Nifanyeje Kupunguza Gharama za Milango?

Nifanyeje Kupunguza Gharama za Milango?

Ukileta ubahili kwenye mlango utatengenezewa mihumula utafurahia show yake😂
Nipo Makini Mno Mkuu sikurupuki na sitojaribu.

Najua kabisa hili eneo lazima maumivu nipo hapa kuona kama kuna ahueni naeza pata.
 
Hii pia ni mti mizuri tunaitumia sana Tanga ...Tatizo sio mepesi mlango unakuwa mzito .
Ukipata mbaya unakosa pattern nzuri hata upige randa vip ,unaona kama unabaki na madoa madoa.
Napenda Milango Mizito ila sio mizito ambayo Mchwa anapita nooo
 
kama una jamaa kati ya tabora, goweko na mpanda jaribu kumcheki maana kwa maeneo hayo milango ya mninga/mkongo/mkurungu inapatikana kwa bei rahisi sana na taratibu za usafiri unatumia trc ambao bei yao ni ndogo sana.
Sina Mkuu natamani kaama ungeweza nisaidia eneo hili ningeshukuru sana.
 
Katika Maeneo yananipasua Kichwa eneo la Finishing ya nyumba ni Milango.

Yani kuna wakati natamani kuweka hata mabati, ilimradi Mlango

Naomba Wazoefu eneo hili mnisaidie Huwa mnafanyaje mkifika eneo la KUWEKA milango nyumba.

Gharama za mlango Mmoja Wa Mbao ya Mkongo inafika hadi 1m na zaidi.

Nyumba yenye Milango 6 maana yake inatoka sio chini ya 6m.

Hapo Hujaenda GETINI kuandaa GETI...

Upande Wa GETI huwa sipati shida kwani najiandaaga kwa Kununua MABATI,Square Pipe,vinatulia kusubiri Muda napata hela kisha naita Fundi Geti linapatikana.

Kwenye MILANGO naombeni mnisaidie mawazo mliyotumia

Binafsi nawaza kukusanya mbao kama mbao kisha baadae nije tengeneza Mlango, Hii imekaaje kuhusu Ubora na Gharama ndugu zangu,kuna kitu ntaokoa au ni yale yale?

Kuna milango ya Chuma Naombeni msiiiweke katika OPTIONS naombeni mnisaidie kuokoa gharama kwenye Milango ya Mbao tu.

Kama Kuna Fundi Pia au Muuza Mbao naomba ajitokeze, Msaada wenu tafadhali.

View attachment 3330414
Weka milango ya kuingilia ndani tuu yaani wa mbele na nyuma then ingia. Taratiiibu ukipata pesa utaweka ya vyumbani wkt huo umeweka hata mapazia tuu. Kikubwa upo kwako mzee.

na nyuma k
 
Weka milango ya kuingilia ndani tuu yaani wa mbele na nyuma then ingia. Taratiiibu ukipata pesa utaweka ya vyumbani wkt huo umeweka hata mapazia tuu. Kikubwa upo kwako mzee.

na nyuma k
Ni sawa Mkuu...

Sina haraka kabisa kuhusu kuingia ndani maana hata nilipo sigharamiki.

Natamani tu kupunguza Cost hata kama ntatengeneza mlango mmoja mmoja lakini iwe yenyewe.
 
Kwa uzuefu wangu wa kuwa karibu na wauza mbao na mafundi furniture una options 2,

1.utafute mbao tofauti na mninga,wengi tumeaminishwa kuhusu mninga lakini kuna mbao kama mtondoro,mtiki,mvule na mkangazi, hizi zina bei nafuu ukilinganisha na mninga,ukipata fundi anafanya finishing vizuri na mbao iliyokauka vizuri hakika utaufurahia uo mlango.

2.option nyingine ni hii,unaweza ukanunua mbao za mninga zilizotumika(vitanda vya zamani, kabati na milango ya zamani ya mninga), ukachukua hizo mbao ukapeleka mashine zikasafishwa na kutengeneza mlango mwingine kwa style unayoitaka wew,hii pia mpka ikamilike ni 200k-350k

Kazi kwako
 
Ni sawa Mkuu...

