Nisaidieni Kumpa Ushauri Huyu Jamaa

Nisaidieni Kumpa Ushauri Huyu Jamaa

rama halavi

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2015
Posts
269
Reaction score
236
Habari za Leo Wana Jamii Forum Wenzangu? Natumaini Wikiend imeanza vizuri kwenu na jumamosi inaenda poa.

Naombeni msaada wa mawazo yeni ili nimshauri huyu jamaa yangu ambaye amepatwa na jambo ambalo linamvuruga akili na moyo wake.

Miezi 2 iliyopita rafiki yangu mmoja alianzisha mahusiano na binti mmoja ambaye waliridhiana na kukubaliana kuwa wapenzi na jamaa alimwambia lengo lake ni kumuoa itakapofika mwakani na walikubaliana mwisho wa mwaka huu yule binti atapoenda kwako kutembelea familia basi awajulishe familia yake kuhusu jamaa na lengo lake na atapopewa jibu basi amjulishe ili jamaa aongee na familia yake wafanye taratibu za kupeleka barua ya uchumba na taratibu zingine zifuate.
Mahusiano yakawa poa tu na mwanamke alionyesha kweli mapenzi ya dhati, kujali, kuheshimu na kuthamini na wakapanga future yao pamoja katika mambo mengi. Jamaa ni muislamu na mwanamke ni mkirsto lakini mwanamke aliridhia na kukubali kubadili dini. Mwanamke ana wivu sana maana ilifika siku akawa anachukua simu ya jamaa anakaa nayo hata siku 3 ili kumchunguza na kwakuwa jamaa sio player hakuwa na mashaka na hili na pia kuna wakati mwanamke akawa akienda ofisini kwa jamaa anamuachia simu yake yeye na kuondoka na kuifata baadae. Mwanamke kwa umri ni miaka 19 anaishi na dada yake mkubwa na anadai dada yake ni mkali sana na jamaa anamjua huyo dada na wana urafiki wa salamu tu. Dem anajishughulisha na ushonaji wa nguo, Ni mwanamke anayejiheshimu na kujitambua na pia sio mchunaji maana alikuwa akiomba pesa basi anaomba hela ya kusuka 2000 au 5000, hela ya vocha, pedi au manukato na vitu vidogo vidogo. Kwa kifupi demu sio mtu wa tamaa.

Matatizo yalianza siku ambayo mwanamke alimpigia simu usiku jamaa kama kawaida ya wapenzi kuongea na simu na katikati ya maongezi demu alionekana kama hayuko sawa na jamaa alipouliza akaambiwa kwanza kabla hajaambiwa nini tatizo amuahidi mwanamke kwamba hatomuacha. Jamaa akaahidi hatomuacha na mwanamke akafunguka kwamba huko nyuma alikuwa na mwanaume na huyo mwanaume ni mganga. Sasa mwezi na nusu uliopita yule mganga alimpigia simu na kumwita sehemu na kula nae yamini ya kutoachana. Mwanamke anasema alifanya hicho kitu ila sio kwa akili yake timamu na anajutia sana hicho kitu maana ameambiwa akikiuka masharti kitu kibaya kitamtokea. Jamma bado akasimamia lengo la kumuoa maana mwanamke alimuhakikishia kuwa hampendi tena huyo mganga na yuko tayari kuolewa na yeye pindi muda ukifika.

Mahusiano yakaendelea kama kawaida ila jumatano ya wiki iliyopita mchana waliongea fresh mpaka jioni ila ilipofika usiku demu alimpigia simu jamaa na kumwambia simu yake amechukua dada yake so asimpigie akirudishiwa simu atamtafuta yeye.

Baada ya siku 2 jamaa akona kimya akaamua kumtafuta mmoja wa ndugu yake huyo demu na kweli alimuhakikishia kuwa demu alinyang'wanywa simu ila karudishiwa asubuh ya leo na alipomuuliza nduguye kama anajua hilo swala la mganga akasema anafahamu na hawana cha kumshauri maana mwenye maamuzi ni yeye mhusika.
So jamaa akampigia simu demu wake kutaka kujua tatizo nini ila haikupokelewa na alipotuma sms pia hazikujibiwa.
Usiku jamaa akampigia tena demu ila hakupokea so akamuomba ndugu wa yule demu amuulizie tatizo nini mpaka demu hapokei simu za jamaa wake, alichojibiwa ni kwamba demu amesema muachane na umtoe kwenye mipango na moyoni mwako basi bila kupewa sababu ya maana ya kuachana kwao.
Jamaa kila akijitahidi kuuliza apewi jibu la maana na mwanamke ghafla amebadilika na amempiga marufuku jamaa asimpigie simu wala kumtumia sms.
Sasa juzi demu kampigia simu jamaa na kudai anamsalimia tu ila akiulizwa sababu za kuachana hataki kusema na demu akikutana na jamaa njiani anajificha. Ila jana usiku demu kaenda ofisini kwa jamaa kupata huduma ya kuingiziwa nyimbo kwenye flash maana jamaa ana ofisi yake ya kuwaingizia watu nyimbo na movi. Demu kakaa nusu saa halafu kaingiza nyimbo 4 tu na jamaa alimuomba wakae sehemu waongee demu akasema hana muda.

