Ticktock dork
JF-Expert Member
- Dec 23, 2015
- 466
- 306
Nabii Elia alipaa moja moja hakufa
but alirudi kama yohana mbatizaji then akafa.
angalia mathayo 11:2-14
malaki 3:1
malaki 4:5
Nabii Elia alipaa moja moja hakufa
Naomba link ya mada yako ya paji la uso, nilisema nikitulia nitasoma ghafla siuoni uziSawa lakini safari hiyo baada ya kukata kamba huchukua muda gani? Tinatambua mimba huchukua si chini ya miezi 9.. Tangu kutungwa mpaka kuzaliwa mtoto.. Kifo je?
Jr
Paji la uso na siri ya jicho la tatu - JamiiForumsNaomba link ya mada yako ya paji la uso, nilisema nikitulia nitasoma ghafla siuoni uzi
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi Mkuu hizi tamaduni mila na desturi zikichanganya na Imani kuna ubaya wowote au kuna makosa maana kuna mambo bado inanipa shida sana kuelewaTamaduni (mila na desturi) vinapokutana pamoja na imani
Ni vema kila kitu kisimame chenyewe na ukitaka kuvichanganya inataji werevu mwingi tafakari na uchaguzi sahihiHivi Mkuu hizi tamaduni mila na desturi zikichanganya na Imani kuna ubaya wowote au kuna makosa maana kuna mambo bado inanipa shida sana kuelewa
Asante Mkuu, naomba kujua kuna darasa maalumu la kujifunza haya mambo ili kuwa mwerevu, na je unaweza kunisaidia kupata darasa hilo? natanguliza shukurani.Ni vema kila kitu kisimame chenyewe na ukitaka kuvichanganya inataji werevu mwingi tafakari na uchaguzi sahihi
Jr
Binadamu tuna tatizo la kujitambua. Tunadhani sisi ni mwili na akili then tuna uhai na hatu Binadamu akifa basi tunadhani maiti ndio thamani yote ya mwanadamu. Embu tugeuze mtazamo wetu, tuseme hivi, Binadamu ni Roho yenye Mwili na Akili. Ukigeuza hivi unapata picha sahihi ya alichokieleza mtoa maada.
Roho haifi bali inatoka kwenye mwili iliyokuwa inau maintain (kuumba) kwa kuupa misosi, Maji na Pumzi, ambavyo vya dunia hii, Lakini pia kuna sababu maalumu ya kuwa kwenye huu mwili, sasa saa ya kufa imeshwadia katika hali ile unarudi kenye moment ya siku ulikuwa unaingia kwenye mimba iliyotungwa na kwa yai na mbegu za wazazi unajua kwanini ulipaswa kuzaliwa yaani what was the mission in life na you did not fulfill your mission, you how it is difficult to find another body kwani kusiwe na kujuta, mataabiko, maumivu wakati wa kukata Roho?.
Kuna wale waliofanya Astral body projection (mbinu ya kutoka kama uhai kenye mwili na kurudia mwili) wanaweza elewa Roho inajielewa hata ikiwa nje mwili kwani inabakia kuwa na impression hii geuka geuka ya Maiti au kucheka bado kunabakia trace ya Roho kwenye mwili, na kwasabu wakati huo Roho inajua hasa ilipaswa kufanya nini maisha yake inapigana kurudia mwili japo kwa muda ili ikamilishe mission yake. Lakini kwa mujibu wa law of nature inashindikana kwa sababu kama ndio mtihani jamaa anamajibu yaani Anadesa. Baada ya kuucha mwili kwa muda bado kuna impression za ubinafsi yaani Ego, Lust, Attachment inakuwa naxo, Roho itabaki kurandaranda na kujaribu kuwa na awapendao mpaka impression zinapo ware out ndio mission ya kutafuta another body inaanza.
Vitabu vya dini vinaposema tumeumbwa mfano wa mungu ndio maana yake, sisi Roho hatuonekani kwa macho ya kawaida kama vile hatuwezi muona Mungu kwa macho yetu.
