Ni wakati gani wafu hufika kuzimu?

Sala dua na maombezi pale na kaburi vina mambo mawili makuu ambayo wengi hawayajui na kinyume chake wanadhani ni kwa ajili ya kuwaombea MSAMAHA waweze kulala mahali pema peponi...
Iko hivi
Kiimani hakuna MSAMAHA baada ya kifo.. Kinachofanywa na watumishi ni kumsaidia tu marehemu roho yake isitangetange na kugeuka mzimu au pepo... Ndio maana tukisikia mtu kafa tunasema APUMZIKE KWA AMANI /REST IN PEACE....

Jambo la pili zile sala dua na maombezi ni kwa ajili ya faraja za kibinadamu kwa wafiwa na mpendwa wao....
Ni kweli mkuu, ila ukiniambia ni njia ya kujifariji hapo nakuelewa zaidi. Ila hapo kwa kipengele cha kwanza sijui sababu sielewi km kuna roho kutangatanga na kugeuka mzimu. Siwezi kubisha nisichokijua labda nipewe elimu ya kina
 
Unajua asili ya mizimu ninini? Ni roho za marehemu zinazorejea duniani bila umbo la mwili.... H huweza kurudi kwa heri ama kwa shari....
Kitu kinachoitwa MIZIMU YA MABABU ushawahi kukisikia!? Kinawatesa sana watani zangu Wachaga... Lazima kila mwaka wailishe kwa damu na pombe... Ili wafanikiwe mambo yao
 
kwa uelewa wangu, kinachokufa ni nafsi na roho na si mwili, mana huu mwili ni ganda tu, ni sawa na roboti ukilichomeka kwenye umeme au ukiliweka betri linafanya kazi lakini ukizima umeme au ukachomoa betri haliwezi kufanya kitu. Sasa basi kama kinachokufa ni nafsi na roho iweje tena hivyo hivyo vinavyokufa viweze kurudi kutangatanga? sio kwamba vinakuwa mfu vinasubiri hukumu?
 
roho yake ilirudi tena kwa njia ya yohana mbatizaji rejea injili ya mathayo 11;11-14

Point yangu ilikuwa kuelezea kwamba sio wote walioenda Mbinguni walikufa wapo walionyakuliwa wakawa hai bila kupitia kifo, hiyo ya kurudi tena kama mtu mwingine ni point nyingine kabisa
 
kwa uelewa wangu, kinachokufa ni nafsi na roho na si mwili, mana huu mwili ni ganda tu, ni sawa na roboti ukilichomeka kwenye umeme au ukiliweka betri linafanya kazi lakini ukizima umeme au ukachomoa betri haliwezi kufanya kitu. Sasa basi kama kinachokufa ni nafsi na roho iweje tena hivyo hivyo vinavyokufa viweze kurudi kutangatanga? sio kwamba vinakuwa mfu vinasubiri hukumu?
Nafsi ni muunganiko wa roho na mwili, nje ya hivyo viwili hakuna nafsi tena bali vinasaba vyake... Roho nayo haifi na haiwezi kuungana tena na mwili wa nyama bali hugeuka kuwa mzimu
 
Hata wewe Mshana unajua kuna siku utakuwa maiti na kulazwa humo mochwari
 
Nafsi ni muunganiko wa roho na mwili, nje ya hivyo viwili hakuna nafsi tena bali vinasaba vyake... Roho nayo haifi na haiwezi kuungana tena na mwili wa nyama bali hugeuka kuwa mzimu
kwahiyo unachosema ni kwamba kinachokufa ni mwili? alafu baada ya hapo roho inahama inabakia kuwa mzimu? au roho inakufa alafu inageuka mzimu?
 
kwahiyo unachosema ni kwamba kinachokufa ni mwili? alafu baada ya hapo roho inahama inabakia kuwa mzimu? au roho inakufa alafu inageuka mzimu?
Ndio kinachokufa ni mwili, roho si lazima igeuke mzimu.. Nimefafanua kwenye post hebu rudia kusoma tena
 
Wakati wa mafunzo yangu huko mbali na baadae kazini nilipata mara si haba wasaa wa kukaa na wagonjwa waliokuwa katika dakika zao za mwisho za kufariki... Wachache nilikuwa nao mpaka roho inaachana na mwili.... Maisha yana vitu vinauma na kuumiza sana... Lakini hakuna maumivu makali kama pale roho inapotaka kujitenga na mwili... Ni tendo moja gumu sana.. Na unayaona wazi mahangaiko ya mfu mtarajiwa....
Nimeshiriki pia mara si haba kuwapokea wafu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti(mortuary) na kuwahifadhi wengine hadi wiki na ushee...Nimeshiriki kuwaandaa marehemu kwa ajili ya kuagwa mara ya mwisho na wapendwa wao... Nimeshiriki kuzika kwa udongo.. Na nimeshiriki si mara haba kuwachoma moto marehemu kama utamaduni wao unavyotaka
Kote huko niligundua kitu kimoja kikubwa sana... Kifo sio jambo la maramoja linaloishia hapo hapo... Kifo ni mchakato unaoanzia tangu kutungwa kwa mimba, kuzaliwa, kufa na mwendelezo baada ya kufa..
Mfu anakuwa mfu kwasababu tu roho imetengana na mwili.. Lakini kuna uhai usioonekana unabaki mpaka pale makaburini! Na ndio maana kuna simulizi nyingi za marehemu kabla hawajazikwa na hata baada ya kuzikwa...
Baadhi ya vituko hivyo ni
. maiti kununa ama kutabasamu
. maiti kukunja uso
.maiti kugeuka kidogo
. maiti kukataa kusafirishwa
. maiti kukataa kuvalishwa nguo
. maiti kushindikana kabisa kubebwa nknk

Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye imani zetu kuhusiana na swala zima la pepo na kuzimu(akhera) na uhalisia wa mfu kufika kuzimu ama peponi muda gani...
Mchakato wa mtiririko wa kikristo uko hivi
Mateso
Kifo
Kuzikwa
Kushuka kuzimu (kwa tafsiri ya hapa kuzimu kuko chini ya kaburi)
Baada ya hayo yote ndio kupaishwa JUU mbinguni(rejea imani ya kikristo)
Hapa ndio inakuja ile tafsiri ya maneno KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.....

Kwahiyo wafu huwa around mpaka wanapozikwa ndio huenda kuzimu... Wale tunaowaona wakirejea duniani kwa vague images, ndoto hisia nk sio wafu tena bali ni mizimu.... Na kwa taarifa yako ni kwamba wafu wote wako kaburini /kuzimu wakisubiri ufufuo siku ya kiama... Hakuna mfu aliye peponi na hakuna mfu anayekwenda kuzimu direct bila kupitia mchakato husika... Hata kama alipotelea baharini, hata kama alioza porini ama aliungua mpaka kubakia jivu... Roho ndio hubeba mchakato wote na kamwe roho haifi...
Upendo wa mungu ni wa ajabu sana aloo, ila ndo hivyo hakuna jinsi

Sisi tunawapenda wanetu ila hatuwatishi tishi hivi, mi babangu wa hapa duniani alinisomesha na kunipa kila alichoweza ila hakukuwa na hii taabu kama hivi sijui ntakusomesha ila unisalimie kila saa n.k, huyu Baba wa mbinguni ni balaa
Ntakusweka kwenye moto
Ntakuteketeza na moto wa kiberiti n.k masharti balaa na Ana matabaka ya kutosha masikini, vipofu, viwete, n.k

Mtu anaua mchungaji na anadunda mtaani
Mtu anatesa wenzie na anadunda mtaani
Mtawala inayesemeka kawekwa na mungu anatesa watu na anadunda tu daadeki.

Any way bandiko lako ni zuri mkuu.
Ngoja tuishi hiyo miaka aliyotupangia tukateketezwe na moto wa milele naana
 
Point yangu ilikuwa kuelezea kwamba sio wote walioenda Mbinguni walikufa wapo walionyakuliwa wakawa hai bila kupitia kifo, hiyo ya kurudi tena kama mtu mwingine ni point nyingine kabisa
ok tupo pamoja
 
Ndio kinachokufa ni mwili, roho si lazima igeuke mzimu.. Nimefafanua kwenye post hebu rudia kusoma tena
hapo ntakupiga bwana, roho ndo huacha mwili baada kufa huu mwili ni ganda tu linalosapotiwa na roho ambayo ni pumzi
 
hapo ntakupiga bwana, roho ndo huacha mwili baada kufa huu mwili ni ganda tu linalosapotiwa na roho ambayo ni pumzi
Sijakuelewa mbona kama unazungumzia kitu kile kile ninachomaanisha mimi... Sasa iweje unipige/unipinge?
 
Sijakuelewa mbona kama unazungumzia kitu kile kile ninachomaanisha mimi... Sasa iweje unipige/unipinge?
Nimekupinga kwasababu umesema MWILI NDIO HUWA UNAKUFA na SIO ROHO, kwahiyo kwa nilivyokuelewa ni unasema kwamba mwili huwa unakufa unaacha roho ambayo inabaki inatangatanga au ina pumzika. Ila nijuavyo mimi roho ndo huwa inakufa huu mwili unasapotiwa na roho hivyo ikifa ndo mwili umekufa
 
Roho ni energy haifi... Roho ni pumzi ya uhai haifi.. Roho ni pumzi ya uhai haikuumbwa...
 
Nimekupinga kwasababu umesema MWILI NDIO HUWA UNAKUFA na SIO ROHO, kwahiyo kwa nilivyokuelewa ni unasema kwamba mwili huwa unakufa unaacha roho ambayo inabaki inatangatanga au ina pumzika. Ila nijuavyo mimi roho ndo huwa inakufa huu mwili unasapotiwa na roho hivyo ikifa ndo mwili umekufa
Mwili ni mwenyeji wa roho hapa duniani mwili ukigoma roho lazima iondoke iende ilipojichagulia wakati ikiishi na mwili...haiwezi kubaki tena hapa duniani kwasababu mwenyeji wake hayupo.
Japokuwa kuna kifo cha roho pia kulingana na maisha iliyokuwa ikiishi ilipokuwa na mwili baada ya mwili kufa roho itasubiri hukumu siku ya kiama kama iliishi vyema basi itaenda pema na kama iliishi vibaya itaenda pabaya (jehanam)
 
Thanks, nimeelewa sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom