Dar: Watu 7 wapofuka Macho kwa kujitibu Ugonjwa wa 'Red Eyes' kienyeji

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1708343176823.png

Screenshot_20240219_042727_WhatsApp.jpg
Wizara ya Afya imesema idadi ya watu waliopata upofu jijini Dar es Salaam kutokana na kutibu ugonjwa wa macho mekundu kwa njia za kienyeji wamefikia saba kutoka wanne.

Februaru 8, Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Profesa Paschal Ruggajo alisema watu wanne waliougua ugonjwa huo wamepata upofu kwa kujitibu kienyeji.

Ugonjwa huo wa maambukizi kwenye ngozi ya juu ya gololi la jicho unaoitwa Conjunctivitis, maarufu Red eyes umeshasambaa katika mikoa yote nchini.

Februari 7, mwaka huu, mratibu wa huduma za afya msingi na matibabu ya macho Zanzibar, Dk Rajab Muhammed Hilali alitoa takwimu za watu saba kupata upofu baada ya matumizi ya dawa za kienyeji kutibu ugonjwa huo.

Idadi hiyo inafanya jumla ya wagonjwa waliopata madhara hasi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kufikia 14.

===========

Dar es Salaam. Wizara ya Afya imesema watu saba jijini Dar es Salaam wamepata upofu kutokana na kutibu ugonjwa wa macho mekundu kwa njia za kienyeji, huku wawili kati yao vioo vya jicho vikitoboka.

Ugonjwa huo wa maambukizi kwenye ngozi ya juu ya gololi la jicho unaoitwa Conjunctivitis, maarufu Red eyes umesambaa mikoa 26 nchini.

Februari 7, 2024, mratibu wa huduma za afya msingi na matibabu ya macho Zanzibar, Dk Rajab Muhammed Hilali alitoa takwimu za watu saba kupata upofu baada ya matumizi ya dawa za kienyeji kutibu ugonjwa huo.

Idadi hiyo inafanya jumla ya wagonjwa waliopata madhara hasi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kufikia 14.

Ugonjwa huo ulioripotiwa kwa mara ya kwanza Januari 13, 2024 athari zake hasi ni vidonda kwenye kioo cha jicho vinavyoweza kusababisha kovu kwenye jicho litakalomfanya mgonjwa apate uoni hafifu au kupoteze uwezo wa kuona kabisa.

Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Jumapili Februari 18, 2024, Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Profesa Paschal Ruggajo amesema hadi Februari 15, watu saba walitolewa taarifa ya kupata madhara kwenye vioo vya jicho.

“Watano wamepata vidonda kwenye kioo cha jicho na wawili walikutwa vioo vya jicho vimetoboka. Wagonjwa wote walionwa kwenye vituo vya tiba vilivyopo Dar es Salaam na umri wao ni kati ya miaka 21 hadi 42.

“Baadhi ya vitu vilivyotumika na waathirika hao ni pamoja na maji ya chumvi, tangawizi, maji ya majani ya mbaazi, vitunguu swaumu, chai ya rangi, vicks na dawa zenye viambata vya steroids,” amesema Ruggajo.

Profesa Ruggajo amesema wizara imeendelea kufuatilia mwenendo wa maambukizi na kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema hadi Februari 15 2024, jumla ya wagonjwa 14,641 wametolewa taarifa, walioonwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kwenye mikoa 26.

Dar es Salaam inaongoza kwa idadi ya wagonjwa 6,940, Pwani (4,480), Morogoro (630) na Dodoma (550).

Profesa Ruggajo amesema wizara inaendelea na hatua mbalimbali za kinga na udhibiti wa ugonjwa huo, ikiwamo utoaji wa elimu kwa kutumia wataalamu wa afya kupitia vyombo vya habari.

“Elimu inatolewa maeneo yenye mikusanyiko hususani shule, magereza na vyuo, nyumba za ibada, usambazaji wa vipeperushi na utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa kupitia vituo vyetu vya tiba na mitandao ya kijamii,” amesema.

Amesema wizara pia inaendelea kuratibu na kusimamia huduma mkoba za macho kwenye maeneo mbalimbali nchini na kubaini wagonjwa wenye shida ya macho mekundu na kuwapatia elimu.

“Hadi sasa vipindi vya kwenye runinga zaidi ya 20 vimetolewa na wataalamu wetu wa afya, redio za kijamii zaidi ya 25 kwenye mikoa mbalimbali, ikiwemo ambayo haina wagonjwa,” amesema.

Amesema wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zaidi ya 25,000 wamefikiwa kwenye shule zao pamoja na walimu wao.

Profesa Ruggajo amesema wanaendelea kutoa elimu kuhusu madhara ya kutofuata kanuni zilizotolewa, baada ya kupata taarifa ya wagonjwa kutumia tiba zisizo rasmi na kupata madhara.

Kutokana na hilo, amesema wizara iliandaa video na kuirusha kwenye vyombo mbalimbali vya kuelimisha.

Akizungumza na Mwananchi Februari 8, 2024, Meneja Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho, Wizara ya Afya, Dk Bernadetha Shilio alisema baadhi ya wagonjwa wanaopokewa kioo cha jicho kinabainika kumeharibika.

Amesema wagonjwa wa aina hiyo wanapotibiwa bado kunakuwa na kovu lenye rangi nyeupe kama karatasi ambalo likibaki hivyo moja kwa moja hupata ulemavu wa kutoona.

Matibabu sahihi

Wizara inaelekeza hatua za kuchukua kwa kuosha uso kwa maji safi na sabuni mara kwa mara.

Tumia dawa ya paracetamol kumeza kwa ajili ya kupunguza maumivu

Nenda kituo cha tiba kwa ajili ya uchunguzi, kama hupati nafuu.

Hakikisha mikono na uso inakuwa safi muda wote.

Jizuie kugusa macho yako kadri uwezavyo.

Tumia vipukusi (vitakasa mikono) mara kwa mara.

Epuka kushikana mikono au kugusa vitu vinavyoguswa na wengi.

Tumia taulo au leso za karatasi kufuta tongotongo au machozi.

Nenda kituo cha kutolea huduma mara upatapo dalili.

Kumbuka kufua mashuka na mataulo kila siku.

MWANANCHI
---
UPDATE: WIZARA YA AFYA YAKANUSHA TAARIFA HII

- Wizara ya Afya yakanusha taarifa ya watu saba kupata upofu kutokana na ugonjwa wa red eyes
 
Hivi zile dawa tulizokuwa tunawekwa utoto za matone siku hizi hakuna?
Zipo na zinasaidia ukiweza kuapply mapema kabla ya tatizo halijakaa sana , na kuna namna yake ya kufanya kwa mtu aliyepata maambukizi ya red eyes, kwa mfano inashauriwa kama umegundua dalili la kuathiriwa na red eyes kwenye moja ya jicho lako basi ni vema kuanza kuweka (ma) tone kwenye lile ambalo bado halijaanza kuathiriwa ili kuepusha maambukizi, ila si unajua watanzania na akili zetu watu wanaokoteza maneno ya vijiweni ndio maana umesikia wengine wamenawa maji ya chumvi na limao, wengine wamepaka asali, utashindwa kupofuka kweli?haya ni sawa na yale ya Covid 19, kila mtu aligeuka daktari akaja na mbinu yake, ili mradi taflani.
 
Wizara ya Afya imesema idadi ya watu waliopata upofu jijini Dar es Salaam kutokana na kutibu ugonjwa wa macho mekundu kwa njia za kienyeji wamefikia saba kutoka wanne.

Februaru 8, Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Profesa Paschal Ruggajo alisema watu wanne waliougua ugonjwa huo wamepata upofu kwa kujitibu kienyeji.

Ugonjwa huo wa maambukizi kwenye ngozi ya juu ya gololi la jicho unaoitwa Conjunctivitis, maarufu Red eyes umeshasambaa katika mikoa yote nchini.

Februari 7, mwaka huu, mratibu wa huduma za afya msingi na matibabu ya macho Zanzibar, Dk Rajab Muhammed Hilali alitoa takwimu za watu saba kupata upofu baada ya matumizi ya dawa za kienyeji kutibu ugonjwa huo.

Idadi hiyo inafanya jumla ya wagonjwa waliopata madhara hasi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kufikia 14.
Ingependeza kama wizara ingea ainisha njia zisizosahihi ambazo zinatumiwa na watu, kwasabab nikawaida yetu kutafuta matibab kwa njia zetu wenyew kabla yakwenda hospital, ikiwa wizara haitoainisha basi watu watazidi kudhurika
 
Idadi hiyo inafanya jumla ya wagonjwa waliopata madhara hasi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kufikia 14.
Inasikitisha sana hii, ghafla tu mtu anaanza kusoma kwa vidole, kweli hakun ajuaye kesho yake
 
Hivi zile dawa tulizokuwa tunawekwa utoto za matone siku hizi hakuna?
Huu ugonjwa hauna dawa
Dawa ni kusafisha macho
Na usijifikichefikiche macho
Siku 2,3 itaondoka yenyewe
Sasa kuna wenginenasikia walikuwa wanaweka mpaka mafuta ya taa machoni ,ugonjwa ukiibukaga huku uraiani wanatokea wataalam kibao
Utasikia weka majani ya chai mwingine anasema nawa na mkojo usoni basi mambo tafrani

Ova
 
Back
Top Bottom