Nibishie... jifanye kama unajikuna
Sent using Jamii Forums mobile app
Sisi huomboleza wapendwa wetu wanapokufa. Huenda tukauliza: ‘Wameenda wapi? Je, wanateseka? Je, wanaweza kutusaidia? Je, tunaweza kuwasaidia? Je, tutawaona tena?’ Dini za ulimwengu hujibu maswali haya kwa njia tofauti-tofauti. Baadhi ya dini hizo hufundisha kwamba ukiishi maisha ya uadilifu, utaenda mbinguni lakini ikiwa unaishi maisha mabaya, utateketezwa motoni. Dini nyingine hufundisha kwamba watu wanapokufa huenda kuishi katika makao ya roho pamoja na mababu zao. Na nyingine hufundisha kwamba wafu huenda ahera wakahukumiwe kisha huzaliwa upya katika mwili mwingine.
Dini zote hizo zinafundisha jambo moja la msingi, kwamba sehemu fulani ya mwanadamu huendelea kuishi baada ya mwili kufa. Karibu kila dini, za zamani na za sasa, husema kwamba sisi huendelea kuishi milele tukiwa na uwezo wa kuona, kusikia, na kufikiri. Hata hivyo, hilo linawezekanaje? Hisia zetu, pamoja na mawazo yetu, zinahusiana na jinsi ubongo wetu unavyofanya kazi. Ubongo huacha kufanya kazi mtu anapokufa. Kumbukumbu letu na hisia zetu haziendelei kufanya kazi baada ya ubongo kufa.
Mfano, katika Biblia
Mungu , Muumba wa ubongo anajua kinachotukia tunapokufa. Anajua ukweli na katika Neno lake, Biblia, anaeleza hali ya wafu. Biblia inafundisha hivi waziwazi: Mtu anapokufa, hayupo tena. Kifo ni kinyume cha uhai. Wafu hawaoni, hawasikii wala kufikiri. Hakuna sehemu yoyote ya mwili wetu inayoendelea kuishi baada ya mwili kufa. Hatuna nafsi au roho isiyoweza kufa. *
Jiulize swali; Moto huenda wapi unapozimika?
Baada ya Sulemani kutaja kwamba walio hai wanajua kwamba watakufa, aliandika hivi: “Lakini wafu, hawajui lolote kamwe.” Kisha akafafanua kweli hiyo ya msingi kwa kusema kwamba wafu hawawezi kupenda wala kuchukia na kwamba “hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi.” (Mhubiri 9:5, 6, 10)
Mkuu bila shaka wewe ni shahidi wa JehovaSisi huomboleza wapendwa wetu wanapokufa. Huenda tukauliza: ‘Wameenda wapi? Je, wanateseka? Je, wanaweza kutusaidia? Je, tunaweza kuwasaidia? Je, tutawaona tena?’ Dini za ulimwengu hujibu maswali haya kwa njia tofauti-tofauti. Baadhi ya dini hizo hufundisha kwamba ukiishi maisha ya uadilifu, utaenda mbinguni lakini ikiwa unaishi maisha mabaya, utateketezwa motoni. Dini nyingine hufundisha kwamba watu wanapokufa huenda kuishi katika makao ya roho pamoja na mababu zao. Na nyingine hufundisha kwamba wafu huenda ahera wakahukumiwe kisha huzaliwa upya katika mwili mwingine.
Dini zote hizo zinafundisha jambo moja la msingi, kwamba sehemu fulani ya mwanadamu huendelea kuishi baada ya mwili kufa. Karibu kila dini, za zamani na za sasa, husema kwamba sisi huendelea kuishi milele tukiwa na uwezo wa kuona, kusikia, na kufikiri. Hata hivyo, hilo linawezekanaje? Hisia zetu, pamoja na mawazo yetu, zinahusiana na jinsi ubongo wetu unavyofanya kazi. Ubongo huacha kufanya kazi mtu anapokufa. Kumbukumbu letu na hisia zetu haziendelei kufanya kazi baada ya ubongo kufa.
