takashi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 905
- 189
Wanaitaka zanzibar ambayo itakuwa na mvua inyeshayo pesa na ambayo watu watakula bila jasho
wapo wanzanzibari ndani ya Tanganyika wanawafundisha kutafuta pesa kwa jasho...Nadhani mnawaona.
Wanaitaka zanzibar ambayo itakuwa na mvua inyeshayo pesa na ambayo watu watakula bila jasho
Seif anawaingiza kwenye mkenge, matatizo yake hayataonekana sasa hivi, as long as wako ndani ya Muungano! Wakitoka tu watajua kwamba wao si wamoja tena! Historia itawatafuna kisawasawa!
topical, hatujawazuia kujitawala, ila sisi bara hatuamui kimdadimdadi mambo makubwa kama kuwa nchi, kumbuka maalim seif hajamaliza mwaka tangu avue kanga na baibui la kike alilokuwa anavaa kujificha, hata hamjui kukaa? Mnahaha tu? Mmeungana basi fanyeni kazi ya maendeleo sio kuchokonoa kwengine kabla hamjawapatanisha vizuri wazanzibari na kuisafisha serikali iliyojaa wezi.
..upande mmoja unaweza kujitoa ktk muungano bila majadiliano au kuushirikisha upande wa pili.
..Zanzibar wana serikali,baraza la wawakilishi,vyombo vyake vya ulinzi na usalama, wanasubiri nini kujitoa ktk muungano?
Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.
Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?
Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari. Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?
- Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
- Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
- Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
- Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
- Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
- Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano
Nonda said:Usemayo ni kweli lakini mara nyingi hupelekea civil war....kuna njia ya kistaarabu ya majadiliano na kura ya maoni....hii ndio njia nzuri na nyepesi ya kupita...au tunapendelea damu imwagike kwanza kama Sudan halafu ndio ije referendum?
Tuanze na Umeme Zanzibar wananunua umeme mara mbili ya bei uuzwao T.bara fuatilia utajua hilo.
Unajua kua TRA wanaenda na boti ya mwanzo zanzibar nakukusanya kodi na jioni hurudi na boti ya mwisho wakiwa na sanduku la pesa za ushuru wakiskotiwa na ulinzi mkali, sasa kuna ubaya gani zanzibar wakitozwa ushuru mara moja wakati pesa haibakii znz? Hii ni mbinu za kuiuwa bandari ya Znz na tayari wamefanikiwa.
Na kuhusu pesa wanazopewa Zanzibar unapeswa kujua kua hawakaiwi bure,zanzibar wanashea 12% ndani ya bank kuu,na pia munakusanya ushuru,sasa kuwalipa wanajeshi wenu kunashida gani hasa ukizingatia kua kua wanajeshi wote wazanzibar ni kutoka bra idadi yao inashinda idadi ya wananchi wa visiwani, sasa si mumejipatia ajira wenyewe tu na pia munalinda koloni lenu.
Nonda,
..u keep on invoking Southern Sudan time and again.
..kwa mtizamo wangu the case and the plight of former Southern Sudanese is quite different frm what is going on in Zanzibar.
..lini ulimuona msudani kusini akiongoza serikali ya Khartoum?
..naomba uondokane kabisa na masuala ya kuzungumzia damu-damu.
NB:
..majadiliano ya nini wakati wa-Zanzibar are convinced kwamba muungano unawarudisha nyuma?
Baraza la Mapinduzi limefanikiwa kuwameza CUF ktk huu muafaka, hivyo leo tunautawala wa chama kimoja Zanzibar chenye malengo ya KiCCM na haitakuwa rahisi kuunda serikali tatu pasipo vyama hivi kuanza mgogoro baina yao. Kumbuka tu ni Mwinyi aliyepiga vita kauli ya Malecela kuundwa kwa serikali tatu akihofia matakwa ya uwakilishi wake na ASP..na knachowashinda CUF ni nguvu ya dola ya CCM bara baada ya Mwinyi na Maalim Seif kufikisha malalamishi haya haya kwa Nyerere wakati wa Malecela na Aboud Jumbe, hofu kubwa ilitoka Zanzibar kwa Wazanzibar na sii bara(The record shows)....
