Ni wakati sasa kwa Serikali kumuomba radhi Tundu Lissu aliyeshauri mapema kuachana na madai ya Barrick

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Ripoti za Mruma na Osoro juu ya Barrick/Acacia kulimbikiza deni hadi kufikia Trln 425 zilizua mjadala mkubwa ambapo aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alizikosoa na kuziita ni “Professorial Rubbish Report”.

Lissu alitoa ushauri wake kuwa kutokana na repoti hizo Barrick hawatalipa hilo deni na wakilazimishwa wakienda MIGA watashinda. Lissu alibezwa alipuuzwa na baada ya siku chache alimiminiwa risasi kuwa ni msaliti anayeshirikiana na mabeberu.

Barrick walitoa fedha za (Good faith) US$ 300M sawa na tsh 700b tu kati ya deni lote.

Jana Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kwa niaba ya serikali amesema serikali imeisamehe Barrick/Acacia deni lote.

Imeichukua serikali miaka mitano 5yrs kukubaliana na ushauri wa Lissu.

Uungwana ni vitendo mnyonge mnyongeni lakini haki zake apewe, Tundu Lissu aombwe radhi.

June 19, 2017
69E98F6A-005A-461E-9451-0AE1EA938BBC.jpeg
 
Ripoti za Osoro na Mruma juu ya Barrick/Acacia kulimbikiza deni hadi kufikia Trln 425 zilizua mjadala mkubwa ambapo aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alizikosoa na kuziita ni “Professorial Rubbish Report”.

Lissu alitoa ushauri wake kuwa kutokana na repoti hizo Barrick hawatalipa hilo deni na wakilazimishwa wakienda MIGA watashinda. Lissu alibezwa alipuuzwa na baada ya siku chache alimiminiwa risasi kuwa ni msaliti anayeshirikiana na mabeberu.

Barrick walitoa fedha za (Good faith) US$ 300M sawa na tsh 700b tu kati ya deni lote.

Jana Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kwa niaba ya serikali amesema serikali imeisamehe Barrick/Acacia deni lote.

Uungwana ni vitendo mnyonge mnyongeni lakini haki zake apewe, Tundu Lissu aombwe radhi.
Mkuu waombe Moderators waweke hiyo VIDEO hapo juu...lilikuwa swala la Muda tuu...pengo la Chadema huko Bungeni hata chekechea Analitambuwa....
 
Ripoti za Osoro na Mruma juu ya Barrick/Acacia kulimbikiza deni hadi kufikia Trln 425 zilizua mjadala mkubwa ambapo aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alizikosoa na kuziita ni “Professorial Rubbish Report”.
Japo ni kweli lakini sio busara kufanya ukosoaji kwa kutumia maneno makali yenye lugha ya maudhi, wewe huna Ph.D, ripoti ya Ph.D holder, huwezi kuita "a professior rubish". Hata akina sisi tuliikosoa ripoti hiyo lakini tulitumia lugha ya kistaarabu! Sensationalism kwenye Professional Presentations inakubalika? Ni swali tu...

Jana Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kwa niaba ya serikali amesema serikali imeisamehe Barrick/Acacia deni lote.
Serikali, mabenki na taasisi za fedha ziko huru kusamehe sehemu ya deni au deni lote, kitu muhimu ni wenye fedha zao kujulishwa. Licha ya umasikini wote uliotopea wa nchi yetu, hakuna ubaya wowote kusamehe deni lolote kwa yeyote, lakini lazima utoe sababu why unasamehe, ila pia unaposamehe majizi ndio muhimu zaidi kuwa transparent, ili isije kuonekana viongozi wetu wamekuwa compromised !.
Uungwana ni vitendo mnyonge mnyongeni lakini haki zake apewe, Tundu Lissu aombwe radhi.
Kwenye hili hebu msikilizeni kwa makini,

View attachment 2366449

Mtu anayeongea lugha hizi, ombwe radhi kwa lipi?. Ila pia Tundu Lissu aliishaondoa hilo neno "professiol rubish"
P
 
Ripoti za Mruma na Osoro juu ya Barrick/Acacia kulimbikiza deni hadi kufikia Trln 425 zilizua mjadala mkubwa ambapo aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alizikosoa na kuziita ni “Professorial Rubbish Report”.

Lissu alitoa ushauri wake kuwa kutokana na repoti hizo Barrick hawatalipa hilo deni na wakilazimishwa wakienda MIGA watashinda. Lissu alibezwa alipuuzwa na baada ya siku chache alimiminiwa risasi kuwa ni msaliti anayeshirikiana na mabeberu.

Barrick walitoa fedha za (Good faith) US$ 300M sawa na tsh 700b tu kati ya deni lote.

Jana Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kwa niaba ya serikali amesema serikali imeisamehe Barrick/Acacia deni lote.

Uungwana ni vitendo mnyonge mnyongeni lakini haki zake apewe, Tundu Lissu aombwe radhi.
Mataga watakuja kupongeza uhamuzi wa serikali kusamehe. Watasema ni uungwana
 
Japo ni kweli lakini sio busara kufanya ukosoaji kwa kutumia maneno makali yenye lugha ya maudhi, wewe huna Ph.D, ripoti ya Ph.D holder, huwezi kuita "a professional rubish". Hata akina sisi tuliikosoa ripoti hiyo lakini tulitumia lugha ya kistaarabu! Sensationalism kwenye Professional Presentations inakubalika? Ni swali tu...

Serikali, mabenki na taasisi za fedha ziko huru kusamehe sehemu ya deni au deni lote, kitu muhimu ni wenye fedha zao kujulishwa. Licha ya umasikini wote uliotopea wa nchi yetu, hakuna ubaya wowote kusamehe deni lolote kwa yeyote, lakini lazima utoe sababu why unasamehe, ila pia unaposamehe majizi ndio muhimu zaidi kuwa transparent, ili isije kuonekana viongozi wetu wamekuwa compromised !.