Sina haraka kabisa kuhusu kuingia ndani maana hata nilipo sigharamiki.

Natamani tu kupunguza Cost hata kama ntatengeneza mlango mmoja mmoja lakini iwe yenyewe.
Kama milango ya nje iko makini ile ya ndani hata makapi fresh ...Mimi mwezi wa sita naweka milango ikiwa ni hatua ya mwisho ,Bajetu ni mil 2.3 kwa milango sita ,mbao mitatu na aluminium mitatu ,bei ya aluminium ni 350k ya mbao sijajua ila nitachukua hata makapi ...Geti mbili kubwa tayari kitambo.
1000071942.png
 
Ni aina ya mllango fulani ambayo imetengenezwa na material ya chuma na bati na ukiweka hautahitaji kuweka mageti au grill. Pia Ina muonekano mzuri sana inapatikana kwenye hardware kubwa kariakoo. uliza security door za nje watakuonyesha.
Vipi kuhusu gharama zake mkuu ni affordable au?
 
Kwa uzuefu wangu wa kuwa karibu na wauza mbao na mafundi furniture una options 2,

1.utafute mbao tofauti na mninga,wengi tumeaminishwa kuhusu mninga lakini kuna mbao kama mtondoro,mtiki,mvule na mkangazi, hizi zina bei nafuu ukilinganisha na mninga,ukipata fundi anafanya finishing vizuri na mbao iliyokauka vizuri hakika utaufurahia uo mlango.

2.option nyingine ni hii,unaweza ukanunua mbao za mninga zilizotumika(vitanda vya zamani, kabati na milango ya zamani ya mninga), ukachukua hizo mbao ukapeleka mashine zikasafishwa na kutengeneza mlango mwingine kwa style unayoitaka wew,hii pia mpka ikamilike ni 200k-350k

Kazi kwako
Option ya Pili ni nzuri shida ni pakupata hiyo milango ya zamani ya mninga
 
Mbao za mninga hazipatikani kwani mbona sioni anaekuka hata na wazo la kununua MBAO?
 
Ndio mana nawambiaga watu Mbao zipo nyingi lakini MBAO MBAO iliyokauka ikakauka vyema.

Hauna Cha Maji wala Hauna mchwa wala kusinyaa na kutanuka hamnaa

MNINGA uliokauka vyema ukapgwa Finishing nzuri, unaweza hata ukaoga nao.
Kabisa mwanawane...mkongo ndio mbao yenyewe ila ndio hivyo miliion moja mlango mmoja.
 
Mlango mzuri 120k
Fremu ngumu ambayo hailiwi na mchwa 120k

120 +120 = 240
240 x 6 = 1.4 M

Hiyo m6 imetoka wapi?
Naongelea hizo bei nipo dar
Weka kitu kulingana na uwezo labda unataka Ile milango ya show ya gharama kubwa
 
Funga shuka ya nini ujitese na pesa ya milango huna..!! 😹
 
kama una jamaa kati ya tabora, goweko na mpanda jaribu kumcheki maana kwa maeneo hayo milango ya mninga/mkongo/mkurungu inapatikana kwa bei rahisi sana na taratibu za usafiri unatumia trc ambao bei yao ni ndogo sana.
Nakubaliana na ww,mwakajana nilikuwa mpanda Wana milango mizuri sana.nilikuwa nawaza tu namna ya kusafirisha.
 
Toka ujenge chumba kimoja cha giza tayari ushakuwa engineer…!! 😹😹
Kwenda huko kenge weee. Wee ujenzi utaulia wapi story zako kila leo ngono tuu. Tua he sie ma engineer wazee wa concrete, slap, footing. Gypsum, plumbing vyote vipo kicheani yaani ata .umeo akitaka jenga ghorofa niite nisimamie alafu nikui amishe ndani ya boma nikulambishe kibamiaz 😜
 
Back
Top Bottom