Nifanye biashara gani. Ushauri wenu unahitajika

BrownRange

JF-Expert Member
Dec 25, 2020
927
1,190
Wakuu poleni na majukumu.

Nimeweka akiba yangu ambayo baada ya miezi miwili inaweza fikia milioni 20. Nifanye biashara gani kwa kipato hicho

Ushauri wenu ni muhimu sana
 
Kwa pesa hiyo, fungua duka la hardware ya vifaa vya ujenzi, welding metals n.k,
ingepeza tafuta mkoa unaokua tofauti na Dar es Salaam
 
Fungua depot ya Vinywaji Vikali uza kwa jumla baada ya Mwaka mmoja njoo utoe ushuhuda hapa..
 
Wakuu poleni na majukumu.

Nimeweka akiba yangu ambayo baada ya miezi miwili inaweza fikia milioni 20. Nifanye biashara gani kwa kipato hicho

Ushauri wenu ni muhimu sana
Ushauri wa watu siyo muhimu sana kama unavyodhani. Ushauri wa watu ni mwanzo tu na kinachotakiwa ni wewe kufanya research ya kutosha kabla hujafanya chochote. Hapa mtu anaweza kukuambia ''Nenda Bagamoyo kanununue mkaa leta Dar, uza kwa jumla''. Kwenye maandishi inaonekana ni kitu rahisi mno lakini ukiingia field utakutana kugundua mambo mengi.
 
Mimi nakushauru fanya biashara yoyote ambayo mtaji wake utakuwa ni milioni tano. Usivuke hapo kabisa. Hakikisha unatumia mtaji wa milioni tano tu.

Najua una milioni 20. Usije ukathubutu kuiweka yote kwenye biashara, tumia robo ya hiyo fedha kama mtaji. Ukifanikiwa kuongeza milioni 3 baada ya miezi sita, sasa ongeza mtaji hapo milioni 5 tena ambayo ni hiyo milioni 3 iliyozalishwa + milioni 2 kutoka kwenye milioni 15 uliyobaki nayo.

Fanya hivyo hivyo kila miezi 6 baada ya miaka 5, utakuwa na biashara yenye mtaji ulionao sasa, ila ni kama tu itaenda sawa, vinginevyo utaanza upya Mkuu.

Kila la heri.
 
Asante sana
 
Dar es Salaam
Uza vipuli vya magari vipya sio used unaweza kuanza kununua hapo hapo Kariakoo na ukafungua Duka nje ya hapo....usiuze used kipuli utapata hasara ukaanza kunikumbuka kuwa nilikushauri vibaya na pia ulenge Toyota hasa vile vitu vinavyoharibika sana unachanganya na oil za Toyota pamoja na Castro maisha yatakwenda tunasema Chuma hakimtupi Mtu..uza vile vyenye mzunguko mkubwa ili usikae na chuma muda mrefu na huku ndio unaanza hata kama sio fani yako tembelea garage za magari ujifunze usikurupuke hiyo ndio penati yako ya mwisho...
 
Biashara Inahitaji uangalie eneo ulipo ama unapotaka kufanya hiyo biashara uhitaji wa hiyo huduma na uendeshaji wake uwe na Uhakika namaanisha usimamizi

Kuuza Mazao( kununua kuhifadhi then unauza kipindi kama hiki)
Huduma za afya(duka la daw,zanahat nk)
Urembo
Chakula (restaurant,duka la vinywaji,vinywaji vikali )
Duka la vyakula
Vifaa vya pikipiki unafuta na fundi
Vyote zingatia eneo na mahitaji
 
Back
Top Bottom