Mkuu naomba unifahamu kua, kutaka mtu atambulike kua nani, haimaanishi kua ndivyo alivyo.
Hao waliomba kutambuliwa hivyo, kwa sababu walikuwa wanataka kupata priviledges fulani katika mfumo huo wa apartheid.
Mimi nnao rafiki zangu huko bara, ambao walishikwa wakati wa mutiny ya 1964 na kwa mujibu wa prison regulations za wakati huo, walitaka watambuliwe kama Indians ili badala ya kula dona, wale chapati. Jee iliwageuza kua Wahindi?
Hapa Zanzibar pia wapo watu ambao wanapenda kujiona au kujiita Waarabu kwa maslahi yao fulani tu.
Wapo pia Waarabu waliojiita Waafrika kwa maslahi fulani ya wakati fulani tu.
Huko bara wako Waislamu waliobadili majina ili waonekane ni Wakristo kwa maslahi fulani.
Jee wale Watanganyika wa Fiji nao warudi?
Kutamani kwa watu kufutiwa visa ya Oman ni sawa na pale nyie wabara mlipotamani kufutiwa passport kuja Zanzibar.
Na mmeingia mpaka Zanzibar yote mshaichukua, wenyewe hatuna pa kukaa.
Nimeshukuru umekiri kuwa
colonial mentality and superiority complex ni matatizo makubwa sana znz.
Watanzania walioko fiji wakitaka kurejea Rufiji walikotoka hewala na waje, tena tunawakaribisha kwa furaha kutokana na uzalendo wao wa kukubali kuhusishwa na wabantu wamatumbi wenzao ambao waznz walioko South Africa wanawaona ni binadamu wa kiwango dhalili.Wafiji hawafikirii kuwa sehemu ya philipino, malaysia aua Oman.
Kuna Jambo ambalo hulielewi au unajaribu kulibadilisha . Mjadala wa kufuata visa za znz niliuona kwa macho, kusoma na kuuliza binafsi. Siku simuliwa na labda nikupe kilichojiri ili usiendelee kudanganywa zaidi.
Tanzania bara kwa miaka mingi walitakiwa kwenda znz kwa passport na wakiwa huko wanakuwa 'treated' kama wageni kutoka nchi nyingine. Walitakiwa kupata work permit, kulipa malipo yote kama foreigners ikiwa ni pamoja na huduma za elimu na afya.
Wakati hayo yakitokea wznz walikuwa wanaingia kama mtu anayetoka mkoani, kufanya kazi bila kuulizwa, biashara, kupata huduma zote kama mtu mwingine. Mfano mzuri ni wasomi wa znz ambao wengi ni graduate wa UDSM akiwemo Maalim Sef. Hawa walisoma bure bila kulipa hata senti tano.
Bara wakahoji, endapo sisi ni JMT iweje kuwepo na vikazwo upande mmoja na mteremko upande wa pili?
Tanzania bara wakasema, kama tunaenda znz kwa passport basi nao waje kwa passport. Narudia wakaweka
condition kuwa wznz waje kwa passport. Hawakuomba kufutiwa pasport bali walisema utaratibu wa kawaida unaotumika duniani ni passport kwa passport au bila passport kwa wote.
Wznz wakabaini kuwa wao watakuwa waathirika wakubwa wa mfumo huo kupoteza haki za uhamiaji na makazi ya kudumu(ndio maana leo nusu wanaishi bara), ajira, mafao ya huduma za kijamii ikiwemo elimu bure (angalia CV ya viongozi wa znz ),umiliki wa ardhi na kupoteza idadi ya watalii. Wao wenyewe
wakaondoa hiyo passport. Hakuna mahali Tanzania bara ilipeleka
ombi, ila iliweka masharti mkuki kwa mkuki, period!
Inachekesha sana kusikia wabara wameichukua znz, ni wapi? maana ajira hawapewi isipokuwa sekta binafsi ambayo wznz wengi hawataki kufanya kazi wanazoita za kitumwa. Lakini muhimu hatuhitaji hoja za maskani, tupe takwimu za wabara waliopo znzna wznz walipo bara.
Kama kuna kitu kinawatisha wznz wengi kuhusu kuvunja muungano ni kuelewa kuwa wataondoka bara na kama ni ukaaji basi nao watakuwa kama mgeni mwingine. Hawa waoapiga kelele ni kama 200 tu, wale wa kawaida msasani, kigamboni, makorora, Ilala n.k hawataki kusikia kitu kuvunja muungano. Mvuvi anayeleta pweza zake feri umwambie aje kama mganda atakumwagia uchafu usoni.
Huko mawizarani ndio usiseme, ni ninyi wachache wenye kutamani rangi na madaraka ndio mnaifikiria kanaani, wenzenu wengi wanayo kanaani hata kama hawasemi.