Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Yap, Baada ya uhuru wa Zanzibar 1963, kulikuwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Unguja. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa ikiandikwa katika nyaraka za serikali hiyo. Baada ya Mapinduzi ndio jina la Pemba likaanza kusikika na kuwa maarufu baada ya Muungano na Tanganyika.

Wanzenji watapata nchi yao pale tu watanganyika watakapodai nchi yao TANGANYIKA. Wanzenji hawana jipya wawe wazi na wapitishe azimio kwny baraza la wawakilishi kama hawautaki muungano. Tahadhari yangu ni kuwa athari ni nyingi kuliko faida, hawa waliohamia kkoo magomen ilala na kwngneko tutawatimua au. Vip tanesco wakikata waya kwa misingi ya kwamba hawafanyi biashara na zanzibar? waache propaganda wanazodangana nazo vibarazan bila ya kutumia logic
 
Mkuu.
Jina Tanzania lina historia yake na maana yake.
Muungano ukienda kuzimu hakuna Tanzania tena.Lile jina tuliloliweka ghalani itabidi tulitoe na kulifuta mavumbi..ili tuanze safari mbele kwa mbele!

Naamini hawa viongozi wa Tanzania, "Tzbara" na Zanzibar wanajificha nyuma ya pazia la muungano huku wakitugawia umaskini.Ukivunjika hawa viongozi hawatakuwa na pa kujifichia.Itawapasa kuchapa kazi au kuelemewa na hasira ya Umma.

Mkuu, unanifunga magoli sana..." I LOVE YOU MAN".
 
mm nataka kukuliza wewe @nguruvv ivi wewe ungekuwa unatokea visiwani unelikubali uburuzwe haka hivi ? or kwa kuwa wewe mtanganyika ndio unaona hivyo unavyoona wewe . usiwe na akili kama za hilo jina lako sawa hebu jaribu kuwa mstarabu unaweza kuifikiria znz kabla ya kuungana hembu vuta hisia kwanza, tell me nn umepicture? watu wenye busara na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yao si ndio ? sema ukweli ...hiii ndio zanzibar tuitakayo bajomba
 
Wanzenji watapata nchi yao pale tu watanganyika watakapodai nchi yao TANGANYIKA. Wanzenji hawana jipya wawe wazi na wapitishe azimio kwny baraza la wawakilishi kama hawautaki muungano. Tahadhari yangu ni kuwa athari ni nyingi kuliko faida, hawa waliohamia kkoo magomen ilala na kwngneko tutawatimua au. Vip tanesco wakikata waya kwa misingi ya kwamba hawafanyi biashara na zanzibar? waache propaganda wanazodangana nazo vibarazan bila ya kutumia logic

hayo yote si lolote si chochote kama uhuru wa nchi yako ....usikonde wewe wacha haya mambo yende uzuri then jibu lako utalipata kwa vitendo sio text
 
Wakat wazenj hawapendi muungano, waingereza nao hawaipendi familia ya malkia (royal family). Wanadai inatumia hela zao vibaya na sio 'fair' kwamba wengine wawe bora zaidi kwasababu tu ni sehemu ya familia ya malkia (source:British Royal Wedding Blogs - Yahoo! Shine). Nini maana ya muungano? Inawezekana kuungana bila kupoteza 'opportunities' ambazo awali ulikuwa nazo? Ukiungana hakuna 'Opportunities' mpya zinazojitokeza? Kwanini Australia na New Zealand bado zipo chini ya himaya ya malkia? Kwa waznz mchawi wao sasa ni muungano, ni kawaida ya binadamu kutafuta mchawi.
 
Sasa hivi kuna NCHI ya Zanzibar kwa sababu ya huu Muungano. Muungano huu umewaudhi wanamapinduzi daima kwa kumpa Urais Dk Shein, Mpemba. Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim SEif ambaye sio tu ni Mpemba bali pia HIZBU damu. Wapeni NCHI yao wapinduane tena.

Wildcat.. ndio maana swali moja ambalo hatujalisikia ni kuona Wazanzibari walioko Bara waandamane kudai nchi yao.. kwanini wanaodai Zanzibar ni walioko Zanzibar zaidi na nje ya nchi - London in particular? Binafsi ningependa waitishwe Wazenji walioko Dar waanza kuisumbua serikali ya TZ kama walivyofanya IRA kwa Waingereza kule.

Nyerere alisema kitu ambacho kinaukweli; wakishatoka kwenye Muungano watajikuta hakuna tena "Wazanzibari" bali kuna Wapemba na Waunguja na na Wabara. Hili ni kweli - ni Wazanzibari kwa sababu ya Muungano. Wanafikiri kwamba husuda na visasi vya kabla ya mapinduzi vimetoweka.
 
