Kumbukumbu tamu za soka

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,180
52,950

Andres Iniesta Kondoo fulani katikati ya msitu wa mbwa mwitu wakali​

Ile picha ya kibabe sana, aliipiga 'Felipe Mondrovera' wa 'Getty images'. Ilikuwa Juni 10 2012 mechi ya kwanza ya EURO. Hispania waliianza kampeni yao ya kutetea taji la mataifa Ulaya. Kumbuka hapo walitoka kuchukua EURO 2008 pale German na Kombe la Dunia 2010 pale kwa Madiba.

Rekodi ilikuwa inasema, hakuna taifa lililowahi kutetea taji la mataifa Ulaya (EURO). Zaidi ya yote, hakuna taifa lililowahi kuchukua mataji matatu makubwa mfululizo. Hata Brazil ya 1958 haikuweza. Ila Hispania walikuja EURO 2012 wakiamini inawezekana.

Kwanini wasiamini hivo? Walikuwa na kila kitu, walikuwa na kila mtu. Xavi Hernandez, Sergio Busquets, Andres Iniesta, David Silva, Cesc Fabregas, Xabi Alonso. Utawaambia nini watoto wa Vicente Del Bosque? Wanapika tu sambusa uwanjani. Hawaelewi kitu zaidi ya kupiga mpira. Miguu yao ina sumu hatari, kila wanaloamua uwanjani linakubali

Hapo nimekutajia tu viungo, sijaugusa ukuta wa Sergio Ramos, Gerald Pique, Alvaro Arbeloa na Jordi Alba. Utawaambia nini? Enzi hizo wanacheza bila namba tisa. David Villa na Fernando Torres hawakumbukwi kabisa kuwa wapo benchi. Hiyo Hispania, acha kabisa! 🙌.

Najua unajua walibeba lile kombe. Hiyo siyo hoja yangu ya msingi. Hoja yangu ni zile njia alizokuwa anapita Andres Iniesta. Kila mechi aliyokuwepo uwaniani, aliondoka na picha za kutisha. Mara nyingi utamuona katikati ya msitu wa wachezaji wa timu pinzani. Lakini ghafla tu utamuona ameondoka. Atatoa pasi yenye macho, Atapiga chenga au atachezewa rafu. Kitu kimoja tu cha hakika ni kuwa hawezi kupoteza mpira.

Moja ni ile niliyoizungumzia pale mwanzo, mechi dhidi ya Italia. Akiwa katikati ya Christian Maggio, Claudio Marchisio, Thiago Motta, Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini. Alipita kati yao na kuwaacha watu mdomo wazi. Mpaka leo, ile picha inatumika na 'getty' kama cover ya picha zao zote za michezo.

Ila kwa Iniesta picha kama zile zipo nyingi sana. Matukio kama yale ameyafanya sana. Yapo zaidi ya 100. Tukisema tuyajadili leo hatutayamaliza. Pale EURO 2012 aliyapiga zaidi ya 30. Ukipata muda uzitazame. Maestro huyu Andres Lujan Iniesta.

