Ni wapi kwa Dar wanatoa huduma ya ujenzi wa nyumba aina hii?

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
39,902
95,407
Wakuu nazimia sana aina hii ya nyumba kwani zipo very simple,attractive,compact na zinakula nafasi ndogo sana.

Ni wapi kwa Dar wanatoa huduma ya ujenzi wa aina hii ya nyumba na gharama huwa ni sh ngapi?

Hizi nyumba huwa zinanivutia sana hasa kwenye design yake ilivyo,imagine haka hapa kana ghorofa moja pamoja na makorokocho kibao.

8NxJ.jpg
ErdPP.jpg
 
Simple but classic

Niliwahi kufanya kazi na makaburu siku za nyuma,kampuni ilikuwa imedesign containers kuwa vyumba.

Yaani container 1.linatengenezwa chumba kimoja kikubwa,ndani wameki design vizuri

Ukiwa ndani huwezi jua kama ni container

It's possible mkuu,ngoja wajuzi wa mambo waje wakujuze
 
Tatizo huna pesa za kumlipa fundi
Ndg unakosea sana, huyu mtu unamfahamu physically?
Je unahukumu kwa kuangalia id au avatar?
Je michango yake humu?

Huku wenye mizaha na majina mabovu ndio vifaru.
Hiyo nyumba ya kontena ni cheap kuliko unavyotaka kutuaminisha.

Je unataka kuwaona watu wote humu wachovu na hawajui ujenzi zaidi yako?

Bora unyamaze tu uheshimike au urudi kukimbiza uzi wako tu
 
Wakuu nazimia sana aina hii ya nyumba kwani zipo very simple,attractive,compact na zinakula nafasi ndogo sana..
Hata mie Kuna muda zilikuwa zinanivutia sema niliamua kwenda with crowds.

Ila cheki Kuna kampuni moja ivi ipo Kenya wanazijenga.

Afu sehemu za baridi ama joto chini 27 zinakuwa poa sana.mana hayo material ni good conductor of heat.ila hata kama wata insulate poa.

Pia kontena waweza pata 5M and above
 
Hata mie Kuna muda zilikuwa zinanivutia sema niliamua kwenda with crowds.
Ila cheki Kuna kampuni moja ivi ipo Kenya wanazijenga.
Afu sehemu za baridi ama joto chini 27 zinakuwa poa sana.mana hayo material ni good conductor of heat.ila hata kama wata insulate poa.
Pia kontena waweza pata 5M and above
Siku hizi sio lazima ununue kontena, unanunua bati na kuzikunja.
Kukunja bati moja ni 8,000 tu
 
Kontena moja ni milioni tatu. Why asiweze kununua hata matatu kujenga hiyo nyumba?!
Kwa muundo huu sio lazima ununue kontena, nunua hollow section tengeneza shape hiyo then una nunua bati kunja kwa muundo wa kontena, na uchomelee, inatoka kitu bomba sana.

Note; ni ms plates
 
Wakuu nazimia sana aina hii ya nyumba kwani zipo very simple,attractive,compact na zinakula nafasi ndogo sana.

Ni wapi kwa Dar wanatoa huduma ya ujenzi wa aina hii ya nyumba na gharama huwa ni sh ngapi?

Hizi nyumba huwa zinanivutia sana hasa kwenye design yake ilivyo,imagine haka hapa kana ghorofa moja pamoja na makorokocho kibao.
View attachment 1861941View attachment 1861942

Kaka hiyo ni kumtafuta fundi chuma mmoja akate na kuchomelea partition jinsi unavyotaka, aki reinforce hizo partiition na angle bar au square bar, then unaanza kupanga container zako kutokana na design unayohitaj,

ukiwa umeshaziwekea saddles ( nguzo za zege kushikilia hizo container.. ili kubalance centre of gravity na kuzi lock container kwenye hizo nguzo za zege isije upepo ukadondosha container la juu

baada ya kupanga na kukata bas tafuta fundi seremala mzuri mbao apige Marines boards zile nene ambazo zitakuwa kama kuta kwa ndan na nje pia chini na juu , baada ya hapo basi unatafuta mtu wa madirisha na milango anaweka kisha unamalizia na mtu wa wiring ya umeme plus mtu decor kwa ajili ya paints na finishing touches

kwa kifupi inakuwa ni nyumba ya bati na mbao.. kama nyumba za ulaya tu ambazo msingi zege ila kuta, ceiling na floor zote mbao, ndo maana wazungu ni rahs kuvunja nyumba ndan kuongeza upana wa sebule au jiko maana anatoa mbao anaweka. zingine. au akitaka mlango anatoboa mbao tu

ukitembelea warehouse nying za makampun ya hardware ujenzi au maviwanda ama haya makampuni ya nayofanya project kwenye remote locations mfano ujenzi wa barabara utaona makaz yao mengi ni containerized, kama kule moro kwenye bwana la nyerere, sema wao yanatengenezwa kutokana na mazingira husika..

hadi vyoo vinakuwa mobile wakihama kambi wanabeba tu .

ukitak ready made kutoka kwenye kampuni au kampuni ndo ikufanyie kazi hiyo utajikuta unalipia mara tatu ya gharama halisi..
 
Back
Top Bottom