Kwenye hili aombwe radhi kwa lipi?.
P
Kwa hiyo mtu akiwa na PhD akiongea/kuandika ujinga uitwe werevu kisa yeye amesoma ana PhD?
Mm nasema hapana ujinga ni ujinga hata kama mtu ni mzee,ana digrii milioni tuwe wakweli kuna wasomi nchi hii ni mizigo na useless kabisa.
 
Tuchukue calculator ili kujua tulivyopigwa.

Nini thamani ya usd 300 mil kishika uchumba dhidi ya deni la usd 191 billion.

191 000 000 000 ÷ 300 000 000 = 636.66

Ingewachukua Barrick miaka 637 kumaliza deni letu kama wangetulipa usd 300 mil kila mwaka.
 
Kila mwenye akili timamu alijua kuwa madai yale ulikuwa uwongo mkubwa. Ni sawa uambiwe kuwa mwenye duka la mtaji wa 2m anadaiwa kodi ya sh 2 bilioni. Lazima uwe punguani kiasi kuweza kuliamini hilo.

Total gold resource ya migodi yote ya Barrick kwa Tanzania ni 0.75MOz Tulawaka + 4MOz Buzwagi + 7MOZ North Mara + 12MOZ Bulyanhulu = 23.75MOz. Mineable resource haiwezi kuzidi 60% = 14.25MOz. Dhahabu iliyokwishachimbwa, japo sina uhakika, haiwezi kuzidi 50%.= 7.1MOz. Thamani ya hii dhahabu iloyochimbwa, kwa bei ya juu kabisa, ya U$2,000 kwa oz = $14 billion (14 billion ×2,300 = TZS 32 trillion)

Hata ungesema hiyo hela yote iwe kodi, halafu wasiwe wametoa kodi hata shilingi moja, bado haifikii hata 10% ya trilioni 360 ambayo waliotuona wajinga walikuwa wakituaminisha.

Hata kama walitaka kuwadanganya wananchi, wangeweka huo uwongo wao uwe unakaribia na ukweli. Lakini wahusika kwa vile walijua wanaongoza nchi ya wasio na kitu vichwani, walijua wapo wenye vichwa vitupu kabisa, ambao ni wengi, watashangilia na kuwaona ni mashujaa. Uwongo ule ni miongoni mwa mambo yaliyotufanya waafrika tuendelee kuonekana kuwa siyo binadamu timilifu.

Kwa namna ambavyo baadhi ya watu wakati ule walivyokuwa wameshibishwa ujinga, hata wangeambiwa kuna mpango wa Serikali wa kumnunulia kila mwananchi ndege aina ya Boeing 737-800, wangeshangilia na kusema tumepata mkombozi. Ujinga ni laana kubwa, hasa ujinga ule unaoelekea kwenye upumbavu.
 
Quinine,

..kuna mahali nilisoma kwamba acacia nao walikuja na madai ya usd 174 million dhidi yetu.

..kwa hiyo upo uwezekano kwamba hata hizo usd 300 million hatukuzipata zote.

Kila kitu kilifanywa kwa usiri mkubwa, halafu Magufuli akawa anawahadaa wetu kwa kuwaita viongozi wa dini , sijui makundi mbalimbali kwenye hizo hafla za utapeli wake. Cha kushangaza watu walikuwaje wajinga kiasi kile cha kuamini maigizo yale.

Halafu bunge lilikuwa halishirikishwi kabisa kwenye mambo yale, kisa Magufuli alikuwa hataki yajadiliwe bungeni maana wabunge wa upinzani wataweka wazi mambo hayo. Mambo haya ndio yalipelekea Magufuli anajisi chaguzi za nchi hii na kujaza wanaccm aliowataka yeye ili kusitokee yoyote wa kuhoji. Jambo hili ndio lilipelekea Lisu kupigwa risasi.
 
Japo ni kweli lakini sio busara kufanya ukosoaji kwa kutumia maneno makali yenye lugha ya maudhi, wewe huna Ph.D, ripoti ya Ph.D holder, huwezi kuita "a professional rubish". Hata akina sisi tuliikosoa ripoti hiyo lakini tulitumia lugha ya kistaarabu! Sensationalism kwenye Professional Presentations inakubalika? Ni swali tu...

Serikali, mabenki na taasisi za fedha ziko huru kusamehe sehemu ya deni au deni lote, kitu muhimu ni wenye fedha zao kujulishwa. Licha ya umasikini wote uliotopea wa nchi yetu, hakuna ubaya wowote kusamehe deni lolote kwa yeyote, lakini lazima utoe sababu why unasamehe, ila pia unaposamehe majizi ndio muhimu zaidi kuwa transparent, ili isije kuonekana viongozi wetu wamekuwa compromised !.

Kwenye hili aombwe radhi kwa lipi?.
P
Kwani kimantiki professorial rubbish ni kitu kisichowezekana? Ile report ilikuja na viwango vya ajabu vya madini na ikapelekea wataalamu wetu kuja na makisio ya ajabu kabisa ni nini tunawadai acacia.

Na toka waliporejea kupeleka hayo makinikia hawaja thubutu kutueleza ni kiwango kipi kimekutwa. JPM asingechelea kuonyesha kuwa lissu hakusema ukweli.

Hivyo report ile ilijaa hadaa. Sasa tunajua ni mengi tu baba yule alituhadaa. Na report zile hazikuwa sahihi. Zilikuwa Professorial rubbish.
 
Back
Top Bottom