Jamaa anashindwa kumuelewa huyu demu na anampenda sana na alikuwa na nia ya kweli ya kumuoa hapo mwakani.

Kinachomuumiza kichwa ni kuachana kwao kirahisi rahisi bila sababu inayoeleweka. Maana anahisi kama sio hilo swala la uganga basi atakuwa kapigwa marufuku na dada yake kuhusu hayo mahusiano na jamaa maana dada mkubwa kuna vitu aliviona na kuviulizia kama simu ya jamaa alipokuwa nayo demu kwa siku 3 na pia picha za ofisi kwa jamaa alizopiga demu na ndugu yake.
Pia kwa upendo aliokuwa anauonyesha mwanamke kwa jamaa na alivyokuwa anajieleza kihisia huyu demu kwa jamaa anaona sio rahisi vyote vipotee haraka hivyo. Sometimes demu akiamka tu alfajiri anampigia simu jamaa waongee ndio aende akafanye usafi wa ndani kwao. Jamaa kila akijiuliza yote hapati jibu na demu hataki kufunguka.

Hebu vaa viatu vya ushauri na unisaidie kumuelewesha huyu jamaa wangu.
Nakutakieni Weekend Njema
 
Sijataka kufika hadi mwisho wa uzi. sababu tayari jamaa yako kaisha pewa. si ameambia demu alikwenda kuila amini na x-wake, hiyo tu inamaanisha hakuwahi kuachana na mganga wake.

Hivi rafiki yako ana miaka mingapi?
 
Mwanamke mwenyewe ana miaka 19!
mwambie aachane naye atamsumbua bure hata aking'ang'ana kumuoa.....

Asubiri akue vizuri au atafute MTU mwingine angalau mwenye 23+
 
Huyo manzi ni mzinguaji chalii apige chini kuna watoto waelewa zaidi ya huyo atapata.

Kama anataka usumbufu kwenye maisha ya baadae amuoe. Siku ingine zingatia taratibu za kiuandishi
 
Mwanamke mwenyewe ana miaka 19!
mwambie aachane naye atamsumbua bure hata aking'ang'ana kumuoa.....

Asubiri akue vizuri au atafute MTU mwingine angalau mwenye 23+

Zaidi ya ushauri huu itakuwa kupoteza muda. Na upo uwezekano umri wa mshikaji nae unasimama mitaa hiyo hiyo, ndio maana kila kitu kwao shida.
 
Demu hana future na wewe.. achana nae kata nae mazoea kabisa mkuu
 
Huyo manzi ni mzinguaji chalii apige chini kuna watoto waelewa zaidi ya huyo atapata.

Kama anataka usumbufu kwenye maisha ya baadae amuoe. Siku ingine zingatia taratibu za kiuandishi
Nimekusoma Chalii na ntajitahidi kuzingatia kanuni za uandishi
 
b41761e0884d61ab0ef5f35afd19cec0.jpg
 
Jinsi ulivyoeleza, hii history inakuhusu wew mwenyew. Usiogope kudate na watoto was shule ni tabu, ndo maana wakibendishwa mkulu anasema wabaki home. Period.
 
Tatizo dini.

Na huyo mtoto kazuiwa na dada yake.
 
Jinsi ulivyoeleza, hii history inakuhusu wew mwenyew. Usiogope kudate na watoto was shule ni tabu, ndo maana wakibendishwa mkulu anasema wabaki home. Period.
Tofauti ya uandishi isikufanye uamini unachosoma. Mimi sio muoga wa msaada ninapohitaji na kama ni kweli inanihusu ningesema. Jaribu kutizama thread zangu zinazonihusu huwa sifichi.
 
Mwanamke mwenyewe ana miaka 19!
mwambie aachane naye atamsumbua bure hata aking'ang'ana kumuoa.....

Asubiri akue vizuri au atafute MTU mwingine angalau mwenye 23+
Under 25 wengi ni pasua kichwa
 
Duh lakini mwanzo wa stori si ulisema kwamba bi dada anajitambua, utambuzi ulikuwa temporarily au?
 
Back
Top Bottom