Tundu Lissu jitafakari juu ya sumu uliyoimwaga Ulaya na Marekani kuhusu nchi yetu na Serikali yake kabla ya kurejea kugombea Urais

Professional Trader

JF-Expert Member
Apr 5, 2016
1,220
1,113
TUNDU LISSU JITAFAKARI JUU YA SUMU ULIYOIMWAGA #ULAYA NA #MAREKANI KUHUSU NCHI YETU NA SERIKALI YAKE KABLA YA KUREJEA KUGOMBEA URAIS:

Nataka niseme bila kumung'unya maneno kwamba, raia yeyote, wa nchi yeyote duniani, iwe Marekani, China, Ujerumani au Uarabuni, mwenye kujaribu au kuthubutu kufanya usaliti dhidi ya nchi yake, haijalishi ni usaliti wa kiusalama au wa kiuchumi, kamwe hajawahi kuwa sehemu ya watakatifu wala hakuna serikali mahali popote duniani iliyowahi kushirikiana na mtu au watu wa aina hiyo.

Hii tafsiri yake ni kwamba, ukishaamua kuisaliti nchi yako, basi ujuwe kwamba umejitangazia vita wewe mwenyewe. Huo ndiyo ukweli na utabakia kuwa ukweli mchungu.

#Baba wa taifa hayati Mwl. Nyerere aliwahi kutuonya kwenye moja ya hotuba zake kwamba, kama kweli tumedhamiria kujenga taifa la haki lisilo la wanyonyaji, kamwe hatuwezi kuogopa kelele za wapumbavu na wanyonyaji.

Tutapata matatizo, tutapata misukosuko, Tutapata majizi humu humu, Tutapata watetezi wa mabepari humu huku, lakini nchi itakwenda. Na mimi nirejee kauli ya Rais wangu Dkt. John Pombe Magufuli kwamba, Tumechelewa mno, #Tumechezewa sana, Tudhamiria nchi iende, atakaye jaribu kutukwamisha, atakwama yeye.

Katika vita ya kiuchumi iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Jemadari Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ikiwemo kukamata makontena ya mchanga wa dhahabu zaidi ya 200 yaliyokuwa bandari ya Dar es Salaam, Rais Magufuli kwa uchungu mkubwa alisema:-

Namnukuu. Nimeamua kuyatoa maisha yangu sadaka kwa ajili ya kuwapigania watanzania ikibidi hata nife. Maisha yangu hayatakuwa na thamani kama Rais kwa kuona watanzania wakifa kwa kukosa dawa hospitali, watoto wa masikini wakikosa elimu, hali ya usafiri ikiwa mbaya, halafu mimi niwe sehemu ya wanaoshiriki kuhujumu taifa hili kwa kufukuzana na machinga barabarani huku tukiacha kukusanya kodi kwa wanaokwepa kulipa kodi ya serikali. Nimeamua nchi iende na atakayejaribu kutukwamisha, atakwama yeye mwenyewe. #MwishoKunukuu.

Wakati Rais wetu akiapa kiapo cha kulitumikia taifa, mwenzetu Tundu Lissu aliamua kusimama upande wa wanyonyaji ACACIA na BARRICK badala ya kusimama upande wa nchi. Tena alienda mbali kwa kumtishia nyau Rais wetu kwamba, kitendo alichofanya cha kukamata mali za wawekezaji kitapelekea nchi kushitakiwa kwenye mahakama za Kimataifa za usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji kwa mujibu wa mikataba iliyopo.

Kitendo cha kutetea #unyonyaji wa rasilimali za taifa ziendelee kuporwa kwa kunufaisha wachache badala ya kulinufaisha taifa, hiyo peke yake ilitosha kumtambulisha Tundu Lissu kwa watanzania kwamba yeye ni adui namba moja kuliko walivyo wanyonyaji wa uchumi wetu ikiwemo kampuni ya kuchimba dhahabu ya ACACIA tuliyoambiwa ilikuwa ikichimba dhahabu nchini bila kusajiliwa popote.

Nataka niseme kwamba, kama taifa tumepigana vita ya kutetea rasilimali za nchi yetu ikiwemo madini kwa kuanza na kutunga sheria, tukasimama kidete, kuzungumza na wawekezaji, Mungu akasimama upande wetu, na hatimaye tukashinda. Sasa tunayo kampuni ya kizalendo ya ubia kati ya Tanzania na Barrick iitwayo Twiga ambayo tunagawana faida 50x50.

#Lisu alikuwa tayari kwa lolote ili kutengeneza Nchi ikose Utulivu na Mungu alivyo wa pekee leo mpango huo muovu ulioupanga umegharibu maisha yake.