FB_IMG_17099989451029502.jpg
FB_IMG_17099989564055578.jpg
 
SOKA LILIPOVAMIWA NA WACHEZA MIELEKA.
.
Tupo kwenye zama za peke yetu. Zama ambazo Chelsea wamemkabidhi Mateo Kovasic viatu vya Claudio Makelele😳! Manchester United wao wamempa Fred jezi ya Roy Keane. Ndiyo zama tulizopo sasa. Zama ambazo Mathijis De Light anatumwa kumkaba Zltan Ibrahimovic bila uwoga. Wakati huo Gennaro Gattuso anamtaka Koulibaly kuwa beki mstaarabu.
.
Ndiyo zama tulizopo sasa. Zama ambazo 'VAR' inamruhusu mvulana Lautaro Martinez kukatiza mbele ya ukuta wa Giorgio Chiellini na Leonardo Bonucci bila uwoga. Zama zimeenda wapi? Zama zile Fergie analazimika kumuuza Paul Ince, si kwasababu hamuhitaji, ila angeitawala vipi 'dressing room' yenye watukutu wawili? Tayari alikuwa na Roy Keane, kumuongeza Ince ni kujitafutia shinikizo la damu.
.
Ni Paul Ince huyu aliyemsababishia ajali ya gari Steven Gerrard mdogo. Alimpa funguo ya gari akimtaka Gerrard aende nyumbani kumletea viatu vya mazoezi bila kujua Gerrard hajui kuendesha gari. Ila Gerrard akalazimika kwenda hivohivo kwa kumuogopa. Angemueleza nini Paul Ince amuelewe? Kwanza ujasiri wa kusimama mbele ya Ince angeutoa wapi? Hawa watu wameenda wapi? Akina Patrice Vieira, wameenda wapi?
.
Unamkumbuka Vieira wa mwaka 2001 pale London stadium? Alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya sana Paul Di Canio, wakati anatoka Neil Radlock wa West Ham alimfuata akimshinikiza atoke haraka, Vieira akamtemea mate, polisi wawili waliingia kumkokota atoke uwanjani mapema. Mmoja alipata likizo ya wiki mbili kuuguza bega lake lililotenguliwa na Vierra. Huyo ndiyo Patrick Vierra. Aliwahi kuoneshwa kadi nyekundu kabla hajaingia uwanjani. Mchezo kati ya Arsenal na Sunderland, shabiki mmoja wa Sunderland alimuonesha Vierra kitendo cha ubaguzi, Vierra alimfuata hukohuko jukwaani. Unajua kilichotokea? Yule shabiki aliondoka uwanjani na pua iliyovunjwa na Patrick Vieirra.
.
Tuachane na Vieira, Unamkumbuka Duncan Ferguson? Siku moja alivamiwa na vibaka wawili nyumbani kwake, mmoja alifanikiwa kumtoroka, mwingine alipokelewa akiwa mahututi na wauguzi wa hospitali. Hiyo ilikuwa ni kazi ya 'Big Dan' aliyekipiga Everton hadi mwaka 2006. Wameenda wapi hawa watu?
.
Labda nilimkosea heshima King Eric Cantona, labda niliikosea heshima tarehe 25 January 1995. Hakuna dhambi kama kuwazungumzia vichaa wa soka bila kuanza na mfalme Eric Cantona na pigo la 'kung fu' alilolituma jukwaani kwa mashabiki wa Crystal Palace. Unajua ilikuwaje?
.
Baada ya beki wa Crystal Palace, Richard Shaw, kumuweka Cantona chini ya ulinzi kwa muda wote wa mchezo, Cantona aliamua kumtandika buti la makusudi. Akaoneshwa kadi nyekundu. Wakati anatoka shabiki mmoja wa Crystal Palace, Michael Richards, akanyanyuka kwenye kiti na kuamua kummiminia matusi Cantona.
.
Cantona hakutaka kujua kama kuna sheria ya kuwaadhibu mashabiki. Alichoamini ni kuwa mtenda maovu anastahili adhabu. Cantona alitoka na pigo moja safi la kung fu kwenda kwa yule shabiki. Haikuishia hapo. Alimsindikiza na ngumi kadhaa hadi polisi walipofika. Alifungiwa kutokucheza soka miezi tisa.
.
Siku moja baada ya kufungiwa, aliita mkutano na waandishi wa habari. Dunia nzima ikiamini Eric Cantona anataka kuomba msamaha. Alitoa hotuba yenye sentesi tatu tu. Tena lilikuwa ni fumbo. Mpaka leo maana yake haijapatikana. Hiyo haitoshi, Cantona mwenyewe anasema mpaka leo, hakuna tukio lake bora kwenye soka kama lile. Nauliza, Hawa watu wameenda wapi?
.
Alikuwepo mtu mmoja pale Chelsea anaitwa Vinnie Jones. Kutokana na tabia yake ya kutokucheka uwanjani na mfululizo wa matendo yake ya kigumu alialikwa kuigiza filamu kama jambazi kuu baada ya kustafu soka. Hawa ndio watu wababe wa kuwazungumza waliopita kwenye soka.
.
Uliwahi kumsikia Thomas Repka? Beki kisiki wa Czech anayesota jela kwa sasa. September ya mwaka 2007 aliwapiga waamuzi wa ziada na Cameraman wa Televisheni aliyekuwa anarekodi tukio hilo.
.
Wahispaniola nao hawakuwa nyuma. Walikuwa na mtu mmoja mwenye jina gumu kama 'reli na chuma yake', Andoni Goikoetxea Olaskoaga. Kwa leo tutumie tu jina lake la utani. 'The butcher of Bilbao'. Alimuhamisha Diego Maradona la liga na kwenda Napoli ya Seria A, baada ya kumvunja mguu mara mbili mfululizo. Maradona akaamua kuondoka Hispania ili asikutane nae tena.
FB_IMG_17100009577032349.jpg
FB_IMG_17100009536757077.jpg
 
PESA, WANAWAKE, POMBE NA LIONEL MESSI

Alikaa chini kwa tafakuri baada ya Mwandishi kumpiga swali moja gumu kidogo nguli wa habari Argentina bwana Daniel Arcos, alipoulizwa nini kitu muhimi zaidi maishani mwako na kinakufanya upende maisha?

