haba kama huna hata mia na huna mzunguko wa kuipata, ila huwez ilinganisha na uhai wako dada, una uhakika wapo serious wanataka wakufunge?
Mana Hakuna watu wenye mikwara kwenye kudai kama bank, wakikukopesha au wakikuomba ukope wanakuletea vijidada vizurii vinawaka waka, sauti nyororo, ngozi chocolate wanakubembeleza mpk ukubali kuchukua mkp mwenyewe,
Wakija kudai sasaaa.... Unaletewa njemba imefumuka usoo. Nyeusi tiii huku imevaa miwani inafunika mpk matundu ya pua, suruali kama pajama, chini bonge ya buti au raba kama za kangi, ikiingia inakua na mbwembwe na mikwara, yaan mnasalimiana huku anazima switch ukutani huku anachomoa cable za tv, fridge, extensions n.k tena anafanya kuvuta(Anashikia kule kwenye kichwa anavuta) huku anasunya, ukiangalia huo uso unaosunya waweza usahau mpk kiwango cha deni na benk uliyokopa
Unasema atakae kusaidia utampa chochote atakachotaka,
My dear sister hicho chochote baadae inaweza iwe mthan zaid ya huu utaman ukakope tena bank hata mara mbili ya hio ulipe kuondokana na chochote,
Binafsi mimi na hvyo sina familia bd, ningetoroka kwanza nikaanze kuzisaka, Kama kuna watakachofanya huko nyuma poa tu, LAWAMA HAPEWI MBUZI, siku nazipata nawaletea kwa suprise uone kama watakusumbua,
Wazee tujifunze kitu hapa, usikubar kutoka kapa