Nifanyeje Kupunguza Gharama za Milango?

Nifanyeje Kupunguza Gharama za Milango?

Ni aina ya mllango fulani ambayo imetengenezwa na material ya chuma na bati na ukiweka hautahitaji kuweka mageti au grill. Pia Ina muonekano mzuri sana inapatikana kwenye hardware kubwa kariakoo. uliza security door za nje watakuonyesha.
Nmeijua Mkuu, ile milango ya Bati Hapana Mkuu yani BATI ni BATI hata liwekweje.

Kwa usalama nakubaliana na wewe ila kwa muonekano Mkuu Status ya MBAO sidhani kama Chuma itakuta.

WEzi wa siku hizi wame Advance hawatumiii tena Milango wanaptia madirishani na hivi watu wanaweka vi Aluminium na vi grill la square pipe chache yani Madirishani ndio Loophole nyingi zilipo kwa sasa.
 
Wahindi mbona hawawazi haya mambo ya milango. Na wanaenjoy maisha kwenye nyumba za msajili
Usifikiri nao wanafurahia yale maisha ya kujibana kwenye maeneo finyu vile. kasome kwanza historia ya hizo nyumba za msajili utajua kwanini wahindi wa kale walijenga nyumba na hawa wa leo hawajengi.
 
Nmeijua Mkuu, ile milango ya Bati Hapana Mkuu yani BATI ni BATI hata liwekweje.

Kwa usalama nakubaliana na wewe ila kwa muonekano Mkuu Status ya MBAO sidhani kama Chuma itakuta.

WEzi wa siku hizi wame Advance hawatumiii tena Milango wanaptia madirishani na hivi watu wanaweka vi Aluminium na vi grill la square pipe chache yani Madirishani ndio Loophole nyingi zilipo kwa sasa.

Unaishi maeneo gani wewe?
Wizi kama huo haupo sikuhizi.
Ni ngumu kumzuia Mwizi akiamua .
Wezi wakiamua wanaingia na wewe ndani hawana muda wa kuvunja mlango.
Ndio maana sikuhizi inashauriwa kuweka Kamara za ulinzi ili kuweza kuwatrack wakifanya tukio, na wewe mwenyewe kumiliki silaha ya moto ili kujilinda
Kuzungushia nyumba fensi
 
Hauhitajiki,
Huyo kaleta mbwembwe nenda kwa mafundi welding hata hapo mtaani kwako.
Watakuundia hiyo milango fresh tu watakutajia vitu vya kununua masheet ya chuma,frem za chuma square pipes unaenda gerezani kariakoo unanunua (kama upo dsm) kama mikoani kwenye mahardware watakuwa wanauza.
ma sheet milango yameshatengenezwa yanaurembo unachagua urembo unaotaka
unanunua kitasa unachotaka .
Hao mafundi wa welding watakuja kukutengenezeq huo mlango hapohapo nyumbani kwako .
Mimi ninaunda huo mlango kwa ajili ya apartment ya kupangisha niliyoimalizia nimeambatisha picha chini
Gharama za material laki 380,000 ufundi pamoja na kuufitisha 200,00.
Mlango wa urefu na upana gani huo kwa material hayo.

Hebu picha za matokeo baada ya mlango huo kukamilika unategemea picha yake kuwaje? Naomba picha tafadhali na ikikupendeza ntaomba picha za huo mlango unaoutengeneza pia baada ya kuisha.
 
Wee labda uliweka mlango wa mbao ya muembe uliopakwa polish 🤣🤣🤣🤣
Ndio mana nawambiaga watu Mbao zipo nyingi lakini MBAO MBAO iliyokauka ikakauka vyema.

Hauna Cha Maji wala Hauna mchwa wala kusinyaa na kutanuka hamnaa

MNINGA uliokauka vyema ukapgwa Finishing nzuri, unaweza hata ukaoga nao.
 
Katika Maeneo yananipasua Kichwa eneo la Finishing ya nyumba ni Milango.

Yani kuna wakati natamani kuweka hata mabati, ilimradi Mlango

Naomba Wazoefu eneo hili mnisaidie Huwa mnafanyaje mkifika eneo la KUWEKA milango nyumba.

Gharama za mlango Mmoja Wa Mbao ya Mkongo inafika hadi 1m na zaidi.

Nyumba yenye Milango 6 maana yake inatoka sio chini ya 6m.

Hapo Hujaenda GETINI kuandaa GETI...

Upande Wa GETI huwa sipati shida kwani najiandaaga kwa Kununua MABATI,Square Pipe,vinatulia kusubiri Muda napata hela kisha naita Fundi Geti linapatikana.

Kwenye MILANGO naombeni mnisaidie mawazo mliyotumia

Binafsi nawaza kukusanya mbao kama mbao kisha baadae nije tengeneza Mlango, Hii imekaaje kuhusu Ubora na Gharama ndugu zangu,kuna kitu ntaokoa au ni yale yale?

Kuna milango ya Chuma Naombeni msiiiweke katika OPTIONS naombeni mnisaidie kuokoa gharama kwenye Milango ya Mbao tu.

Kama Kuna Fundi Pia au Muuza Mbao naomba ajitokeze, Msaada wenu tafadhali.

View attachment 3330414
Mkuu kama nyumba hii inayoonrkana ni yako basi huwezi kushindwa kununua mlango wa laki nane
 
Mm nakushauri ukomae tu ili uweke Milango imara wa Mbao.

Sijui uko stage gan sasahivi kwenye hiyo milango.
ila kwa kawaida huwa Anza na kuweka frame nzur ya Mlango wa mbele na nyuma.
Hii wastan ni 200k kwa fremu kwa kila mlango.

Vuta pumz , then weka frame za ndan kuingilia chumban. Hii bei inakuwa 150k coz frem hizi sio nene kama za milango ya mbele na nyuma.

(milango ya choon weka aluminium door - 250k -300k kwa mlango ).

Ukimaliza hapa milango ya ndan weka temporary au hata wa mbele unaweza weka hivi maana si kuna Grill. Alaf ukiwa na nguvu sasa unabadilisha mlango mmoja mmoja kuweka ile mbao nzur na design nzur inayokupendeza.

All in all ni kwamba Usiteseke kufanya milango yote kama huna hela.
Anza fremu, then tulia.
 
Unaishi maeneo gani wewe?
Wizi kama huo haupo sikuhizi.
Ni ngumu kumzuia Mwizi akiamua .
Wezi wakiamua wanaingia na wewe ndani hawana muda wa kuvunja mlango.
Ndio maana sikuhizi inashauriwa kuweka Kamara za ulinzi ili kuweza kuwatrack wakifanya tukio, na wewe mwenyewe kumiliki silaha ya moto ili kujilinda
Kuzungushia nyumba fensi
Nakubaliana na wewe Mkuu, Hivi vitu tunaweka ili tu kukamilisha nyumba tusiingie gharama tena na tena lkini sio swala la security.

Mwizi/Jambazi Hazuiliki akiamua
 
Mkuu kama nyumba hii inayoonrkana ni yako basi huwezi kushindwa kununua mlango wa laki nane
Sio Yangu Mkuu ila Muonekano wa Yangu utakua hivyo ikikamilika.

Swala sio UWEZO mkuu, mbona tunapoteza pesa kila siku kufanya anasa na vitu vya kufurahisha Nafsi zetu?

Hapa Swala ni Angalau basi badala ya kuntoka 1.4 ya Mlango wa ndani na 2m ya Mlango wa Mbele ishuke iwe angalau hata 800k kwa milango ya ndani na 1.5m kwa Entrance Door.

HEla zenyewe za kuunga unga sana Mkuu sana sana sana uje uitoe yote kwa Mlango m1 tu asee inatia mawazo.
 
Mm nakushauri ukomae tu ili uweke Milango imara wa Mbao.

Sijui uko stage gan sasahivi kwenye hiyo milango.
ila kwa kawaida huwa Anza na kuweka frame nzur ya Mlango wa mbele na nyuma.
Hii wastan ni 200k kwa fremu kwa kila mlango.

Vuta pumz , then weka frame za ndan kuingilia chumban. Hii bei inakuwa 150k coz frem hizi sio nene kama za milango ya mbele na nyuma.

(milango ya choon weka aluminium door - 250k -300k kwa mlango ).

Ukimaliza hapa milango ya ndan weka temporary au hata wa mbele unaweza weka hivi maana si kuna Grill. Alaf ukiwa na nguvu sasa unabadilisha mlango mmoja mmoja kuweka ile mbao nzur na design nzur inayokupendeza.

All in all ni kwamba Usiteseke kufanya milango yote kama huna hela.
Anza fremu, then tulia.
Frem Mkongo Frem kama Frem hujagusa Mlango ni 450k Mkuu.

Frem ya 200k Mkongo labda Ipo ila sio kwa milango yangu na ukubwa na unene ninaotaka.

Wazo la kununua mbao kama mbao je,lipoje?
 
Frem Mkongo Frem kama Frem hujagusa Mlango ni 450k Mkuu.

Frem ya 200k Mkongo labda Ipo ila sio kwa milango yangu na ukubwa na unene ninaotaka.

Wazo la kununua mbao kama mbao je,lipoje?
Uko Dar sehem gan? Nikuelekeze sehem!
 
Frem Mkongo Frem kama Frem hujagusa Mlango ni 450k Mkuu.

Frem ya 200k Mkongo labda Ipo ila sio kwa milango yangu na ukubwa na unene ninaotaka.

Wazo la kununua mbao kama mbao je,lipoje?
Mkaratusi na mvule vip?
 
Kusema ukweli maishani mwangu sijawahi fanya kazi ya mbao tofauti na Mkongo.

Imani yangu imejengeka kwenye MKONGO tu na si mti mwingine
Hii pia ni mti mizuri tunaitumia sana Tanga ...Tatizo sio mepesi mlango unakuwa mzito .
Ukipata mbaya unakosa pattern nzuri hata upige randa vip ,unaona kama unabaki na madoa madoa.
 
Back
Top Bottom