Madhara ya sauti za vijiweni yanaonekana kwasababu watu wanasadiki kile wanachosikia bila tafakuri. Kwa mznz wakawaida anayeishi kigamboni au ilala hili la muungano halielewi, angependa watu waishi kama walivyo. Hoja za kundi la kuuvunja muungano nyingi zimejikita katika madaraka, tunataka mawaziri sawa JMT, tunataka wabunge idadi sawa, tunataka IGP au CDF kwa zamu n.k yote hayamgusi mznz wa kawaida.Mkandara;
Leo hii Zanzibar hakuna chama cha Upinzani hivyo kulazimu sauti ya wananchi inapitia misikitini na vijiweni. Tatizo lenu kubwa hamtaki kuamini kwamba hao kina Seif wapo kwa maslahi yao binafsi zaidi ya kuitaka Zanzibar huru kama mnavyodai
Ridhaa ipi zaidi ya ile ya wabunge wao ndani ya JMT? Na wala hajajitokeza kiongozi kulisema hadharani, yote haya yapo vijiweni, maskani na misikitini.Na kuhusu malalamiko ya mabadiliko ndani ya katiba ya muungano pasipo ridhaa ya Wazanzibar sijui kama umewahi kufikiria sababu kubwa ya mabadiliko haya badala ya kuwasingizia bara
Na ikitokea vinginevyo Rais wa znz akashindwa kutekeleza majukumu kwa sababu za kibinadamu, makamu ambaye ni Seif wa CUF ndiye atakuwa Rais kwa muda huo, sasa akiwa ndani ya JMT, si hili ni kuleta GUN bara hata kama Tanzania bara!Itawezekana vipi leo hii uchaguzi umtafute rais wa Muungano kutoka CCM lakini makamu wake awe ni rais wa Zanzibar hata kama CUF imeshinda hapa hawa watu watakuwa wanatekeleza sera na ilani za chama gani.. Huyo Seif kama makamu wa rais akiwa bara atazungumza kwa niaba ya Wazanzibar au makamu wa rais na kwa sera za CUF au CCM
Ni kutafuta tu sababu hata kama haipo. Husikii wanasema IGP na CDF wawekwe kwa kupokezana, sijui ina mantiki gani hii!!! Ni matokeo ya hadithi za vijiweniDr.Shein akiwa makamu wa raiis ndio itabadilisha kitu gani badala ya kuwepo Bilal na alishindwa vipi kuwawezesha alipokuwa makamu wa rais
Wakati wanajadiliana Seif na Karume hawakushirikisha mtu kutoka JMT, jambo jema. BLW likafanya marekebisho yaliyogusa katiba ya JMT bila kushirikisha JMT. Leo hakuna waziri kiongozi znz, katiba ya JMT inamtambua na haimtabui makamu wa Rais. Kwahiyo hakuna sababu kuleta mambo ya GNU ndani ya JMT.Haiwezekani kabisa kuwa na rais na makamu kwa kufuata nchi wanazotoka bali uwezo wao na mrengo wa chama chao, isipokuwa rais wa Zanzibar anatakiwa utoka chama kilichoshinda uchaguzi wa Zanzibar lakini si awe makamu wa rais. Kufanya hivyo ni kuingia tena muafaka wa CCM na CUF hivyo kuondoa kabisa utawala wa vyama vingi
Serikali ya tatu ishughulikie nini? mbona hakuna mznz anayenijibu, maana ukitaka kitu lazima kuwe na sababu. Serikali ya tatu itaendeshwaje na kwa utaratibu gani?Baraza la Mapinduzi limefanikiwa kuwameza CUF ktk huu muafaka, hivyo leo tunautawala wa chama kimoja Zanzibar chenye malengo ya KiCCM na haitakuwa rahisi kuunda serikali tatu pasipo vyama hivi kuanza mgogoro baina yao
