Ni wakati gani wafu hufika kuzimu?

Ni wakati gani wafu hufika kuzimu?

Kabla hajalala huo usingizi ulishawahi kumuona anavyokuwa
 
We jamaa ni muongo muongo sana alafu unajifanya mjuaji wakati we ni binadam kama bibadam kwingine inshort maisha ni fumbo, huko kuzimu hujawahi kufika wala mbinguni hupajui acha porojo zako
 
Wakati wa mafunzo yangu huko mbali na baadae kazini nilipata mara si haba wasaa wa kukaa na wagonjwa waliokuwa katika dakika zao za mwisho za kufariki... Wachache nilikuwa nao mpaka roho inaachana na mwili.... Maisha yana vitu vinauma na kuumiza sana... Lakini hakuna maumivu makali kama pale roho inapotaka kujitenga na mwili... Ni tendo moja gumu sana.. Na unayaona wazi mahangaiko ya mfu mtarajiwa....
Nimeshiriki pia mara si haba kuwapokea wafu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti(mortuary) na kuwahifadhi wengine hadi wiki na ushee...Nimeshiriki kuwaandaa marehemu kwa ajili ya kuagwa mara ya mwisho na wapendwa wao... Nimeshiriki kuzika kwa udongo.. Na nimeshiriki si mara haba kuwachoma moto marehemu kama utamaduni wao unavyotaka
Kote huko niligundua kitu kimoja kikubwa sana... Kifo sio jambo la maramoja linaloishia hapo hapo... Kifo ni mchakato unaoanzia tangu kutungwa kwa mimba, kuzaliwa, kufa na mwendelezo baada ya kufa..
Mfu anakuwa mfu kwasababu tu roho imetengana na mwili.. Lakini kuna uhai usioonekana unabaki mpaka pale makaburini! Na ndio maana kuna simulizi nyingi za marehemu kabla hawajazikwa na hata baada ya kuzikwa...
Baadhi ya vituko hivyo ni
. maiti kununa ama kutabasamu
. maiti kukunja uso
.maiti kugeuka kidogo
. maiti kukataa kusafirishwa
. maiti kukataa kuvalishwa nguo
. maiti kushindikana kabisa kubebwa nknk

Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye imani zetu kuhusiana na swala zima la pepo na kuzimu(akhera) na uhalisia wa mfu kufika kuzimu ama peponi muda gani...
Mchakato wa mtiririko wa kikristo uko hivi
Mateso
Kifo
Kuzikwa
Kushuka kuzimu (kwa tafsiri ya hapa kuzimu kuko chini ya kaburi)
Baada ya hayo yote ndio kupaishwa JUU mbinguni(rejea imani ya kikristo)
Hapa ndio inakuja ile tafsiri ya maneno KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.....

Kwahiyo wafu huwa around mpaka wanapozikwa ndio huenda kuzimu... Wale tunaowaona wakirejea duniani kwa vague images, ndoto hisia nk sio wafu tena bali ni mizimu.... Na kwa taarifa yako ni kwamba wafu wote wako kaburini /kuzimu wakisubiri ufufuo siku ya kiama... Hakuna mfu aliye peponi na hakuna mfu anayekwenda kuzimu direct bila kupitia mchakato husika... Hata kama alipotelea baharini, hata kama alioza porini ama aliungua mpaka kubakia jivu... Roho ndio hubeba mchakato wote na kamwe roho haifi...
Nimerudi, niko available.....
 
Kifo kifo kinaogopesha jamani woiiii
Kaka asante endelea kututisha kaka angu
 
wale wanaokufa wamelala kwao mateso yanapungua kidogo?
 
wale wanaokufa wamelala kwao mateso yanapungua kidogo?
Kimwili hawana fahamu tena lakini kiroho mambo ni tofauti.... Roho ikitulia kaburini ndio ile hali tunayoita REST IN PEACE... Lakini roho ikigeuka pepo shida huanzia hapo... Inakuwa ni roho ya kutangatanga na mahangaiko mengi na Hii ndio dhana ya jehanum
 
Kimwili hawana fahamu tena lakini kiroho mambo ni tofauti.... Roho ikitulia kaburini ndio ile hali tunayoita REST IN PEACE... Lakini roho ikigeuka pepo shida huanzia hapo... Inakuwa ni roho ya kutangatanga na mahangaiko mengi na Hii ndio dhana ya jehanum
Nimekupata mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom