Manifestation
Senior Member
- Jan 22, 2020
- 193
- 315
Kwanza ugonjwa wa akili ni kitendo cha kuanzia kufanya matukio kinyume na utaratibu na Kwa kujiamini sana bila wewe kujijua unakosea Ila jamii inakuona wewe unakosea, unaweza ukawa unasikia sauti za watu wanakuita Ila huwaoni, unaweza ukawa unajibizana na sauti ambazo huzioni, unaweza ukawa mhubiri WA uongo ukawa unatamka maneno ya kwenye biblia na Qur'an amabayo hayaendani na ukweli.
Changamoto kubwa kwetu Tanzania ukiugua ugonjwa WA akili watu wanaanza kusema umelogwa na kubatiza majina kama saa mbovu/ dish limeyumba/ kichwa/ hajielewi nk Ila ukweli wa dhati huu hi ugonjwa kama magonjwa mengine na unatibika kama unavyoona malaria; kaswende na mengine mengi yanayotibika kutegemea umekuathiri kiasi na sababu zilizofanya upate na kama unaendelea kujihatarisha Kwa kuendelea na visababishi kama pombe/ sigara/ bangi/ msongo/ kujitenga na jamii.
Kwa uzoefu wangu baada ya kuugua ugonjwa huu na kupona unaweza ukawa unatukana serikali au kusifia; unaweza ukawa unahubiri injili ya kweli au ya uongo, unaweza ukawa unaongea Mambo ambayo hayapo kabisa, unaweza ukachoma vyeti vyako vyote, unaweza haribu vitu vya nyumbani, unaweza ukachoma Qur'an, biblia, unaweza ukavua nguo zako zote barabarani; unaweza ukawapiga watu, unaweza ukawa na overdriving kila mahali unapita kama upo na gari, unaweza unapita katikati ya barabara na unakimbia kuface mahari.
wagonjwa wa akili Wana Mungu sana na huwa mara nyingi wengi wanakuwa na wito na hawatembei katika wito ndio maana wanapata misukosuko ili waweze kujijua wao ni WA kina Nani na wanatakiwa wafanye nini.
Sababu ya kuandika ujumbe huu ni baada ya kuona Jana mtumishi WA serikali amefukuzwa kazi Kwa sababu ya kuchana Qur'an, Ila ukimuangalia kwa makini yule jamaa aliyechana Qur'an hayupo Sawa na akienda polisi huko anaweza akaambulia kipigo na mateso na ukakuona jamaa yupo Sawa Ila kama ukimuangalia kwa makini na kumtuatilia sana utakuja gundua Yule ni mgonjwa.
Mfano wa watu wengine ambao Nina hakika nao ni wagonjwa WA akili ni Dr shika & mchungaji/nabii Tito hawa ni wagonjwa wanaotembea barabarani ni wa kuwaangalia sana sio WA kutengwa wala kunyanyapaliwa na vizuri jamii ikawaweka karibu ili waweze kutengamaa Huku wanatibiwa katika hospital za karibu Yao,.
Nilitibiwa muhimbili nikapona Kwa dawa ziitwazo olanzapine n haloperidol kama utakuwa na maswali kuhusiana na ugonjwa huu Kwa uzoefu ninaweza kushare ili kuweza kupanua uelewa.