Ni wangapi wanakumbuka jina la mwalimu wa darasa la kwanza?

Ina maana mi na wewe Mkuu ndio hatuna kumbukumbu eeee? 😜😜
mimi hawa wenzangu mkuu sijui kwann tumekutana huku JF wakat wana mauwezo YA kumbukumbu kiasi hicho (walitakiwa saivi wawe huko wanamshauri RAIS na kumkumbusha Timetable):D:D
 
Pole kwa kusahau Mtani, mimi nina walimu wangu kadhaa wa Primary, yaani siwasahau mpaka leo.

Std 1, alikuwa ana bonge la tabasamu halafu mdogo mdogo. Akaja akahamishwa, std 2 tukapewa mwingine, huyu alikuwa jirani yetu, term ya pili tukapewa mwingine tena.

Kwa hiyo 1-2 walimu watatu wote wa kike.
Safi sana Mtani.
 
Hahahaaa. Nimecheka sana Duuh.

Hapa ukiamua hata weye waeza mtaja wa uongo nani atajua kwani. :D:D:D

Hahaha, kuna kamba tunafungana humu JF si za kitoto.

Ila kumkumbuka mwalimu siyo kazi sana, mimi kila mwalimu aliyekuwa ananipenda namkumkumbuka.

Kuna mmoja alikuwa nikikosea ananipa fimbo kuwapita wote, akawa nikifanya vizuri ananipa zawadi nikawa simwelewi kabisa.
 
Hahahahaaa. Hapa labda itokee watu wakasoma shule moja na mwaka wa kuanza la kwanza ukawa mmoja ndio inaezekana mtu akaonekana anaongopa.

Ila nje ya hapo kamba hazizuiliki.

Walimu wa hivyo wapo sana tu na waeza kuta aliona una akili ila we una kauzembe na si wajua tena kila mwalimu anakuwa na wanafunzi wake darasani ambao anaona mwisho wa siku watamnyanyua.
 
Back
Top Bottom