Ni wakati muafaka wa Kurekebisha Taasisi za TRA na PCCB kufanya kazi kwa Weledi

AeIoU

Senior Member
Mar 14, 2008
178
139
Katika kipindi cha awamu ya tano kilichojibatiza na kujiita serikali ya "mwendazake" ampapo mzee wa Lupaso RIP Ben Mkapa alilikemea hilo bila kificho.

1. TRA waligeuka kuwa genge fulani la wahalifu kwa kupora pesa kwa wafanyabiashara kwa kuwabambikiza kodi za juu na za uongo ili kutengeneza mazingira ya rushwa. Hii ilisababisha biashara nyingi kayumba na hatimae kufungwa kabisa. Ndio maana Commissioner General Dr. Mhede aliondolewa kabisa.

2. Nao PCCB waliachana kabisa na core function yao wakawa maagent wa kukusanya madeni na ukwapuaji wa pesa za watu na ndio maana hata yule Director General Brigadier General Mbungo ndio maana aliondolewa na Rais Mama Samia kwa kuwa alikuwa hajui kabisa abachokifanya.

3. Baada ya kuona kama hawatakushinda kama umetii masharti yote na una haki zote TRA walikuwa wanaungana na PCCB na kuwabambikiza watu kesi za uhujumu uchumi ambazo kimantiki nyingi hazikuwa za ukweli.

Sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa maadili Raisi wetu na kipenzi chetu Mama Samia anapisema "na kazii iendelee" tafsiri yake haipo kimaneno kama inavyotamkwa bali ni kivitendo zaidi hii maana yake kwa tafsiri yangu mimi nionavyo haina mshazari kabisa na ile ya mwendazake "hapa kazi tuu" bali ni fumbo kwa wasioelewa kuwa na ile kazi ya zamani ya kukandamiza wanyonge wa Tanzania na iendelee? Jibu ni hapana!

Nakaribisha mitazamo tofauti!
 
Back
Top Bottom