Swali kwaza: Je, hivi bank kukuwekea pesa katika account yako then ukazitumia, sheria inasemaje hapa?! Maana cha kuokota si cha kuiba, wewe umeikuta katika account yako na hukuomba kuwekewa, shida mwanaharamu, umezitumia iwaje sasa wakuulize tena na haukuwaomba?!
Swali la pili: Wewe na bank mliingia mkataba gani juu ya hizo million 25?! Je walikukopesha, ulifanya overdraft, au ilikuwaje, ni mkataba gani ambao umevunja juu ya hizo 25 million hadi wakupeleke mahakani kuzidai....maana hii ni kama uokote bahasha ya mamilioni usijue ni ya nani kisha ukaamua kuitumia then atoke mtu aseme ni zake na atake kukushtaki ili kuzidai, sasa anakudai kwa makubaliano yapi, alikukopesha au alikuazima, kwa mkataba upi nauliza?!
Swali la tatu: Sheria za wafanyakazi wa bank zinasemaje juu ya negligence ya wafanyakazi wao pale wanapofanya uzembe kama huu wa kudeposit pesa kwenye account ya mtu ambaye hausiki na pesa?!
Swali la nne: Bank huwa zinaweka insurance cover kwenye pesa zake, je inapotokea tukio kama hili, bank wanapata hasara kweli, sio kwamba hapa insurance wanalipa hizi hasara
Swali la tano na la mwisho: Je, hawa watu 25, utawalipaje na wote wakitaka pesa zao kwapamoja?!