Wanzenji watapata nchi yao pale tu watanganyika watakapodai nchi yao TANGANYIKA. Wanzenji hawana jipya wawe wazi na wapitishe azimio kwny baraza la wawakilishi kama hawautaki muungano. Tahadhari yangu ni kuwa athari ni nyingi kuliko faida, hawa waliohamia kkoo magomen ilala na kwngneko tutawatimua au. Vip tanesco wakikata waya kwa misingi ya kwamba hawafanyi biashara na zanzibar? waache propaganda wanazodangana nazo vibarazan bila ya kutumia logic

Sio mbaya kila mtu atarudi kwao...Zanzibar walianza kutumia umeme kablya ya TANESCO kuanzishwa...
 
mm nataka kukuliza wewe @nguruvv ivi wewe ungekuwa unatokea visiwani unelikubali uburuzwe haka hivi ? or kwa kuwa wewe mtanganyika ndio unaona hivyo unavyoona wewe . usiwe na akili kama za hilo jina lako sawa hebu jaribu kuwa mstarabu unaweza kuifikiria znz kabla ya kuungana hembu vuta hisia kwanza, tell me nn umepicture? watu wenye busara na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yao si ndio ? sema ukweli ...hiii ndio zanzibar tuitakayo bajomba

Aah wapi! Zanzibar ilikuwa na Wazalendo wa Zanzibar lini? embu tuambie watu weusi kule Zanzibar wakati wa utawala wa Sultani walikuwa na nafasi gani katika utawala? Sizungumzii watu weusi wanaojiona Waarabu - nazungumzia watu weusi ambao wanaonwa ni watu wa bara na masalio ya watumwa walikuwa na nafasi gani kabla ya Mapinduzi?

Zanzibar ina republicans na inao royalists.. hili halijabidilika na halitabadilika baada ya Muungano. Sawasawa na nchi nyingine ambazo zilifuta wafalme wao. Bado kuna watu wanajiona wana undugu wa karibu na Oman - kwa sababu ya Nasaba; lakini hawaoni wana undugu na Bara kwa sababu ya Nasaba hiyo hiyo!.

Watu wanadanganya - nje ya Muungano hakuna Zanzibar kuna Pemba na Unguja!! Na sababu itakayowafanya kutaka kutoka kwenye Muungano na wakakubaliwa itaifanya Pemba nayo kutaka kutoka kwa Unguja na sidhani kama kuna Waunguja watakaokataa.
 
Wildcat.. ndio maana swali moja ambalo hatujalisikia ni kuona Wazanzibari walioko Bara waandamane kudai nchi yao.. kwanini wanaodai Zanzibar ni walioko Zanzibar zaidi na nje ya nchi - London in particular? Binafsi ningependa waitishwe Wazenji walioko Dar waanza kuisumbua serikali ya TZ kama walivyofanya IRA kwa Waingereza kule.

Nyerere alisema kitu ambacho kinaukweli; wakishatoka kwenye Muungano watajikuta hakuna tena "Wazanzibari" bali kuna Wapemba na Waunguja na na Wabara. Hili ni kweli - ni Wazanzibari kwa sababu ya Muungano. Wanafikiri kwamba husuda na visasi vya kabla ya mapinduzi vimetoweka.

acha kasumba ...Kwanini Tanganyika masikini???? au wewe ndio wale wafuasi wa yule DIKTETA aliyewahi kutawala Tanganyika?
 
Huna hoja Ngalikihinja, si tuliambiwa tutakuwa kama Burundi?

Wacheni fitna zenu hizo, Zanzibar itakomboka tu Mungu akipenda.
 
Wakat wazenj hawapendi muungano, waingereza nao hawaipendi familia ya malkia (royal family). Wanadai inatumia hela zao vibaya na sio 'fair' kwamba wengine wawe bora zaidi kwasababu tu ni sehemu ya familia ya malkia (source:British Royal Wedding Blogs - Yahoo! Shine). Nini maana ya muungano? Inawezekana kuungana bila kupoteza 'opportunities' ambazo awali ulikuwa nazo? Ukiungana hakuna 'Opportunities' mpya zinazojitokeza? Kwanini Australia na New Zealand bado zipo chini ya himaya ya malkia? Kwa waznz mchawi wao sasa ni muungano, ni kawaida ya binadamu kutafuta mchawi.

Mkuu.
Hayo mawili kwenye nyekundu.

Mimi naona kuwa tumewasukuma to the limit hawa wazenj...kuifuta serikali ya Tanganyika na jina la sehemu,Tanganyika.....kuipa free pass ya kutumia mamlaka ya Muungano kwa mambo ya Tanganyika bila ya urasimu ambao Serikali ya zanzibar inapata katika kuendesha uchumi wake...kutanganza nia ya kutoka serikali mbili kwenda moja...lakini pia ahadi hewa za miaka mingi za kushughulikia "kero za Muungano" bila ya kutatua kero hizo.....pia siamini kuwa hawapendi Muungano..nilichokifahamu hawapendi Muungano huu kwa jinsi unavyoendeshwa na kuchakachuliwa.na wanadai kujadiliwa upya na kama haiwezekani basi uvunjwe.

