Nifanye nini kufuta kumbukumbu za matukio mabaya kwa watoto wangu?

Natakakutulia

Member
Jan 20, 2020
56
384
Salaam wakuu

Miaka michache iliyopita nilipitia mambo mengi kwenye ndoa ambayo nikiri kuwa hayakuwa mazuri kwa ukuaji wa watoto wetu kisaikolojia.

Watoto walishuhudia nikipigwa mara nyingi sana, nikitukanwa au kusemwa vibaya. Na hata kuna wakati ugomvi ukitokea chumbani walikuwa wanakuja kusikiliza mlangoni kwetu na kujua ndani kuna ugomvi au kusikia kilio na milio ya makofi na mangumi. Na pia walikuwa wanaona nikiwa nimevimba uso macho au michubuko iliyotokana na vipigo. Na mara kadhaa kama mlango haukufungwa walikuwa wakiingia chumbani kunitetea ili nisiumizwe zaidi.

Hawana umri mkubwa wote watatu bado wako shule za msingi. Mara nyingi walikuwa wakiona baba yao akifika tu na upepo wa ndani unabadilika kama sio wao kupigwa basi ni mama maana alikuwa mkali sana kwa watoto na kwangu.

Nilianza kuhisi tatizo kwao kipindi ambacho bado tupo pamoja hatujaachana. Siku moja mwanangu aliniuliza swali, MAMA KWANINI TUSIENDE KWA BIBI ILI BABA ASIKUUE? ( Kauli kubwa wakati akinipiga alikuwa anasema IPO SIKU NITAKUUA) na watoto walikuwa wanasikia hivyo kuoata hofu ya mimi kuuawa siku moja. Nikaamua kuongea na baba yao kuhusu swala hilo kuwa watoto wanahofu aache kunipiga ila akajibu nimewajaza sumu kuwa baba yao mbaya nk ioa sijawahi fanya hivyo na ukatokea ugomvi akanipiga na kunifukiza kabisa ili nisimwqribie watoto wake.

Japo baadaye niliwapata watoto na kuanza kuishi nao maana tangu hapo tuliachana moja kwa moja na sasa naishi maisha mengine. Ila tatizo limebaki owa watoto kioa mara wanaomhelea jinsi nilivyopigwa na yote.

Mnaweza kuwa mmekaa unaona mtu anasema mama bora tulivyokuja huku hata hupigwi tena, au wala sisi hatupigwi tena nk najaribu kuwaambia baba yenu anawapemda, ni mtu mzuri nk ila hawaeleqi na wananibishia na kumfananisha na monster wa kwenye movie. Binafsi siongelei chochote kibaya kwao ioa wao hawasahau katu. Na hata akipiga simu kutaka kuwasalimia hawakubali hadi nakata siki, nikimwambia hawataki ananilaumu kuwa wqnajaza sumu kitu ambacho sifanyi.

Naandika haya nikiwa nimeshajitahidi kufanya mambo kadhaa ikiwa ni pamoja kuwaamisha kwamba baba yao ni mtu mwema, na anawapenda ila hawakubali.

Binafsi nilishaolewa, sasa wanampenda baba yao mpya na wanasemq ndio baba yao na si yule mwingine( huwa wanamwambia wao wakiwa wanapiga naye stori, wanamwambia shule waitwe fulani bin jina la baba mpya) hataki kusikia kuhusu baba yao kabisa.

Je, hii inaweza saidika kifuta hizi kumbukumbh au niwaache tu walivyo?
 
Sasa na wewe unataka kuharibu kwa kusema uongo! Hao usione ni watoto ni binadamu nao na wana akili na hisia, kama waliona baba yao akikupiga na kutishia kukuua kwanini uwaambie baba yao ni mtu mzuri na anawapenda? Kwahiyo unawafundisha watoto kuwa mtu mzuri huwa anapiga watu na kutaka kuwaua.

Nadhani kwa kuwa umeshaondoka huko wewe usiongee kuwa baba yao ni mtu mzuri na anawapenda, kama hutaki kuongea ubaya wa baba yao basi kaaga kimya tu na uwaache wao waongee ili wayatoe mioyoni mwao. Usitetee ujinga wa baba yao utawavuruga zaidi!

Watasahau tu, hao ni watoto wanavyozidi kukua watayasahau yote hayo ila waache waongee na usitetee unyama wa baba yao
 
.... pole Sana,ila naamini kuna reasons behind kwa nini alikuwa anakupiga. Mojawapo ni kuchepuka (labda ulianza mahusiano na huyu mumeo wa sasa wakati ukiwa na baba yao). Kwa kuwa tumesikia upande mmoja hatuna jinsi kupokea kama lilivyo. Too bad kwamba watoto wame-experience hilo.
 
Tafuta professional counselor wapo wengi kwenye mahospitali na ni wabobezi wa matatizo ya kisaikolojia iwe depression, stress, trauma, daydreaming waeleze watakusaidia sana wewe pamoja na watoto
 
.... pole Sana,ila naamini kuna reasons behind kwa nini alikuwa anakupiga. Mojawapo ni kuchepuka (labda ulianza mahusiano na huyu mumeo wa sasa wakati ukiwa na baba yao). Kwa kuwa tumesikia upande mmoja hatuna jinsi kupokea kama lilivyo. Too bad kwamba watoto wame-experience hilo.
Hakuna kitu kinachohalalisha kumpiga mwenza wako.

Kachepuka, mpe talaka!!!
 
.... pole Sana,ila naamini kuna reasons behind kwa nini alikuwa anakupiga. Mojawapo ni kuchepuka (labda ulianza mahusiano na huyu mumeo wa sasa wakati ukiwa na baba yao). Kwa kuwa tumesikia upande mmoja hatuna jinsi kupokea kama lilivyo. Too bad kwamba watoto wame-experience hilo.
Ni kweli kuna sababu. Sababu ni kuwa alikuwa ana mwanamke mwingine ambaye alikuwa anataka kuishi naye hivyo alikuwa ananifukuza niondoke aishi na huyo mwanamke.

Mwanaume ninayeishi naye sikuwa naye kipindi cha ndoa nilimpata baada ya kuachika.

Soma nyuzi za nyuma utakuja kukutana na kioamde kinachomuhusu.

Asante.
 
Asante
Sasa na wewe unataka kuharibu kwa kusema uongo! Hao usione ni watoto ni binadamu nao na wana akili na hisia, kama waliona baba yao akikupiga na kutishia kukuua kwanini uwaambie baba yao ni mtu mzuri na anawapenda? Kwahiyo unawafundisha watoto kuwa mtu mzuri huwa anapiga watu na kutaka kuwaua.

Nadhani kwa kuwa umeshaondoka huko wewe usiongee kuwa baba yao ni mtu mzuri na anawapenda, kama hutaki kuongea ubaya wa baba yao basi kaaga kimya tu na uwaache wao waongee ili wayatoe mioyoni mwao. Usitetee ujinga wa baba yao utawavuruga zaidi!

Watasahau tu, hao ni watoto wanavyozidi kukua watayasahau yote hayo ila waache waongee na usitetee unyama wa baba yao
Asante,
 
Pole kwa kipigo,ila kidogo napata wasiwasi,embu tujuze tatizo lilikuwa ninininkwa ww kulakipigo mfulurizo? Chanzo chabhayo yoote isije ikawa ninwewe pia
 
Wewe umekumbwa na Post traumatic stress disorder hivyo inakufanya uone Kwamba na watoto wako watakua na hali hiyo. You're Ok, Anza upya.

Halafu utamu wa nyama mfupa, na utamu wa ndoa kipigo. Muuliza bimkubwa wako atakuambia. So Usiwaze PTSD inakusumbua tu🚶🚶
 
Nikwambie tu ukweli...HAWATOSAHAU....mimi nakumbuka matukio ya toka nikiwa darasa la 1..2..3 ya wazazi wangu...now nna 36 years sisahau na sitosahau..japo simchukii mzaz wangu ila matendo siyasahau.....
Never ever...na wala sihitaj kulishwa maneno..ni kwamba niliona kwa macho...picha zipo kichwan
 
Back
Top Bottom