Mkuu hamia mbeya tena nakushauri nenda Tunduma.Nakushauri uende huko kwa sababu zifuatazo
1:Hakuna ukabila kwenye ile boda,watu hawashughuliki kujua wewe ni nani na umetoka wapi,wapo bize na kutafuta pesa.Arusha kuna ukabila kiaina,ikiwa wewe si mzawa wa kaskazini itakuchukua muda kutengeneza chaneli hususani za biashara.
2:Ukiwa Tunduma utakutana na watu wa mataifa mbalimbali ambao wanafanya ujasiriamali wa kuuza na kununua bidhaa kama vile samaki,mahindi,ulezi nk kwa mtaji mdogo unaweza ukaanza na baadaye ukakua taratibu.Arusha fursa kama hizo zimebanwa sana.
Ikiwa utakua kimtaji na ukawa unaishi mbeya ni rahisi ukanunua mazao ya chakula na kupeleka Arusha kuuza,ukiwa Arusha huwezi kununua mazao kule na kupeleka Mbeya.
4:Watu wa Mbeya ni wakarimu kuliko wale wa Arusha,ni rahisi kupokelewa Mbeya hata na watu wasiokujua na ukaishi nao na kufanya mambo yako.Arusha ni ngumu kupokelewa kirahisi hususani kama sio mwenye asili ya kaskazini mwa Tanzania