Wakati #serikali ikipambana kutetea rasilimali zake ili ziwanufaishe wananchi, kwa upande wake yeye Tundu Lissu alikuwa akipambana kuzunguka Ulaya na Marekani kumwaga sumu kwa nchi wafadhiri ili nchi yetu inyimwe misaada, iwekewe vikwazo vya kiuchumi. Kama vile hiyo haikutosha, akajitoa kimasomaso kwa ajili ya kusaidia wenye madeni na Tanzania kukamata ndege zetu huko Canada na Afrika kusini, lengo likiwa ni kuhakikisha serikali ya awamu ya tano inakwama. Wahenga walisema Mungu si Athumani, hatimaye licha ya figisu figisu, tumeingia uchumi wa kati.

#Napata taabu sana, #ninapomtafakari mtu wa aina hii, anapata wapi ujasiri na nguvu za kufikia hatua ya kutangaza kugombea Uraisi wa nchi ambayo ameshiriki kuibomoa tena kwa mikono yake mwenyewe? Hivi ni nani aliyemshauri Tundu Lissu atangaze kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kama hakushauriwa na mtu isipokuwa ni mawazo yake, wakati anawaza kugombea uraisi alikuwa ndotoni au? Yaani uje ugombee urais, ufaidi matunda ya vita ya kiuchumi ambayo hukuipigania? Wewe ni nani? Nina hasira, Sitaki kusema sana, Wakati ni ukuta, tunamsubiri.

Nimecopy kutoka kwa mdau mmoja uko facebook ILA UJUMBE UWAFIKIE VIJANA WOTE WAFUATA UPEPO NA MANENO YA VIJIWE WA CHADEMA MJITAFAKALI
 
Ni hivi, Tundu Lissu atarejea hapa nchini taka msitake. Magufuli hana jinsi zaidi ya kujiandaa kushindana naye kwenye uchaguzi, maana hiyo ndio demokrasia. Tunaujua vyema uzalendo wa Tundu Lissu na wala hatuna muda wa kusubiri kuhadithiwa na yoyote. Nyie mnaoleta hizi porojo ni wafaidika binafsi wa madaraka ya Magufuli, hivyo ni lazima mpange mapambio ya kumtetea ili familia zenu ziende choo.

Tunajua mgombea wenu hana uwezo wa kushindana kwa hoja, na hizi ngonjera ni ili kumuepusha na ushindani ambao anapaswa kukutana nao. Ajiandae kukabiliana na ushindani ili ajieleze vizuri. Dunia ya kulisha watu matakwa ya kiongozi tu imeshapita.
 
Wapi Azory, wapi Ben Saanane, wapi katiba mpya ambayo ndiyo msingi mkuu wa hayo yote uliyoyaandika...leta majibu kwanza kisha uje tuongee hoja yako..
Ni kweli watanzania hawa si mbumbumbu kama tunavyofikiri.

Kwa akili yako katiba mpya ndio inaweza kuleta maendeleo tanzania? Au uyo ben alikua ni nan ni mtu anayetoa ajira zaidi ya elfu 1000 Tanzania? .....Mkuu wakati mwengine uwe unaongea mambo makubwa yenye tija kwa Taifa acha ujinga wa kulilia watu wasio na tija yeyote kwa taifa (hayupo na mambo yanaenda safi kabisa). ....Katiba ni ile ile na mambo yanaenda kwa kufuata katiba iliyopo, kenya wamebadili katiba ndio nini cha ajabu kimetokea / Watanzania kwa sasa hatutaki poyoyo tunataka mfanya kazi mtemda kazi kweli sio poyoyo nyingi badilikeni wakuu
 
Tunaelewa maana ya neno Msingi? Ulishasikia mtu anajenga nyumba bila msingi?

Sasa ndiyo haya ya kumsujudu mtu ambaye hafuati katiba na sheria za nchi...upoyoyo
 
Ni hivi, Tundu Lissu atarejea hapa nchini taka msitake. Magufuli hana jinsi zaidi ya kujiandaa kushindana naye kwenye uchaguzi, maana hiyo ndio demokrasia. Tunaujua vyema uzalendo wa Tundu Lissu na wala hatuna muda wa kusubiri kuhadithiwa na yoyote. Nyie mnaoleta hizi porojo ni wafaidika binafsi wa madaraka ya Magufuli, hivyo ni lazima mpange mapambio ya kumtetea ili familia zenu ziende choo.

Tunajua mgombea wenu hana uwezo wa kushindana kwa hoja, na hizi ngonjera ni ili kumuepusha na ushindani ambao anapaswa kukutana nao. Ajiandae kukabiliana na ushindani ili ajieleze vizuri. Dunia ya kulisha watu matakwa ya kiongozi tu imeshapita.

Kwa bahati nzuri Kipindi iki Watanzania Wanajua Mbivu ni ipi na mbichi ni ipi ngoja tuone 🤣
 
Kwanza kwa jinsi alivyoitukana Tanzania ni dhambi kubwa akifika bongo akabaki uraiani.
 
Back
Top Bottom