Wapo wanaosema mapinduzi daima, na wengine wanasema mapinduzi ni ya Nyerere na Okello. Angalia mkanganyiko huu! ndio chanzo cha manung'uniko ya muungano, yaani muungano ni 'bangusilo' the place to vent out frustration as a result of underground family feud.Kumbuka tu mkuu wangu wakiondoka tu CCM bara, ule uadui wa Hizbu na ASP utarudi kwani CCM Zanzibar ni ASP kwa uhalisia wake na CUF ni Hizbu kiasili - picha haziivi..Muafaka huu ni kwa faida ya CCM na hadaa kwa viongozi wa CUF
Siku zote nasema wznz wengi wanaimba nyimbo wasizojua maana ya tungo zake. Unaposikia watu wanasema vunja muungano ili tufutiwe visa za Oman, inasikitisha sana na inafikirisha. Hivi muuza pweza pale feri au mpiga matofali pale kigamboni tatizo lake ni kwenda Oman kweli!! yaani muungano hauna maana zaidi ya kufutiwa visa ya Oman, so sad!Ulalamishi wa Zanzibar ni kwa Wazanzibar hali nusu ya Wazanzibar wamehamia bara na karibu the population ni watu wa kuja. Mhindi mkimbizi wa kiismaliia kuhoji uzawa na uraia wa Karume hali yeye mwenyewe rangi yake inamtema. Tabia hii ya kibaguzi wanayo wahindi na waarabu,siku zote hujiona wao wabora zaidi ya mtu mweusi, huu upepo wa kuitaka Zanzibar kwa nguvu zote usiwe ni sauti ya hao wabaguzi ambao asili yao ni HATE.. yaani roho mbaya kwa watu wa mataifa na mila tofauti na zao
Mimi nachoweza kusema ni kwamba tunahitaji katiba mpya na all parties ktk jamii zetu wahusishwe ipaswavyo kuhakikisha haki za bande
zote zinatazamwa kwa mara nyingine kulingana na mfumo wa kisiasa uliopo leo na sii maswala ya Wazanzibar au Wabara unless haki na desturi za Wananchi wa upande wowote zinakiukwa.
Laa sivyo nitakwambia tu kwamba Wapishi wengi huharibu mchuzi na ndicho nachokiona kwa Zanzibar kwani maswala muhimu ya kukiwezesha kisiwa hiki yanakiukwa na ulalamishi wa Zanzibar ni kwa Wazanzibar hali nusu ya Wazanzibar wamehamia bara na karibu the population ni watu wa kuja mnatafuta mengine makubwa zaidi. Leo imefikia hata Mhindi mkimbizi wa kiismaliia kuhoji uzawa na uraia wa Karume hali yeye mwenyewe rangi yake inamtema. Nachelea kusema kwamba tabia hii ya kibaguzi wanayo sana wahindi na waarabu ambao siku zote hujiona wao wabora zaidi ya mtu mweusi, huu upepo wa kuitaka Zanzibar kwa nguvu zote usiwe ni sauti ya hao wabaguzi ambao asili yao ni HATE.. yaani roho mbaya kwa watu wa mataifa na mila tofauti na zao..
Last edited by Mkandara; Today at 08:58 PM.
The ZNZ issue always AMAZES me!
Sijawahi hata siku moja kuelewa nini kinatakikana na kila mhusika na kwa sababu gani!
SEHEMU MBILI ZIKIUNGANA/KUUNGANISHWA KISHA IKATOKEA KUWA HAZISHIKAMANI - JE NI VEMA KUONGEZA GUNDI KULAZIMISHIA KUUNGANISHA..AU NI KUANGALIA NI VIPI SEHEMU HIZO ZIBAKIE KIVYAKEVYAKE?
HUENDA GUNDI IMECHOKA, KUONGEZEA ZAIDI HAKUTATUA SABABU INAYOFANYA GUNDI KUACHIA...
Haaa haaa haaa! Nipo Mkuu, naona ulisahau kuwa kuna Tanzania visiwani kama ilivyo Tanzania bara, katika Serikali ya Muungano. Binafsi ninapenda kuwa na Tanzania Visiwani, ambayo inaundwa na Unguja na Pemba. Zanzibar ni jina la mji mkuu wa Unguja.