Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Kuna Mwalimu Mmoja aliona Duka LA nafaka limejaa mzigo.

Alipouliza mtaji wote kias gani, akajibiwa kama million 9.

Basi, Akaenda benki kuchukua Hiyo millioni 9 ili afungue duka kama lile.

Kilichomtokea,
Alijikuta biashara Anaifungua na mtaji wa million Moja na Nusu.

Kutokana na Usimamizi mbovu,
Duka halikudumu hata mwaka Mmoja,

Miezi 6 tu alijumlisha duka lote kwa thamani ya laki 6.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaha ukiskia watu wanapiga hela bisharani usidhanie kipompi pompi!
 
kitabu chenyewe hiki hapa. sasa najua maswali yatakuja mengi maana sii kila mtu anaamini anaweza kupata maarifa ya kumfaa katika vitabu sasa hapa pia naambatanisha ushuhuda wa mtu ambaye ameweza kufanya hivyo.


INSI BIASHARA YA SAMBUSA ILIVYOBADILISHA MAISHA YANGU NILIANZA NA ELFU KUMI SASA NATENGENEZA ZAIDI YA MILIONI TATU!
Kama ni mhitimu wa masomo ya ualimu hasa wale wenzangu wa masomo ya Arts naamini sina haja ya kukuambia niliyokua nikipitia miaka miwili iliyopita. Baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo mwaka 2015 nilikua na matumaini makubwa ya kuajiriwa moja kwa moja nikiamini ualimu ni dili. Lakini haikua hivyo, hata katika shule binafsi ambako niliomba kujitolea nilikosa kabisa hivyo kuamua kurudi nyumbani kusubiria ajira za Serikalini zitangazwe.
Lakini muda ulikua unakimbia na miezi sita ilipita hakukua na cha tangazo la ajira wala nini, nilishachoka kusubiria ajira hivyo nilitaka kutafuta kitu cha kufanya kwa maana ya biashara. Nilikua na mawazo mengi ya biashara lakini tatizo lilikua ni mtaji, kila wazo lilikua linahitaji mtaji si chini ya milioni moja, sikua na hata Shilingi ndani hivyo mawazo yote mazuri yalikufa kabla ya kuanza.
Mimi najua kupika na siku moja nilikua napika Sambusa za nyama, nilikua napika kwajili ya kula nyumbani. Sambusa zangu ni nzuri sana na watu huzipenda. Hivyo siku moja wakati ninapika niliwaza kwanini nisianze biashara ya kupika na kuuza sambusa. Nilipiga mahesabu kwa kuanza nilihitaji mtaji wa kama Shilingi elfu kumi tu, hiyo nisingeikosa lakini bado nilikua na mawazo nikiona kama ni kazi ya kudhalilisha elimu yangu
.
Niliachana na hilo wazo hasa nikifikiria kuwa sitakua nikipata hela ya maana na ajira labda zinakuja. Siku moja nilikua mjini, alikuja mtu anapitisha Sambusa, anauza moja Shilingi mia tano, nilinunua na kuonja hazikua na ladha kabisa, hata sikula nilitupa. Lakini wakati narudi nyumbani lile wazo lilinijia tena, niliona kuna fursa, nikiwaza kama nikiweza kupika sambusa 100 tu kwa siku, kwa bei ya Shilingi mia tano nitapata Shilingi elfu hamsini ukizidisha kwa mwezi ni kama Shilingi milioni moja na nusu.
Baada ya kupiga hayo mahesabu na kuwaza mshahara wa mwalimu ambao hautafiki hata laki sita nilijiona fala kuanza kuwaza watu watanionaje. Sikutaka kumuambia mtu kwani nilijua watanikatisha tamaa, nilikua na kama elfu kumi ndani, nikanunua Unga, nyama na kusaga kisha kutengeneza sambusa, nilitengeneza chache tu. Nikaziweka kwenye kikontena cha plastic, sasa kazi ilikua kwenye kuuza kwani kweli nilikua naona aibu. Nilizipeleka kwenye duka la jirani ilia niuzie.

Jioni hazikuisha, kwetu ni mjini mjini uswahilini hivyo kumechangamka, jioni baada ya kuona hazijaisha nilizisambaza mwenyewe jioni jioni kwenye vijiwe vya kahawa na maeneo mengine. Huwezi kuamini ziliisha na siku hiyo nakumbuka nilitengeneza kama smabusa hamsini hivi na ukipiga faida ilikua inakuja kama elfu kumi na tano. Siokuamini, kesho yake nilitengeneza sambusa mia nazo ziliisha kwani nilikua nazungusha mwenyewe.
Labda niseme na kuwa mwanamke kulinisaidia kwani wateja wengi walikua wanaume na mimi ni muongeaji sana. Baada ya hapo sasa niliamua kufanya hii kama biashara, nilianza kupika sambusa nyingi zaidi na kwakua nilikua na muda ilikua rahisi. Nilitengeneza kama kajiko flani hivi kamkaa kwajaili ya kubebea na kuuza sambusa za moto (nadhani mshawahi kukutana navyo mtaani vinauza sambusa za moto), nikatafuta kijana ambaye alikua akizunguka kuuza Sambusa hasa saa za jioni.

Nilikua nikimlipa Shilingi elfu kumi kwa siku kwa maana kutokana na anavyouza kwa maana kwamba kama ni kimpa sambusa mia atauza kwa kuchukua Shilingi mia kwa kila sambusa. Mambo yaliendelea hivyo mpaka kufikia kuajiri mtu mmoja wa kunisaidia kupika na wengine watatu wa kuuza mtaani. Lakini sikuishia hapo, nilianza kupika Sambusa kwaajili ya migahawa, nilizunguka kuna sehemu ambazo hawapiki Sambusa na kuwa nawapelekea.
Lakini pia nachukua oda za kuwapikia watu binafsi kwaajili ya majumbani ambapo bei inapungua kidogo kwakua huchukua nyingi, pia sasa napika pia kwenye sherehe ambapo nashirikiana na wale wapishi kwa kuwapelekea sambusa zangu. Kwa wengi biashara ya Sambusa huiona kama ndogo na ya kipuuzi lakini sasa nimeajiri watu saba ambao nafanya nao kazi na kwa mwezi mambo yakiwa mazuri naingiza mpaka milioni tatu kama faida.

Niko mbioni kufungua Sambusa Cafee (Nashukuru Kaka Iddi) hapa nitakua nikiuza sambusa za aina mbalimbali lakini pia nauza na Juice ila kitu kikubwa ni Sambusa. Lakini pia nitakua nikiuza Bites nyingine mabazo zinaendana na Sambusa au nyama ya kusaga kama Kababu na Egg Chops. Ni biashara nzuri kama ukiifanya kijanja, kama uko sehemu za mjini kwani pamoja na hali ngumu lakini mtu kutoa mia tano kula Sambusa haoni shida sana.
Mara nyingi nauza sambusa kama Bites na si kama chakula. Mwanzoni vijana niliokua nawatumia nilikua nawalipa kwa siku kutokana na mauzo yao, lakini sasa nawalipa kwa mwezi lakini pia ni kutokana na mauzo yao. Kwamba kama akiuza Sambusa mia anapata elfu kumi, basi mimi nazimtunzia na kwa mwezi namlipa laki tatu, lakini kama hatafikia mauzo aliyopangiwa basi inapungua kutoka katika mshara wake kile ambacho hakukiuza.
Katika Mahoteli, migahawa na sehemu za Mama Lishe, biashara ni asubuhi, huko nawapelekea nao huuza na tunagawana faida. Lakini katika kuzunguka mtaani jioni ndiyo kunakua na biashara kuanzia saa kumi na moja mpaka saa tatu za usiku. Kama unataka kufanya biashara hii usijikite katika sehemu moja changamka na sambaza kila sehemu.

Lakini pia kuna maeneo ya Stend hii ni mchana zaidi, silazima ufanye wewe tafuta vijana, kuna vijana wengi hawana kazi wapo mtaani tu watumie. Mimi kwa sasa suala la kuajiriwa halipo tena nina malengo makubwa ambayo yalianza kidogo kidogo, miaka miwili iliyopita nilikua najua tu kupika Sambusa sasa nimejiajiri kwa sababu ya Sambusa na kumbuka yote haya nilianza na mtaji wa kama elfu kumi tu hivi.
NB; Katika kuanzisha biahsara haijalishi umeanza na mtaji mkubwa kiasi gani bali namna ambavyo unaweza kuuza kitu kidogo ulichonacho na kukipanua kuwa biashara kubwa. Kama uko mtaani au umfanyakazi unataka kufungua biashara na hujui uanzie wapi Kitabu cha “Biahsara50” kitakusaidia kufanya hivyo. Kuna bishara nyingi unaziona kubwa lakini unaweza kuanza kidogo kidogo na nimefundisha katika Kitabu changu.

malizia mambo mengine kwenye hii page


Hii naweza sema nakubaliana na wewe maana biashara zinazoonekana za kudhalilisha utu ndio huwa na faida maradufu.
Ndio biashara pekee ambazo zinatumia mitaji midogo ila zina faida kubwa kwa haraka sana maana gharama za kuuzia zipo chini.
Ila kibongo bongo kila mtu anataka amiliki duka la nguo ndio ajihisi ana biashara. Mtu akibutua tu Million zake kadhaa zote anatia kwenye duka la nguo ambako turnover ni ndogo sana.

