Nichukue mkopo ninunue hati fungani, then malipo ya hati fungani nitumie kurejesha mkopo?

Habari za leo wadau,

Nimepata hili wazo week hii, ushauri wenu kama linatekelezeka.
Background kidogo:

Mimi ni kijana, nina nafasi ya kupata mkopo kwa interest rate ya 5.6% kwa mwaka, kiasi cha mkopo nachoweza kuchukua maximum ni 125M marejesho miaka 4-10.

Mimi sio mtu wa biashara na pia kazi nayofanya hainipi muda wa kufanya biashara.

Nimewaza nichukua huu mkopo (100M) then niwekeze kwenye hati fungani za muda mrefu(15 years - 13.5% au 20 years - 15.49%, source:BOT)

Then hela nayopata kwenye hati fungani niitumie kurejesha mkopo wangu ambao utakuwa wa miaka 6. Kwa maana hiyo mambo mengine yataendelea kama kawaida.

Ni wazo nimeliwaza sijui wanajukwaa mnalionaje, ushauri wowote unakaribishwa.

Asante
Kama nimekuelewa hivi. Japo umesema hati fungani ni ya muda mrefu miaka 15 hadi 20, hujafafanua malipo yaani kwa maana ya gawio la hati fungani utakuwa unapata kila mwaka au unaanza kuvuna lini toka uwekeze kutoka kwenye hati fungani?
 
Mmh bank gani inakuchaji JUST 5.6% interest kwa mwaka??
Tujue tukimbilie huko!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Unaweza fanya hivo endapo tu utakuwa na uwezo wakupata milioni tano naa, yakuongezea hapo kufanya loanrepayment kila mwaka hadi miaka sita iishe, ... Kwa maana earning rate utakayo pata kutok uliko wekeza haitoweza kulipa principal na interest ya mkopo... Gap litakuwa M5. ambayo ni deficit ndani ya miaka mi6 tu. Baada ya hapo utakua unapata kibunda chako bila wasiii
 
Mm nakupongeza Kwa kile unachotaka kukifanya najua upo ulaya au USA (riba ya mkopo)

Mm ushauri wangu ungetafuta mda wa kujifunza kuwekeza kwenye sector mbalimbali mfano stocks,bonds,real estate ,crypto etc.

Mwaka mmoja unatosha kutafuta elimu ya kuwekeza kwenye industry unayochagua then badae ndo unawekeza hela yako ulikojifunza.

Mafano mm nina mwaka wa pili najifunza kuwekeza kwenye USA stocks. Mwezi wa kumi naanza rasmi kununua hisa za makampuni ya USA japo last year November nilianza kununua Kwa udogo na nimeona faida kubwa hadi sasa (400%).

Nakushauri anza kwanza Kwa kujielimisha huku ukianza Kwa udogo.badae ukishakua vizuri unaweka hela yote.kuwekeza bila elimu ya ndani ni disaster.
Hili ni wazo ambalo pia ninalifikiria. Kwa sasa najaribu kusoma kuhusu crypto na mutual funds
 
Kama nimekuelewa hivi. Japo umesema hati fungani ni ya muda mrefu miaka 15 hadi 20, hujafafanua malipo yaani kwa maana ya gawio la hati fungani utakuwa unapata kila mwaka au unaanza kuvuna lini toka uwekeze kutoka kwenye hati fungani?
Malipo ya hati fungani ni mara mbili kwa mwaka(kila baada ya miezi sita) Hapo katikati naweza kucover mwenyewe
 
Mm nakupongeza Kwa kile unachotaka kukifanya najua upo ulaya au USA (riba ya mkopo)

Mm ushauri wangu ungetafuta mda wa kujifunza kuwekeza kwenye sector mbalimbali mfano stocks,bonds,real estate ,crypto etc.

Mwaka mmoja unatosha kutafuta elimu ya kuwekeza kwenye industry unayochagua then badae ndo unawekeza hela yako ulikojifunza.

Mafano mm nina mwaka wa pili najifunza kuwekeza kwenye USA stocks. Mwezi wa kumi naanza rasmi kununua hisa za makampuni ya USA japo last year November nilianza kununua Kwa udogo na nimeona faida kubwa hadi sasa (400%).

Nakushauri anza kwanza Kwa kujielimisha huku ukianza Kwa udogo.badae ukishakua vizuri unaweka hela yote.kuwekeza bila elimu ya ndani ni disaster.
Kuwekeza kwenye stocks na crypto kuna risk kubwa tofauti na kwenye bonds, hata nikiamua kuwekeza huko itakua ni amount ndogo ndogo kila mwaka
 
Sio TZ mkuu
Nimeangalia wazo lako ni zuri na ninapenda kuwafahamisha hata hapa ndani zipo taasisi zinazotoa chini ya asilimia 10 ya riba kwa wafanyakazi wao kama mikopo ni njia ya kuwapa wafanyakazi motisha. Wasiwasi wangu tu ni pale unapokupa kwenye dollar na unakuja kuwekeza kwenye shilingi hapo kuna kitu kidogo cha kuongalia tofauti ya inflation ya TShs na ile ya nchi unayokopa ili izije kukata baadaye kuna watu wanafanya hedging hapo ukiweza kuweka sawia inaweza kuwa investment nzuri sana ila ningekushauri baadhi uweke kwenye fixed deposit ili ukiwa i need ya hela unaweza kuvunja tu mkataba ukakabiliana nayo. uwe na ya mwaka 1, 2, 5 na 10 itakusaidia kwenye mambo yatakayoibuka. Malipo ya T-bond huwa ni mara mbili kila baada ya miezi sita.
 
Asante kwa ushauri, kuna mdau amesema TPB wana rate nzuri kwa sasa 11% kama sikosei kwa miaka miwili
 
Mpango mzuri. Ningekuwa na access ya mkopo Kwa rate hiyo nisingefikiria mara mbili. Kama wanaruhusu kufanya repayment kila miezi 6 ni vyema zaidi, utaya time marejesho yaendane na coupon payment. Kama walivyosema wengine, utahitaji zaidi ya miaka 6 kumaliza deni na riba. Umesema unaweza kukopa Hadi miaka 10. Kuwa salama na kuondoa pressure za kuhitaji kutafuta fedha za ziada kusupplument marejesho, ningechukuwa mkopo wa Muda mrefu zaidi (Muda utakaofanya coupon pekee zitoshe kufanya marejesho). Ikitokea Una fedha za ziada katika kipindi hicho, Una Uhuru kuzitumia kupunguza deni ili liishe mapema zaidi ya original tenor ya mkopo.
 
Back
Top Bottom