Ni wakati sasa wa Dr. Rioba kujitathmini

Ni wakati sasa wa Dr. Rioba kujitathmini

K M S

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2016
Posts
524
Reaction score
424
Leo mkuu kapiga simu redio Clouds na kusema yake machache na kuwapongeza watendaji wa ATCL na wengineo kwa kazi nzuri wanaoifanya. Hii inamaanisha Mh. Rais ni msikilizaji mzuri wa radio hii na inavyoonekana amevutiwa na ubunifu wao katika kuandaa vipindi.

Ni wazi kuwa kule kwingine hakuna mvuto na ubunifu na hii inaashiria kuwa waliopewa dhamana si wabunifu. Sasa kwanini waendelee kukalia hivyo vyeo?

Dkt. Rioba jipime kabla hujapimwa!

HERI YA MWAKA MPYA
 
Hiyo TBC ni taasisi ya umma sio lazima ubunifu yenyewe inapata ruzuku kwahiyo hamna shida. Inasemekana eti yenyewe inafanya kazi kwa matakwa ya system, yaani ndio serekali yenyewe. Kuna jamaa alitoa povu hapa juzi ngoja ni mcc aje amwage tena povu.

cc: Mlau
 
Tbc ilishapote kitambo,
na sababu kubwa ni kutosahihisha makosa yanayotokana na utendaji wa serikali
kila kinachofanywa na serikali wao kazi ni moja tu kusifia bila kufanya uchambuzi ulio huru.
Nani ataangalia au kusikiliza habari ambayo tayari unajua itakavyokuwa?
 
C unajua mawingu ni ya nyumbani Kwa faru john sasa ulitakaje mkuu ,wewe umepitwa na ule usemi kua anayemlipa mpiga zumari ndie anachagua wimbo
 
Tbc ilishapote kitambo,
na sababu kubwa ni kutosahihisha makosa yanayotokana na utendaji wa serikali
kila kinachofanywa na serikali wao kazi ni moja tu kusifia bila kufanya uchambuzi ulio huru.
Nani ataangalia au kusikiliza habari ambayo tayari unajua itakavyokuwa?
Tbc hakuna waandishi wa habari kuna wasaka tonge. Kama wangekuwa waandishi hawange kubali kulishwa maneno. Acha waiue kabisa tujue hakuna chombo cha umma wawe kama gazeti la uhuru tunalofungiwa nalo maandazi huku mikoani.
Ati hawana pesa za kurusha bunge lakini wanazo za kumuonuesha Makonda akipita kambi ya fisi na kumpa coverage kwa masaa.
 
Ninaimani na Dr Rioba, hata iweje bado ni yule yule wa tume huru ya katiba.
 
Leo mkuu kapiga simu redio Clouds na kusema yake machache na kuwapongeza watendaji wa ATCL na wengineo kwa kazi nzuri wanaoifanya. Hii inamaanisha Mh. Rais ni msikilizaji mzuri wa radio hii na inavyoonekana amevutiwa na ubunifu wao katika kuandaa vipindi.

Ni wazi kuwa kule kwingine hakuna mvuto na ubunifu na hii inaashiria kuwa waliopewa dhamana si wabunifu. Sasa kwanini waendelee kukalia hivyo vyeo?

Dkt. Rioba jipime kabla hujapimwa!

HERI YA MWAKA MPYA
Ni aibu sana kwa Dr Ryoba kuzidiwa ubunifu na B12 au Adam Mchomvu .
 
Leo mkuu kapiga simu redio Clouds na kusema yake machache na kuwapongeza watendaji wa ATCL na wengineo kwa kazi nzuri wanaoifanya. Hii inamaanisha Mh. Rais ni msikilizaji mzuri wa radio hii na inavyoonekana amevutiwa na ubunifu wao katika kuandaa vipindi.

Ni wazi kuwa kule kwingine hakuna mvuto na ubunifu na hii inaashiria kuwa waliopewa dhamana si wabunifu. Sasa kwanini waendelee kukalia hivyo vyeo?

Dkt. Rioba jipime kabla hujapimwa!

HERI YA MWAKA MPYA

Hahahaaa! Tatizo kule Job Description inakipengele kimoja tu.... 1. Utatakiwa kusifia tu.

Kuna jamaa ana jina la silaha "Knife" na mwingine kama movie ya John Cena "Marine" wananiboa sana.
 
pesa wandugu pesa ndio inayonifanya ning'anie kwani hata mimi moyo unaniuma ila ndio hivyo tena nitafanyaje na ubunifu wangu ndio umeishia hapo
 
Kumbuka clouds ni chombo cha kibihashara n tofauti na TBC , then kumsifia. Mshondani wako sio tatzo, Bali ujue mbinu gani anatumia?ilo ndo swali na kujifunza sijaona tatzo kusifia mshindani mwenzío.sio kila ki2 tunalopoka2 tujifunze na tubadilike
 
Vijana tupunguze mihemko ya kisiasa mana kila ki2 tunaingiza siasa
 
Vijana tupunguze mihemko ya kisiasa mana kila ki2 tunaingiza siasa
Siasa inatoka wapi mkuu wakati mambo yako wazi tuambie nilini TBC wamepigiwa simu kwa staili kama hii
 
TBC wanaambiwa mini watangaze na mini wasitangaze. Ubunifu utoke wapi ? Rioba alikuwa mkosoaji nje ya uwanja, Sasa amepewa Nazi ulimi unamtoka anaomba dakika 90 ziishe. Keisha kabisa.
 
Back
Top Bottom