Nilikuwa single kwa muda mrefu sikuwa na imani na wakaka hata kidogo. Mwez jana nikakutana na mkaka mstaarabu na mwenye akili ya maisha alinivutia sana kwa maana alikuwa anahitaji mwanamke wa maisha halikadhalika mimi.
Nikajikuta nimezama kwa kipindi kifupi ndani ya wiki 2 nilijikuta nimemuamini
Ghafla tu akaacha kupokea simu zangu na kutojibu ujumbe
Sikukata tamaa nilimtafuta tena kwa upole sana maana sikujua kosa langu na hatukugombana
Duuuuh sikuamini text yake ya mwisho ilinihuzunisha saaaaanaaa "Its over..kwasasa siko tayari kuwa katika mahusiano"
Nawaza sijui nini nimemfanyia nakosa amani na naogopa kumsumbua zaid nahisi atanichukia.
Kwanza nikupe pole kwa mkasa uliokukuta / kukutokea.
Kwa ushauri wangu na mtazamo wangu.
Kuna kitu ambacho nataka nitambue toka kwako, kipindi mpo katika uhusiano wenu wiki 2.
1. Umewahi kuongea nae kitu chochote kuhusu wewe kwa undani.
2. Umewahi kuonesha hisia za karibu sana kipindi upo nae.
Kama ulimuonesha hisia zako mapema mno kuwa unahitaji kuwa nae katika uhusiano, basi hapa umefanya kosa kubwa,
Hata kama umependa mwanaume kiasi gani, kamwe usioneshe hisia zako mapema kuwa umempenda kwa dhati.
Mkiwa katika uhusiano kamwe usimueleze kila kitu kuhusu wewe, na jaribu asijue kila kitu kuhusu wewe,
Mpe muda zaidi ya miezi sita hata mwaka mzima, hiki ni kipindi ambacho wapenzi huanza kufahamiana baadhi ya mambo kwa kiasi Fulani,
Labda huenda huyu mwanaume alikutambua kila kitu chako na baadhi ya mambo yako na jinsi ulivyo mpa mchezo,
Amekuona mwanamke dhaifu,
Na huenda akafikiria kuwa unafanya umalaya, au akitokea mwanaume mwingine utashindwa kuwa na msimamo dhabiti, hicho alicho kifikiria.
Hapo ungetakiwa uanzishe mahusiano nae lakini usingeonesha hisia zako kwa ukaribu,
Halafu ungejaribu kuonesha umakini, msimamo, na mwelekeo katika mambo yako, hata angekuomba mchezo ungemkatalia na kusubiri baada ya miezi 6 hata mwaka ndio umpe hii ingesaidia kumfanya aamini kuwa upo makini hata kama umependa kwa kiasi gani?
CHA KUFANYA / JINSI YA KUMRUDISHA
mvumilie kwa muda kidogo takribani wiki 2 au hata mwezi 1.
Mfuate tena mweleze kuwa huna kosa na unahitaji uwepo wake, unahitaji ukaribu wake, mmbeleze mwambie ukweli atakuelewa,
Na usifanye makosa kwa kumnyenyekea sana na kumwendea kila wakati unamuomba mrudiane.
Mshawishi kwa kila neno na kila namna ikiwa na sababu / maelezo ya kujitosheleza akakuelewa na mkarudiana.
Endapo atakubali mrudiane.
Kamwe usirudie makosa uliyofanya,
Na pia jaribu kumchunguza pia Hutu mwanaume kama ana familia, ama uhusiano na mtu mwingine,
( pia unaweza kumchunguza hata kabla hujarudiana nae, kama ana mpenzi mwingine ama familia, ni chanzo kipi kilimfanya achukue uamuzi wa kusitisha mahusiano yenu )
Akikataa kurudiana nawe / ukiona hana muelekeo wa penzi lenu kurudi,
Usiogope wala usiumie sana,
Maana hizi ni moja ya changamoto katika mahusiano, kabla ya ndoa.
Cha msingi, mwambie ukweli na hujapendezwa na maamuzi aliyochukua,
Na kama ameamua iwe wewe kubaliana na matokeo cha msingi Fanya mambo mengine ya muhimu,
Ambayo yatakuweka bize,
Huku ukijaribu kusahau maumivu ya kuachwa na mtu umpendaye.
Kumbuka malipo ni duniani, lazima yatamkuta tu huyu mwanaume.
Usiwaze sana jaribu kusahau mahusiano kwa muda mfupi.