Nifanyeje, naombeni mawazo yenu

Nifanyeje, naombeni mawazo yenu

Director-k

Member
Joined
Mar 12, 2014
Posts
88
Reaction score
26
Nimeanzisha mahusiano ya uchumba na binti na tuna muda kama mwaka mmoja.

Siku moja katika maongezi yetu nikamdadisi vya kutosha kuhusu suala la afya akafunguka mengi sana. Baadhi ya matatizo aliyonayo ni athma, madonda vya tumbo na mengine siwezi kuyasema kwa kulinda maadil ya JF.

Mwanzoni nilikua tayari nishamuahidi nitakua nawe kwenye shida na raha.
Sasa kulingana na matatizo aliyonayo mi naogopa kumuoa.

Tayari nishajitambulisha kwao na yeye kwetu wanamfahamu na ameshakataa wachumba kwa kunisubiria mimi.
Je nifanyeje? nisaidieni mawazo tafadhali.
 
1409123444261.jpg
Ntarudi
 
Nimeanzisha Mahusiano Ya Uchumba Na Binti Na Tuna Muda Kama Mwaka Mmoja. Siku Moja Ktk Maongez Yetu Nikamdadis Vya Kutosha Kuhusu Suala La Afya Akafunguka Meng Sana, Baadh Ya Matatizo Aliyonayo Ni Athma, Madonda Ya Tumbo Na Mengine Siwez Kuyasema Kwa Kulinda Maadil Ya Jf. Na Mwanzon Nilikua Tayar Nishamuahid Ntakua Nawe Kwenye Shida Na Raha.
Sasa Kulingana Na Matatizo Aliyonayo Mi Naogopa Kumuoa. Na Tayar Nshajitambulisha Kwao Na Yeye Kwetu Wanamfaham Ma Ameshakataa Wachumba Kwa Kunisubiria Mimi.
Je Nifanyeje?? Nisaidien Mawazo Tafadhal

Hapo kwenye madonda ya tumbo n.vidonda vya tumbo.halaf pia wewe ulishaahid kua nae kwenye shida na rah sasa mbona hapa kwenye shida unamkimbia mapema?????? Imagine ndo wewe unafanyiwa haya tafteni sulihu ya hayo yanayomsaidia kumucha sio suluhisho
 
kaka ushukuru sana umepata mtu ambae amekwambia ukwel kuhusu matatzo yake........
kaa chini ufanye maamuz sahih
 
Amefanya makosa kukwambia kweli? je angedanganya ukaja kuona baada ya kumuoa? unampenda kweli? na hayo maradhi yake ni makubwa sana kiasi ambayo hayatibiki? ulishamuona dr kujua athari zake ni zipi na ni stage gani ilofikia?
 
Cc @Exel, tabibumtaratibu, miss chagga, Khantwe,Miss neddy Heaven on Earth, miss strong, REALITY embu mashaurini huyu afanyeje!

Kuna wakati huwa nawaza role ya wazazi katika kutuchagulia wachumba, ni ya msingi sana!

Vijana wa leo tumekuwa wajinga wenye elimu, kila kitu twajifanya twaweza tu! Enzi hizo wachumba walipokuwa wanachaguliwa na wazazi, factor kama hizi zilikuwa zinaangaliwa sana!!!

As long as umempenda na ulimuahidi, chukua mzigo wako!
 
Usikimbie matatizo mkuu yatatue ....unaweza ukamwacha ukapata mwngine asikwambie ukweli na ukakuta ana matatizo au magonjwa nakubwa zaid ya hayo istoshe hayo maginjwa ulio taja hapo yoote yanatibika

Chinekeeeeeeee
 
Napia amemuambia ukweli na yeye alimuahidi kuwa atakua nae kwenye shida na raha sasa abebe tu mzigo kwani maradhi kaumbiwa binadamu.
Kuna wakati huwa nawaza role ya wazazi katika kutuchagulia wachumba, ni ya msingi sana!

Vijana wa leo tumekuwa wajinga wenye elimu, kila kitu twajifanya twaweza tu! Enzi hizo wachumba walipokuwa wanachaguliwa na wazazi, factor kama hizi zilikuwa zinaangaliwa sana!!!

As long as umempenda na ulimuahidi, chukua mzigo wako!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom