Nifanyaje naona aibu, anamlazimisha mtoto wake aniite baba

Eeh watu jamani mlivyomshambulia mtoa mada issue ni kwamba yeye hajisikii vizuri kuitwa baba na huyo mtoto hayo ya elimu ndogo, sijui umri na blah blah zingine za nini sasa,mtoa mada watoto wengi wakiwa na umri huo ndo wanaanza kujifunza kuongea na Mara nyingi wanaanza na baba au dada so wewe usiwaze kakikuita baba we kapokee tu unakaambia wow uncle,na mama ake mzoeshe tu Hilo jina la uncle kwa mfano unamuuliza uncle hajambo au ukikaletea zawadi kaambie uncle chukua zawadi, watoto wepesi Sana kushika vitu in no time kataanza kukuita uncle, au na kua uncle hutaki mkuu??
 
Una umri gani bro..tusije tukaanza kumshauri kijana aliyefel form four juzi. Lugha zikapishana. Anyway hama.

Nenda kapange kwingine huko utaitwa majina mengine, mfano msela, man, muhuni, auncle,nk
 
Msaada wa haraka unahitajika wakuu, Nifanyaje kuzuia hii hali. Hapa nilipopanga kuna Mwanamke nilimkuta anaishi.

First time nilijua labda ni mwanafunzi maana umri wake unachezea 18~19 , Ila baada ya muda nilikuja gundua anamtoto umri unachezea kama mwaka na miezi 8.

Shida ilipoanzia kuna siku nilikuwa nje nafua yeye alikuwa amekaa na yule mtoto wake, siunajua tabia za watoto kakaropoka huku kanatembea kuja kwangu baba baba baba.

Yaani toka siku hiyo imekuwa ndio wimbo baba baba. Nikiwa naondoka anamwambia mwambie baba akulete zawadi, nikirudi jioni anamwambia kampokee baba kanakuja kugonga mlango baba baba yaani.

Fedhea kubwa inapokuja kuna wapangaji wengine wapo sasa ile nikiwa narudi kile kitoto kinakuja baba baba yaani nashindwa hata nijibu nini naishia tu kujichekesha kinafiki.

Hapa nilikuwa nawaza nimwambie amkataze yule mtoto naona haiwezekani, Au nijiegeshe tu kuwa baba hewa. Nahitaji ushauri wandugu natanguliza shukrani.

Binafsi sion shida kabisa katika hilo nimewahi kukutana na hali hiyo mara kadhaa katika nyumba za kupanga. Mfurahie mtoto hana kosa ni malaika tu kuna raha katika kucheza na watoto
 
Kuwa makini, huwezi jua anayemtunza ni nani, umbea unaweza kufika kwa mwenyewe ukaliwa kichwa hivi hivi.
 
Hii hutokea pale kavulana kanapokutana na single mother!!

Sasa we hutaki kuitwa baba kumbe unataka uitwaje kwa mfano?! Basi utasikia aniite uncle... !! Unamvua mama ake nguo za ndani halafu mtoto wake akuite uncle?! Hivi zinawatosha kweli nyinyi?
 
Hii hutokea pale kavulana kanapokutana na single mother!!

Sasa we hutaki kuitwa baba kumbe unataka uitwaje kwa mfano?! Basi utasikia aniite uncle... !! Unamvua mama ake nguo za ndani halafu mtoto wake akuite uncle?! Hivi zinawatosha kweli nyinyi?
,,,,ama utasikia jamaa anataka aitwe baba mdogo😁😁😁
 
Kuna hasara gani mtoto malaika wa Mungu kukuita baba. Au unadhani atakubania kupiga mbususu za majirani.

Huwezi jua kukuita baba kunamfariji kvp huyo mtt ambae huenda hajawahi kumuona baba yake.

NB: tumia upstairs vzr kjana
Umesema kweli yote Mkuu
 
Mkuu toa faraja huwezi kujua ya Mungu, embu waza na wewe umekuwa na mtoto alafu ukafa akiwa mdogo, ukiwa zako huko mbinguni ukaona namna watu wanakataa mwanao asiwaite baba japo kwa faraja wewe unadhani utakuwa kwenye hali gani na mwanao atakuwa kwenye hali gani?

Mkuu kuwa mfariji inasaidia.
 
25 years bro. Mwaka kesho kwa majaaliwa namaliza masters naanza PhD. kwani kuomba ushauri kunatatizo mkuu
Hata ungekuwa tayari ni PhD holder at that age,bado una utoto mwingi.Mtoto wa less than a year kukuita Baba unaona shida gani au unakereka mama yake anaposema mwambie baba akuletee zawadi?
 
Yan kakesi kadogo hivyo unashindwa kukahandle? Bora ww mm huwa nang'anganiwa na watoto ata nisio wajua ila kwavile najijua nafas yangu ktk jamii siwez waonea aibu wala kuwakwepa maana wao hakuna wanachojua.

We kubari tu kuitwa baba, tena mara moja moja uwe unakabebea vizawadi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom