Kuna jambo limenitokea ambalo ningeomba uafafanuzi wa wajuzi. Kuna rafiki yangu alifariki kwenye ajali iliyohusisha gari tatu lakini alikufa pekee yake. Tukiwa msibani, zikaanza minong'ono kuwa ajali ile imetengenezwa na jamaa waliokuwa naye ofisini. Kulikuwa na issue fulani ya mamilioni ambayo ilikuwa inapigwa kiaina. Yeye alikataa kushiriki ile issue ikafikia suala lile limeanza kuchunguzwa na neno lake lingeweza kuhatarisha dili nzima. Baada ya mazishi kama miezi 6 hivi, ikanitokea nikitaka kulala usiku nahisi uwepo na mshikaji na kama anataka kuniambia kitu. Bahati mbaya nikawa sielewi vizuri kinachoendelea. Baada ya hali hiyo kunitokea kama siku 3 mfululizo, siku ya nne nikiwa ofisini nikapigiwa simu na moja ya lile kundi (watuhumiwa) kuniambia kuwa lile suala limeletwa ofisini kwetu hivyo anaomba nilifuatilie limalizike na jamaa akaahidi kunitoa pakubwa issue ikikamilika. Kimsingi nilijawa na hofu na nikajiuliza au ndo hisia nilizokuwa nazo kuwa jamaa marehemu anataka kuniambia kitu.
Kimsingi niliwaambia ninakwenda masomoni hivyo sitakuwa na nafasi ya kushughulikia (nilidanganya) lakini nafsi yangu imekataa kushiriki hiyo kazi
Hii ni nini?