Mfano, katika Biblia
Mungu , Muumba wa ubongo anajua kinachotukia tunapokufa. Anajua ukweli na katika Neno lake, Biblia, anaeleza hali ya wafu. Biblia inafundisha hivi waziwazi: Mtu anapokufa, hayupo tena. Kifo ni kinyume cha uhai. Wafu hawaoni, hawasikii wala kufikiri. Hakuna sehemu yoyote ya mwili wetu inayoendelea kuishi baada ya mwili kufa. Hatuna nafsi au roho isiyoweza kufa. *
Jiulize swali; Moto huenda wapi unapozimika?
Baada ya Sulemani kutaja kwamba walio hai wanajua kwamba watakufa, aliandika hivi: “Lakini wafu, hawajui lolote kamwe.” Kisha akafafanua kweli hiyo ya msingi kwa kusema kwamba wafu hawawezi kupenda wala kuchukia na kwamba “hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi.” (Mhubiri 9:5, 6, 10)
Big up mkuuWakati wa mafunzo yangu huko mbali na baadae kazini nilipata mara si haba wasaa wa kukaa na wagonjwa waliokuwa katika dakika zao za mwisho za kufariki... Wachache nilikuwa nao mpaka roho inaachana na mwili.... Maisha yana vitu vinauma na kuumiza sana... Lakini hakuna maumivu makali kama pale roho inapotaka kujitenga na mwili... Ni tendo moja gumu sana.. Na unayaona wazi mahangaiko ya mfu mtarajiwa....
Nimeshiriki pia mara si haba kuwapokea wafu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti(mortuary) na kuwahifadhi wengine hadi wiki na ushee...Nimeshiriki kuwaandaa marehemu kwa ajili ya kuagwa mara ya mwisho na wapendwa wao... Nimeshiriki kuzika kwa udongo.. Na nimeshiriki si mara haba kuwachoma moto marehemu kama utamaduni wao unavyotaka
Kote huko niligundua kitu kimoja kikubwa sana... Kifo sio jambo la maramoja linaloishia hapo hapo... Kifo ni mchakato unaoanzia tangu kutungwa kwa mimba, kuzaliwa, kufa na mwendelezo baada ya kufa..
Mfu anakuwa mfu kwasababu tu roho imetengana na mwili.. Lakini kuna uhai usioonekana unabaki mpaka pale makaburini! Na ndio maana kuna simulizi nyingi za marehemu kabla hawajazikwa na hata baada ya kuzikwa...
Baadhi ya vituko hivyo ni
. maiti kununa ama kutabasamu
. maiti kukunja uso
.maiti kugeuka kidogo
. maiti kukataa kusafirishwa
. maiti kukataa kuvalishwa nguo
. maiti kushindikana kabisa kubebwa nknk
Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye imani zetu kuhusiana na swala zima la pepo na kuzimu(akhera) na uhalisia wa mfu kufika kuzimu ama peponi muda gani...
Mchakato wa mtiririko wa kikristo uko hivi
Mateso
Kifo
Kuzikwa
Kushuka kuzimu (kwa tafsiri ya hapa kuzimu kuko chini ya kaburi)
Baada ya hayo yote ndio kupaishwa JUU mbinguni(rejea imani ya kikristo)
Hapa ndio inakuja ile tafsiri ya maneno KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.....
Kwahiyo wafu huwa around mpaka wanapozikwa ndio huenda kuzimu... Wale tunaowaona wakirejea duniani kwa vague images, ndoto hisia nk sio wafu tena bali ni mizimu.... Na kwa taarifa yako ni kwamba wafu wote wako kaburini /kuzimu wakisubiri ufufuo siku ya kiama... Hakuna mfu aliye peponi na hakuna mfu anayekwenda kuzimu direct bila kupitia mchakato husika... Hata kama alipotelea baharini, hata kama alioza porini ama aliungua mpaka kubakia jivu... Roho ndio hubeba mchakato wote na kamwe roho haifi...