Nifanyaje naona aibu, anamlazimisha mtoto wake aniite baba

Wewe bado mvulana mdogo sana i bet huzidi 22 ..
Sasa hayo mambo ya masters na phd yametoma wapi?
Shida sio mimi labda ni kwako na nilie mquote maana ungeanza kwanza kushangaa mada yangu na form 4 failure vinaingiliana vipi
 
Msaada wa haraka unahitajika wakuu, Nifanyaje kuzuia hii hali. Hapa nilipopanga kuna Mwanamke nilimkuta anaishi.

First time nilijua labda ni mwanafunzi maana umri wake unachezea 18~19 , Ila baada ya muda nilikuja gundua anamtoto umri unachezea kama mwaka na miezi 8.

Shida ilipoanzia kuna siku nilikuwa nje nafua yeye alikuwa amekaa na yule mtoto wake, siunajua tabia za watoto kakaropoka huku kanatembea kuja kwangu baba baba baba.

Yaani toka siku hiyo imekuwa ndio wimbo baba baba. Nikiwa naondoka anamwambia mwambie baba akulete zawadi, nikirudi jioni anamwambia kampokee baba kanakuja kugonga mlango baba baba yaani.

Fedhea kubwa inapokuja kuna wapangaji wengine wapo sasa ile nikiwa narudi kile kitoto kinakuja baba baba yaani nashindwa hata nijibu nini naishia tu kujichekesha kinafiki.

Hapa nilikuwa nawaza nimwambie amkataze yule mtoto naona haiwezekani, Au nijiegeshe tu kuwa baba hewa. Nahitaji ushauri wandugu natanguliza shukrani.

Acha utoto wewe mvulanaaa... kuitwa Baba na mtoto mdogo asiye na dhambi ambaye ni sawa na malaika ni baraka sana...Muache mtoto ajisikie vizuri kwani hautopungukiwa chochote. Kila urejeapo nyumbani tafadhali mletee zawadi na uwapo nyumbani cheza nae kama Baba kwani ndio faraja yake.

Believe me, haitakucost chochote!
 
Kwani wewe unavyopita barabarani halafu ukamkuta mmama mtu mzima ambaye humjui ni mama nani ila ni mtu mzima umri wa mama.


Ukamwambia shikamoo Mama,kuna kunakuwaga na shida?????Au ushwahi kukataliwa kwamba mimi sio mama yako???


Guys siku hizi watoto wengi wamekosa watu wakuwa play role za Baba maana maendeleo yamekuja na ngono zembe nyingi.Na vijana hatutaki majukumu tunawaza kut*mba tu.

Mtoto akikuita baba ni ishara nzuri as long as ni mtoto kuwa na upendo nae.Akikuwa atajua kutofautisha yupi baba yake mzazi yupi sio.

Yaani na wewe unakataa mtoto kama mama wa kambo khaaaaa.Hii tabia wanaume hatuna kabisaaa.

Sasa zawadi ya mia mbili nayo ni big deal kwamba ukimnunulia mtoto pipi ya 200 utafirisika.Waache watoto wawe watoto roho zetu mbaya na mitazamo yetu negative tubaki nayo wakikuwa watajua kumbe hiki si sahihi hiki ndo sahihi.
 
Haya mambo haya kuna katoto kalikua na haya mazoea mpaka baba yake akaweka uhasama baina yetu, ila binafsi huwa inanifariji mno na nina watoto wa hivi si haba japo waswahili na imani zetu wanadai itapelekea kuwa na kizazi cha kimagumashi
 
Jiongeze mpende huyo mtoto mnunulie zawadi na mahitaji mengine ili upate baraka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom