Mkuu Mkandara, Maalim sasa hutamsikia maana keshagawiwa keki, huyu bw hata siku moja hutamsikia hadharani akipinga muungano, ila kwenye vijimikutano vya barazani ndiko mahali pake. Hana ubavu wa kuzunguzia muungano hadharani kwasbabu atasema nini na ni yeye alimtonya mwalimu?
Wazanzibarikujitenga hewala.Hewala kwasababu kero na manung'uniko yasio na sababu za msingi yanachosha. Wale wa kawaida kama ilivyo watanzania wengine wangependa kurekebisha kasoro na kuweka mfumo unaokidhi haja ya sasa,kuna kikundi kinachosema neema ipo njiani, sijui kama neema hiyo ni kwa wote au wateule.
kinachonikera ni kulalamika bila hoja za mashiko.Muungano eti haujawatendea hata jema moja,ni maovu tu. Huu unafiki ndiyo unaudhi, kweli Muungano una matatizo lakini sitaacha kusema unafaida.
Baadhi ya kero na hoja wasizozijibu:
Mapinduzi yameletwa na Nyerere (Ghaisany na mzalendo.net), sasa wanasherehekea nini Jan 12 kama ni uvamizi.
Sijui kama wanajua nini mapinduzi kwasababu wenye nywele za kimanga wanasema a a ! kipilipili wanasema mapinduzi daima,wanaposhindwa kufikia muafaka wanashambulia Tanzania na Nyerere na kusingizia muungano.
Wanasema mambo ya muungano ni 11, sawa! ajabu hilo la mafuta sijui lilitabiriwa vipi mwaka 1964. Hatumii neno nishati kwasababu lina maana zaidi ya wanayoipenda. Katika hayo 11 mengi ni yale yanayowanufaisha wao. Hawaongelei ardhi n.k. Kila kinachowagusa wao ni cha muungano vinginevyo ni chao.
Mengine ni ya ajabu, eti kwanini mkuu wa majeshi au IGP hajawahi kutoka znz, utadhani wakuu hao wanapigiwa kura. Jamani!!! Mbona hatujawahi kuwa na CDF au IGP Mmakonde au Muha!! Ni taratibu gani zinatumika kuwapata watu hawa!!
Wanasema Luxenbourg ina watu 500,000 lakini inapewa uongozi EU, sijui wanajua kuwa ile ni european union kama E.A.C ambayo uongozi unazunguka na sasa tuna katibu mkuu kutoka Rwanda n.k. Utafananishaje na muungano wa nchi. Je tuchague watu tu kwa jiografia au uwezo. Tanzania bara walimtaka Salim bila kujali anatoka wapi, 2/3 ya Halmashauri kuu ilikubali, 2/3 kutoka znz wakaleta fitna huyo ni hizbu n.k sasa wanalalamika wanaonewa!
Wanasema wakijitenga watafutiwa visa za Oman, ah ! hili sina comment maana sijui nianzie wapi.
Wanasema Bara wanawatoza kodi ndio maana biashara inakufa, ha! walitaka vitu viingie znz halafu watumie mgongo wa muungano kuviingiza bara bure, changu ni chako, chako ni chetu!
Wanasema watapata misaada kutoka uarabuni, hata hili sina comment ! na watajiunga na OIC kana kwamba OIC ndio dawa ya matatizo hili nawatakia kheri.
Sasa hivi wanataka Tanganyika irudi, ah! hawahitaji Tanganyika wao kama wameweza kubadili katiba yao bila kuwiana na ya muungano wanashindwa nini kupeleka muswada kwa njia za sheria, wakapiga kura ya maoni wakajitenga.
Hoja ya kutaka Tanganyika ni kutaka kusema sasa tuwe na serikali ya shirikisho ili yale yanayowagusa yawe ya shirikisho, hili sikubaliani nalo maana ni kubebeshana mizigo tu, wao wavunje muungano kila mtu aishi kwa amani.
Wanasema turejee mambo 11, hata hili halina maana, maana hayo 11 mengi yanawagusa, wakati huo huo wanasema mafuta a a! hawasemi nishati. Wapi imesemwa urais ni kupokezana katika hayo 11, wapi imeandikwa mawaziri ni 1/2 kwa 1/2, wapi imesemwa mkuu wa majeshi au IGP ni kupokezana. Nina maana hata hayo 11 sijui kama wanayaelewa ni yapi.
Ukweli mambo ni mengi sana kuorodhesha, lakini la muhimu ni wao wasimame kidete kuirejesha nchi yao kati ya zile nyingi MMKJ alizoorodhesha. Mimi nawaunga mkono katika jitihada za kuirudisha znz ya kale iliyosheheni miti ya mizambarau, hewa ya jasmini, mito na asali, ile ya Sultan! lakini siungi mkono unafiki wa kuushtumu muungano bila kutaja hata kizuri kimoja. Muungano una matatIzo na hata Tanzania bara wanalamika lakini haiondo zuri moja litokanalo.
Leo wanalalamika muungano mbaya lakini mashaalah wapo Kigamboni, Msasani , Ilala n.k kama raia mwingine wa Tanzania.
Muungano ungekuwa mbaya kama wanavyoandika nusu wasingeishi huku.
Ukweli ni thawabu si dhambi lakini unafiki una aya yake, muogopeni mwenyezi mungu kwa kauli zenu.