Nifanye nini kufuta kumbukumbu za matukio mabaya kwa watoto wangu?

Acha kila mtu atumikie faida ya matendo yake. Usiwahaminishe watoto uongo utawajengea mentality ya kikurya (kupigwa ndio kupendwa)
 
Cha kuwasaidia labda wambie wasije kuwa mama baba yao full,stop acha kuwaambia uongo unawachanganya wakijiongelesha achana nao
 
Mimi mpaka kesho nakumbuka babu alivyokua anampiga bibi mpaka anamuacha mtupu. Ilifika kipindi babu akiingia ndani tu najua kelele za vipigo zinaanza. Siku zingine wanaanza kupigana saa nane za usiku naamka naanza piga kelele majirani waje wawagombelezee.
 
Watoto wana hisia na wanajua kizuri na kibaya. Waache wajisikie wanavyojisikia na usiwaongopee baba yao mtu mzuri wakati mpigaji sio mtu mzuri kwenye jamii. Siku watamsamehe baba yao sasa hivi hawapo tayari waache kwanza.
 
Mtoto anasahaugu kitu? Wewe uliskia wapi hilo? Mie nakumbuka abuse aliofanya mzee dhidi ya maza kipindi chote cha utotoni hakuna kitu sikumbuki yani.
 
Ishu ni kuvurugwa kiwizad tu! Kuna kamati iliundwa ili kumfarakanisha mzee wako na maza wenu! Hizo zipo sana mkuu sema uzuri ombwe hilo lilipita salama bila kuacha madhara zaidi ni mtikisiko tu.
 
Wanawake wanafiki sana nyie, huyo jamaa sio mjinga kukupiga piga bila sababu,inaonekana wee mwanamke una mdomo pistol na hata story yako inaonesha wazi kabisa unawajaza sumu watoto.
 
Pole sana dada kwa yote uliyopitia.

Licha ya changamoto zako zote, una bahati kwamba watoto wako katika umri huo mdogo wameweza kutofautisha kati ya jambo sahihi na jambo ambalo sio sahihi.

Kwa utambuzi huu wa watoto wako, naweza kusema kuwa hawahitaji msaada wowote kutoka kwako kwa sasa kuhusiana na madhira yaliyotokea huko nyuma.

Wanapokumbusha kuhusu matukio ya nyuma ni wazi kuwa wanapitia kipindi cha kupona (Healing process); ikiwezekana waache waongee wakiwa comfortable kwa kuwa ni jambo lililopita.

Unachoweza kufanya kwa sasa ni

1. Kuwapa moyo kwamba dunia ina watu wema pia

2. Ishi kwa namna ambayo itawapa uhakikisho kuwa ile hali ya awali haitajirudia.

3. Wakuze katika misingi ya dini

Nikutakie kila lenye kheri .
 
Ugomvi wa wazazi ni mbaya mno kwa watoto, sitaki kufafanua zaidi.
 
Usitumie nguvu kubwa kuwaambia eti baba yao ni mzuri wakati waliona kwa macho yao. Hiyo kumbukumbu haifutiki leo wala kesho. Wataendelea kukumbuka siku zote. Kinachoweza kuisha ni chuki dhidi yake, lakini si kumbukumbu ya matukio yake.
Wafunze tu kumcha Mungu, hayo mengine achana nayo, time will tell
 
kula mavi hutojuta utakuja kunishukuru

ukitoka hapo hizo kumbukumbu zitafutika utabaki unayawaza maviπŸ˜„πŸ˜„
Hivi hayo mavi ya mnyama gani kwanza usikute dawa tunayo sema hatujuiπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Me akili yangu imekomea kuwa una watoto watatu na jamaa mwingine kakuoa. Mtunze sana huyo jamaa na utulie kabisa.
 
Daaah!! Pole sana kwa uliyopitia!! Jitahidi kwa nafasi yako kuwafundisha kuwa watu wema, na ikiwezekana wamsamehe
 
Wewe ni mkorofi sana. Haiwezekani mme akupige pasipo sababu na kuishi na watoto wako lazima utawaambukiza tabia yako ya hovyo.
 
Hakuna kitu chochote kinacho halalisha kumpiga mtu mzima unless ni (self defence) acha kutetea upumbafu.
Kitendo cha wewe kunyanyua mkono na kumpiga wewe ndo una makosa regardless ya alichofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…