Hilo la pili,mbona mifano inakimbia kidogo na kuacha uhalisia?
New Zealand, Austaralia hawana Benki kuu? Serikali zao zinapata vikwazo vya kuendeleza nchi zao kutoka kwa Malkia?

Kama ilivyo kwa waafrika kulalamika kila baya kwa wazungu..kweli naamini kuna mambo ambayo Zanzibar wangeweza kuyafanya wenyewe kama wangekuwa na "viongozi" lakini mambo ya Benki kuu na sera za kifedha zinakuwa manipulated na vyombo vya Muungano. Wana sehemu yao ya "uchawi" lakini na Muungano unawabana. Kivipi, kama kupitia serikali ya muungano wanapotaka kukopa kwa shughuli za maendeleo yao na sio mara zote kupata go ahead.

Mkuu. Muungano ni utata tu hata kwa Tanganyika, Viongozi wajanja tu ndio wananufaika katika Muundo wa Muungano uliopo,huku wananchi wakiachwa "kupata kikombe cha babu"
 
Endelea hivyo hivyo ... Lakini kwa taarifa yako Muungano utavunjwa, ukikasirika ,ukinuna, ukilia shauri yako... watu wa Zanzibar sio wazembe wala wajinga... Kama wewe mtanganyika huwezi kudai haki zako hilo juu yako... Na huwezi kufanya hivyo kwasababu wewe unafaidika zaidi na huu Muungano "fake". HEBU NAMBIE HUWO UWELEWO WAKO AU WENU, kWANINI TANZANIA (TANGANYIKA) MASIKINI?
AU WEWE UMERIDHIKA NA HALI YA MAISHA ILIVYO SASA... AU WEWE NI MIONGONI MWA WALE WALIOKO KATIKA SYSTEM KWAHIYO UMEWEKA PAMBA MASIKIONI... KERO ZA MUUNGANO SASA ZINA MUDA GANI ? AU MPKA SIKU MKIFURAHI NDIO MTATATUA HIZO KERO ? SASA WEWE UNATEGEMEA NINI BAADA YA MUDA WOTE BILA YA UFUMBUZI WOWOTE...
WATU WANATAKA UHURU WA MAMLAKA YA NCHI YAO...KAMA HILI LINAKUKERA BASI WEWE NI MKOLONI, MWEUSI . NA HII NI MBAYA ZAIDI ,KWASABABU WEWE MWENYEWE UNANJAA, HUJUI NINI UNAFANYA, KIGEZO ANGALIA NCHI YAKO...UMASIKINI ,PAMOJA NA RASILIMALI ZOTE ZILIZIPO... KAMA UNA ELIMU BASI HIYO ELIMU YAKO YA BURE, INAKUSAIDIA WEWE MWENYWEWE NA SIO MTU MWENGINE.
UJINGA KUKAA KIMYA...HOPING ONE DAY EVERYTHING WILL BE FINE...HATUTAKI MUUNGANO WA KULAZIMISHANA...PERIOD .

Takashi,
Tafdhali jibu hoja kama zinavyoletwa na wachangiaji. Tumewahi kukuonya kuwa hili si jukwaa la matusi, na kama ungependa hivyo rudi mzalendo.net. Usituvurugie mjadala kwa kupachika hoja chini ya kiwango na matusi, nadhani umekuwa kero ndani ya mjadala.

Tunaongelea muungano wa Tanzania ndio mada. Soma hapo juu utathimini mwenyewe kama unafaa kuwa sehemu ya mjadala huu, vinginevyo unawadhalilisha wenzako. Tafadhali waache wenye hoja na akili wasemezane.

Hili si jukwaa la kupiga mayowe, jibu hoja kwa hoja kama huna kaa kimya. Tunajua wenzetu huwa mna jazba, tunajua pia mnauwezo wa kujifunza kutoka kwa wenzenu, tafadhali ustaarabu na staha utakayoonyesha itawasitiri wazanzibar wote na aibu unayowatia.
 
hapo mwanakijiji anawazindua watanganyika mlo lala usingizi mzito amkeni mudai tanganyika yenu., wenzenu wa ZNZ Washaamka wanataka chao. Watanganyika ni wavivu wa kushiriki/kuelewa siasa.

Wanamdai nani na nini? Zanzibar in serikali, bendera yake, rais wake, bunge lake n.k, n.k. Ardhi yao ni yao peke yao (japo kuna Wazanzibari wanamiliki ardhi Bara (soma Tanganyika), KILICHOPORWA kutoka kwa Wazanzibari na Nyerere - or whoever - NI KIPI?????

Jamani, mna uwezo wa kujitoa HATA LEO HII. Kwa nini hamchukui hatua nyie msio wavivu wa kufikiri na kuelewa siasa? Au Wazanzibari ni hodari wa kulalamika (sio wavivu wa kulalamika) lakini WAVIVU KUPINDUKIA kuchukua hatua??
 
Wildcat.. ndio maana swali moja ambalo hatujalisikia ni kuona Wazanzibari walioko Bara waandamane kudai nchi yao.. kwanini wanaodai Zanzibar ni walioko Zanzibar zaidi na nje ya nchi - London in particular? Binafsi ningependa waitishwe Wazenji walioko Dar waanza kuisumbua serikali ya TZ kama walivyofanya IRA kwa Waingereza kule

Mkuu ndio maana hawataki kura ya maoni, wanajua kuwa wale wanaopiga kelele wapo uingereza na hawajui hali halisi.
Yule mznz anayetoka na mtumbwi kwenda kuvua halafu akashusha pweza feri, akaingia kariakoo akachukua viazi na kupeleka znz utamwambia muungano ni mbaya kwa hesabu zipi.
Yule mznz wizara ya fedha au utumishi anayesomwesha mtoto kuanzia vidudu hadi chuo kikuu akiwa bara utamwambia aandamane kwa lipi. Yule mpemba mwenye duka kariakoo utamwambia aandamane ili arudi pemba kumuuzia nani, n.k
Kiongozi gani wa znz asiye na makazi Dar! Ukisikia wameandamana ni London si Dar, wanajua nini wanapata.

Mnatakiwa mdai nchi yenu, kwanza mkiwa kwenu, lakini kupiga kelele ukiwa Dar haisadii, pelekeni hoja BLW ili mpate kinga ya kisheria mdai nchi yenu, ni haki yenu, vinginevyo ndio unafiki ninaousema, huwezi kuwa Dar halafu unalaani mfumo likokuwezesha kuwepo Dar!

Labda kwa kuanzia tu, wazanzibar mlioko Dar andamaneni kudai muungano uvunjwe, hapo tutajua mpo serious.
 
Mimi najiuliza kwamba je wanzibar kiuchumi mmoja mmoja hawajanufaika na muungano?kwa nini wasisusie Dar .Nikiangalia msururu wa wanasiasa ambao wana vyeo kutokana na muungano na walivyowekeza bara na matamshi wanayoyatoa wakiwa zenji ni kama wanafanya usanii .Yale maduka ya spea yaliyoko kariakoo mashamba ya mipunga waliyonunua kyela na sehemu nyingine za bara.Wapemba walivyohamiag kwa wingi Tanga.Kwa watu wa zenji walivyo huku bara sidhani kama wazo la kuvunja muungano wanalikubali ni kama unawaambia wapoteze mapato yao yanawaezesha kuishi kulea n.k.
 
Hao walihama kwao na kuhamia huko kutokana na fitna na ukandamizaji wenu. Sasa mnavuna mlichopanda. Hivi ndivyo mnavyoimarisha "muungano", sasa mnalalama nini dhidi ya Wapemba. Fanyeni kazi wacheni kuendekeza ufisadi:

Wapemba na Wazanzibari wako kila pembe ya dunia kwa ukoloni wenu mweusi.

View attachment 28312

View attachment 28313

Hii ngoma yenu ime backfire na sasa wa kulaumiwa ni hao viongozi wenu na wetu wanaofaidi matunda ya huu "muungano" feki na wanaowadanganyeni kila siku kuwa hii ni nchi moja.

Zanzibar for Zanzibaris and we cant wait to see your backs
 
Wildcat.. ndio maana swali moja ambalo hatujalisikia ni kuona Wazanzibari walioko Bara waandamane kudai nchi yao.. kwanini wanaodai Zanzibar ni walioko Zanzibar zaidi na nje ya nchi - London in particular? Binafsi ningependa waitishwe Wazenji walioko Dar waanza kuisumbua serikali ya TZ kama walivyofanya IRA kwa Waingereza kule.

Nyerere alisema kitu ambacho kinaukweli; wakishatoka kwenye Muungano watajikuta hakuna tena "Wazanzibari" bali kuna Wapemba na Waunguja na na Wabara. Hili ni kweli - ni Wazanzibari kwa sababu ya Muungano. Wanafikiri kwamba husuda na visasi vya kabla ya mapinduzi vimetoweka.

hii ni sahihi kabisa WA Zanzibar si wamoja hata kidogo. Umoja wao unatokana na kuchukia bara. nilikuwa kule kipindi cha uchaguzi - wale wana uhasama sana
siku wakiachwa watachinjana sana na hakutakuwa na kitu kinaitwa Zanzibar na tuombe Mungu siku hiyo isitokee
 
Back
Top Bottom