Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah

Pole Nifah kwa changamoto

Hongera sana kwa kufanya maamuzi magumu.

"Kuvunjika kwa koleo, sio mwisho wa uhunzi". ZINGATIA.
 
Kwamba wewe hujawahi kupata bebe humu, watu mpo vizuri underground šŸ˜€šŸ˜€šŸ˜€
Halafu ss sikujua km kanieoewa au vipi nikawa naogopa, akinipa huyu nitaumia sbb nampenda!

Nikaamua nisimpe,Bora niumie sijampa kuliko niumie Kwa vyote ,kumpa na kuachwa🤣🤣🤣

Halafu Sina hakika km kaoa maana sioni ht dalili labda km kaamua kutoweka mambo yake kwenye Mitandao, ngoja nimchekišŸƒšŸƒšŸƒšŸƒšŸ˜‚šŸ˜‚
Nikiweka šŸ†” yake hapa utashangaa sn,sahivi hayupo active sn km zamani ila yupo
 
Nifah umeamua kutulisha matango pori dahh!
Mi siamini kabisa ila umefanya vema kwa tulicho expect naona utakua freee walai sio kwa mawe hayaa ni hukuu paaaahh kulee paahhhh 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mbona hamna shida? Mpaka naleta hii maana yake najua ninachokifanya.
 
Humu niliemuelewa kaka mmoja tu,na nilionana nae kabisa,na anajua km niliemuelewa!

Kitambo kidogo hapo!
Unfortunately ht sikumfaidi those days, nilikuwa muoga muoga najutaaa🤣

Ndo maana nawashangaaga wanao fikiria sijui kaliwa na fulani sijui nn,nachekaaa,hawajui!
Joannah
Nani huyo kapoteza shilling?
 
Back
Top Bottom