Alnadaby
JF-Expert Member
- Sep 28, 2006
- 505
- 41
Wakulu,
Kutoka katika ajira ya kuajiriwa na kuingia katika ajira ya binafsi ni kazi kubwa.Mimi niko njia panda nataka kupata mkopo wa kununua truck ili hata nikiacha kazi yangu ya kuajiriwa niendelee na uzoefu nilionao kwa kuwa transporter.
Nina kiasi cha 20% cha mtaji ninaotaka.Nataka benki inikopeshe 80% ya mtaji.Pia nina nyumba yenye thamani ya 50% ya mkopo unaotakiwa ambayo itakuwa dhamna kama itahitajika.
Nilijaribu kutuma maombi na biz plan yangu kwenye benki moja nikaambiwa niweke ile pesa ya 20% katika akaunti yangu,niwe na barua ya guarantee kutoka kwa kampuni itakayonipa shughuli ya kusafirisha bidhaa zake,niwe na collateral.
Nilipata mkataba mzuri na barua ya undertaking kutoka kampuni iliyonipa mkataba wa kuifanyia kazi miaka 3 na hiyo ilitosha kwangu kulipa kwa instalments na kurejesha mkopo kwa miaka mitatu.Nilihakikishiwa kupata mkopo huo bila matatizo na mkubwa mmoja na hata mkurugenzi wa tawi hilo.Kwa bahati mbaya huyu Mkurugenzi wa tawi akawa amehama hapo.
Huku nyuma bwana mdogo aliyekuwa akisema mambo yanawezekana akawa anataka kufanya ufisadi na mimi nikaona nitapata hasara. Appraisal ilichukua miezi 4 jamani,just imagine.
Baada ya miezi kama 4 ya appraisal maombi yangu yalikataliwa kwa sababu sikuambatanisha tin no. na leseni ya biashara na sababu nyingine ikiwa ni akaunti yangu kutotembea(ku-circulate),Barua ya undertaking ya tajiri yangu ambaye ana akaunti humo kwenye benki ninayoombea mkopo ya mamilioni mengi haikutambuliwa,ni mambo ya kushangaza na kwa kiasi fulani inamdhalilisha kwani licha ya yeye binafsi kuwa na akaunti yenye ni mihela kubwa humo kale kakijana kamejifanya hakamtambui.
Hata hivyo nilikuwa na tin no. na licence ingawa sikuziambatanisha hapo awali na kale kajamaa hakakuniarifu kuwa nivipeleleke na kuvi present.
Kwa maana hiyo naona kama vile kuna ugumu au uzito wa mwajiriwa kupata mkopo ambao unaweza kumwendeleza katika biashara aliyoizoea hadi akawa naye ni mtu aliyejiajiri na kuweza kusonga mbele bila kutoa rushwa.
Kwa kuwa benki iliyonikatalia sina nayo imani kwa sasa kwa sababu ya ile habari ya ufisadi wa kuomba chochote hasa kutoka kwa meneja wa kitengo cha biashara.Na kwa kuwa nimetokwa na imani na CEO wao ambaye awali alinipa matumaini makubwa ya kunisaidia lakini nilipomwomba aingilie suala hili akawa kimya basi naomba ushauri wa wana JF.
Ni benki ipi inaweza kufanya appraisal ya muda usipozidi mwezi mmoja na ambayo itakubali kunikopesha bila matatizo?
Naomba ushauri wenu wakulu.