Laiti watu wangejua vitu vya 500-1000 vinaweza kuuzika kwa wingi na urahisi kuliko vitu vya 20,000-100,000 kwa siku basi wengi tungekuwa mbali sana. Sema ndio hivyo vitu vya jero mpaka buku ndio tunaona biashara za kudhalilisha utu.

Bhakresa sio chizi kuuza juice, maji na soda za 600-1000. Angeweza hata kufungua woolworth yake bongo hapa ila kwa kufuata kwake kanuni za biashara tutaendelea kumpigia makofi kila siku.
 
"KWA SIKU ANAFUNGA MILIONI 2 MPAKA 3,

WASTANI KWA WIKI ANAFUNGA MILIONI 10 MPAKA 15,

KWA MWEZI ANAFUNGA MILIONI 40 MPAKA 60."

JAMANI NDUGU ZANGU WATANZANIA,
TUACHE SHUGHULI ZINGINE ZA KUPOTEZA MUDA,
TWENDENI TUKAUZE CHIPSI DARUSO BAR, UDSM.

"ILA MAISHA LAZIMA YAENDELEE."
Amesahau kuwa hio ilikuwa awamu ya mkwere!
 
Wakuu!

Wasalaam!

najua kuna magreat thinker hapa, wanao uwezo wa kunishauri vyema,

Ni Hivi kutokana na sababu ambazo siwezi kuzielezea hapa kiundani, nimejikuta kwamba kama nisipokuwa na uwezo wa kuzalisha angalau 175,000 au approximately laki mbili kwa wiki, yaani wastani wa shillingi laki nane hivi kwa mwezi nje ya mshahara basi hesabu zangu za kujikwamua zitachelewa,

Ni HESABU ZA Kujikwamua kimaisha, sio kutoka, yaani namaanisha kufanya hivi ni lazima ili nijikwamue, kisha nikishajikwamua ndo nianze kupiga mahesabu ya kutoka kimaisha

Nina uwezo wa kuinject any amount kama capital lakini isizidi million 1. na sio lazima hizo return ziwe za haraka, yaani hata kama return za 200,000 kwa wiki zitaanza baada ya mwezi miezi miwili sio mbaya sana, cha muhimu ni kuwa within a period of six month from today, na kuendelea had miaka 6-7 mbele, ninapaswa kuwa na mradi nje ya mshahara unaoniingizia atleast 200,000 kwa wiki, na mradi huo usinigharimu zaid ya million kama mradi sasa, uwezo wa kuusimamia mimi pysicaly ni ijumaa, jumamosi na jumapili, lakini naweza weka mtu naemuamini, ninao few of them ambao wanaweza lipwa na mradi huo huo.

Naombeni sana mawazo weyu, wakuu, hali ya baba wa taifa sio nzuri, Huwa nakuwa mjanja mjanja sana kwenye hayo mambo ila hadi nimekuja hapa tambua nahitaji mawazo yako chanja

so kabla hauja fikiria kupuuzia, au kujibu upuuzi na kejeli au kuchukulia poa, jaribu kuvaa viatu vyangu japo hauvion vizuri kisha unijibu.

Asante
Kaba
 
inategemea na mahali ulipo pana fursa gani,,
mfano dogo langu anaenda kwa wavuvi wa samaki ananua wale sangara wakubwa sana then anatoa kitu flani kwenye yule samaki kinaitwa bondo,,

iilo bondo anauza kwa wachina mpaka laki nne,
huyo samaki ana mnunua laki mpaka laki na nusu
akishatoa bonndo samaki anamuuza fasta kwa watu wa hoteli au migahawa,,,

sasa hapo ulipo ww kuna fursa zipi,,kilimo dhahabu,,mifugo,,utalii,,,
Hv hawa wachina wanaonunua mabondo wanapatikana wapi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nikushauri mimi nnachofanya, unahitaji mtaji wa Mil 4 kutengeneza laki 8 Kwa mwez kwa ufuatliliaji kdg, me nakopesha kwa riba ya 20% kwa mwezi au 10% kwa wiki. Miez 5 unakua ume double pasa yako. Me nakopesha wafanyakaz wenzangu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Endapo mtu anataka kuwekeza pesa zake kwako. Unatoa riba asilimia ngapi?

Mfano, mtu akikupa 3M, utampa kiasi gani kwa mwezi? Kumbuka wewe ndio unaefanya hiyo kazi ya kuzalisha.
 
Back
Top Bottom