Daniel akasema kwa Dear Gambe inanisafirisha kimawazo, pili wanawake ni tiba stress zinakufa, tatu pesa ambayo inaweza kuhamisha milima ya Olympus kutoka Ugiriki mpaka Ulanga Morogoro na nne ni Lionel Messi, mtoto mmoja anaecheza na kuwafundisha wenzie soka

Alimaliza vipaumbele vyake Daniel na kumwambia Mwandishi bwana achana na mimi nipate gambe nyingine, Mwandishi nae akafunga dodoso lake na kuanza safari ya kurejea ofisini kwenda kujaza taarifa yake vyema, japo alistaajabu sana majibu ya Daniel ila alichoka baada ya kusikia ya Sergio Fernandes

Sergio Fernandes ni msomi wa daraja la juu kwenye sheria nchini Argentina, ni moja kati ya Mahakimu wakubwa nchini humo nyuma ya sifa yake kubwa nchini mwake yeye aliweka nadhiri yake kuwa jezi aliyoinunua ya Diego Maradona wakati anatambulishwa Newell's Old Boys 1993, atampa mrithi wake sahihi

Zilipita siku, wiki, mwezi na hatimae miaka jezi namba 10 ya Diego Maradona inaoeza kabatini, mkewe Cathrine alimuuliza hii jezi itakaa ndani mpaka lini?? Sergio alimjibu mpaka pale mrithi wa Maradona atakapopatikana nitamkabidhi jezi hii, baada ya hapo nipo tayari kufa nikiwa nimetimiza nadhiri yangu

Hiyo ilikuwa 2005, kesho yake tu Lionel Messi anaanza kuonyesha maajabu Camp Nou, ikapita tena miaka mpaka 2014 tayari Lionel Messi kafanya kila kitu kwenye dunia, Fernandes alipotaka kumpa Jezi akapigwa konga na police akafeli kumpa jezi yake lakini bado hakukata tamaa

Kumbuka Fernandes ni msomi mkubwa aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa Argentina, lakini anahangaika ili tu ampe Messi jezi ya Maradona kwakuwa anaamini ni mrithi wake, ndoto ikatimia 2018 kwenye kombe la dunia kwa msaada wa Mwandishi Vero Brunatti, Messi akapewa jezi yake

Lionel Messi hakuvaa jezi hiyo kwakuwa aliamini kama Maradona bado yuko hai basi Mfalme ni yeye, ila siku alipokufa Messi alivaa hiyo jezi Novemba 25,2020 ikiwa ni miaka miwili tangu apewe, akafunga bao na kuionyesha, pia akaiambia dunia yeye ndie MFALME MPYA
FB_IMG_17100011371314839.jpg
 
PESA, WANAWAKE, POMBE NA LIONEL MESSI

Alikaa chini kwa tafakuri baada ya Mwandishi kumpiga swali moja gumu kidogo nguli wa habari Argentina bwana Daniel Arcos, alipoulizwa nini kitu muhimi zaidi maishani mwako na kinakufanya upende maisha?

Daniel akasema kwa Dear Gambe inanisafirisha kimawazo, pili wanawake ni tiba stress zinakufa, tatu pesa ambayo inaweza kuhamisha milima ya Olympus kutoka Ugiriki mpaka Ulanga Morogoro na nne ni Lionel Messi, mtoto mmoja anaecheza na kuwafundisha wenzie soka

Alimaliza vipaumbele vyake Daniel na kumwambia Mwandishi bwana achana na mimi nipate gambe nyingine, Mwandishi nae akafunga dodoso lake na kuanza safari ya kurejea ofisini kwenda kujaza taarifa yake vyema, japo alistaajabu sana majibu ya Daniel ila alichoka baada ya kusikia ya Sergio Fernandes

Sergio Fernandes ni msomi wa daraja la juu kwenye sheria nchini Argentina, ni moja kati ya Mahakimu wakubwa nchini humo nyuma ya sifa yake kubwa nchini mwake yeye aliweka nadhiri yake kuwa jezi aliyoinunua ya Diego Maradona wakati anatambulishwa Newell's Old Boys 1993, atampa mrithi wake sahihi

Zilipita siku, wiki, mwezi na hatimae miaka jezi namba 10 ya Diego Maradona inaoeza kabatini, mkewe Cathrine alimuuliza hii jezi itakaa ndani mpaka lini?? Sergio alimjibu mpaka pale mrithi wa Maradona atakapopatikana nitamkabidhi jezi hii, baada ya hapo nipo tayari kufa nikiwa nimetimiza nadhiri yangu

Hiyo ilikuwa 2005, kesho yake tu Lionel Messi anaanza kuonyesha maajabu Camp Nou, ikapita tena miaka mpaka 2014 tayari Lionel Messi kafanya kila kitu kwenye dunia, Fernandes alipotaka kumpa Jezi akapigwa konga na police akafeli kumpa jezi yake lakini bado hakukata tamaa

Kumbuka Fernandes ni msomi mkubwa aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa Argentina, lakini anahangaika ili tu ampe Messi jezi ya Maradona kwakuwa anaamini ni mrithi wake, ndoto ikatimia 2018 kwenye kombe la dunia kwa msaada wa Mwandishi Vero Brunatti, Messi akapewa jezi yake

Lionel Messi hakuvaa jezi hiyo kwakuwa aliamini kama Maradona bado yuko hai basi Mfalme ni yeye, ila siku alipokufa Messi alivaa hiyo jezi Novemba 25,2020 ikiwa ni miaka miwili tangu apewe, akafunga bao na kuionyesha, pia akaiambia dunia yeye ndie MFALME MPYAView attachment 2929670
Endelea kuleta hivi vitu mkuu,ninavielewa sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom