Ni vitu vipi vinaiangusha Tasnia ya Bongo Movie? Changia Mawazo

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari wana JF,

Nimejiuliza sana hivi kwanini Movies zetu za kibongo na series zetu hazipendwi kama hao Waturuki, wakorea, wafilipino, wahindi etc?

Kwangu mimi nimepitia tamthiliya na muvi mbali mbali za kibongo na kugundua kasoro zifuatazo:

1. Zinakosa uhalisia ,uhalisia wa kimatukio, wahusika na kiutaalamu.

2. Wanakosea Muendelezo wa matukio, Mtu kavaa hivi akitokea sehemu nyingine unaona kuna tofauti.

3. Teknolojia duni
Ni vitu gani vingine Bongo movies wanakwama tuwasaidie?
 
Mi nadhani kabla hatujawalinganisha bongo movie na wakorea,waphilipn,wahindi tuangalie sisi kama tanzania tunalingana na nchii izoo kwenye tasnia ipiii footbal vitasa uchumi tecnologia hawakufika hapo siku moja wameanza lini kuproduce izoo movie zao bongo tumeanza lini turidhike na level yetu huku tukisupportiana kesho tuwebora zaidi
Walitangulia lakini bongo movie wanaweza badilika pia
 
Kusema la haki turudi kule kwa Musa banzi uchawi ndo tunajua movie ziliuza sana mpak vibanda umiza ila now kingereza cha ugoko kingi hamna maana mapenzi huwezi angalia na wazazi mara ya kwisho kuangalia bongi movie ni ile ya kanumba uncle jj inaanza yuko kweny mkutano anaongea then anafukuzwa tangu hapo sijaangalia ile seriously Tena movie

Naangalia YouTube ila movie Kama girl friend ya zamani Maisha na muziki ila haina sauti kule
 
Hahahaa changia mawazo wasonge mbele
Mkuu hao hawaehauriki. Kabisa. Unadhani hawaoni hizi nyuzi, wanaona ila wanajiamini wao ndio kila kitu.

  • Movie zao ata ule uhalisia kidogo tu hazina.
  • Kila mlinzi/mfungua geti ni tahira.
  • Kila mchekeshaji lazima apige kelele na avae kama kichaa.
  • Wanaume kuigiza scene za mwanamke.
  • Hao wakina mkojani sijui ata uwa mnawaelewaje.
  • Movies hazina ata ile scripts sijui inaitwa. Naona kama msanii anatafuta maneno pale pale kwenye camera.
  • Movie moja hafu visa kama mia mbili hivi. Movie inaanza mtu na mke wake wana ugomvi, utakuta katikati jamaa amerogwa kazini, kisha boss wake amefumaniwa na mwanafunzi, then mkuu wa shule wa uyo mwanafunzi ameibiwa baiskeli, then mama wa mwizi wa baiskeli bishara yake ya vitumbua inaenda vizuri, yaani unapotea.
Tukianza warekebisha hao tutaonekana tunawaonea wivu. Waache waendelee kunyonywa na Sinema Zetu, DSTV na Channel zingine.

Me nasahivi saburia Thor: Love & Thunder. We endelea msubiria Mkojani aendelee kusema “Nyamazaaa weweeee”
 
Technology, budget na kujuana sana (connection)
Bongo ukiwa maarufu tu unalamba deal la uigizaji bila kujali una kipaji au kinyume chake.

Vile vile wenzetu wako serious na kazi zao, wana crew nzito na ya kutosha kila mtu na kazi/fani yake aliyosomea wakati kibongo bongo, Director ndie muandika story, Dereva, mshika taa, sijui make up n.k.

Hata time taken kwenye Movie zenyewe ni tatizo, wenzetu kuandaa Movie moja for 2/3 years ni kitu cha kawaida sana, bongo movie inaandaliwa ikizidi sana mwezi then inaingia sokoni, uhalisia utatoka wapi?

Mambo ni mengi aisee, siwezi kuandika yote.
 
Mkuu hao hawaehauriki. Kabisa. Unadhani hawaoni hizi nyuzi, wanaona ila wanajiamini wao ndio kila kitu.

  • Movie zao ata ule uharisia kidogo tu hazina.
  • Kila mlinzi/mfungua geti ni tahira.
  • Kila mchekeshaji lazima apige kelele na avae kama kichaa.
  • Wanaume kuigiza scene za mwanamke.
  • Hao wakina mkojani sijui ata uwa mnawaelewaje.
  • Movies hazina ata ile scripts sijui inaitwa. Naona kama msanii anatafuta maneno pale pale kwenye camera.
  • Movie moja hafu visa kama mia mbili hivi. Movie inaanza mtu na mke wake wana ugomvi, utakuta katikati jamaa amerogwa kazini, kisha boss wake amefumaniwa na mwanafunzi, then mkuu wa shule wa uyo mwanafunzi ameibiwa baiskeli, then mama wa mwizi wa baiskeli bishara yake ya vitumbua inaenda vizuri, yaani unapotea.
Tukianza warekebisha hao tutaonekana tunawaonea wivu. Waache waendelee kunyonywa na Sinema Zetu, DSTV na Channel zingine.

Me nasahivi saburia Thor: Love & Thunder. We endelea msubiria Mkojani aendelee kusema “Nyamazaaa weweeee”
Wata uchukua ushauri huu mkuu
 
Kusema la haki turudi kule kwa Musa banzi uchawi ndo tunajua movie ziliuza sana mpak vibanda umiza ila now kingereza cha ugoko kingi hamna maana mapenzi huwezi angalia na wazazi mara ya kwisho kuangalia bongi movie ni ile ya kanumba uncle jj inaanza yuko kweny mkutano anaongea then anafukuzwa tangu hapo sijaangalia ile seriously Tena movie

Naangalia YouTube ila movie Kama girl friend ya zamani Maisha na muziki ila haina sauti kule
😂😂😂
 
1. Wakivaa yale ma Make up yao wanatisha jamani, sijui ni nani anawakandika vile

2. Wanawake wakubwa mno yaani mitipwatipwa haipendezi kucheza scenes za harakati zaidi ya mambo ya familia, hawajui vile Models hupendezesha screen.

3. Ubunifu wa Story zero na hii inatokana na Waandishi kua na Low IQ, hawawazi mambo makubwa zaidi ya yale yale tuliyoyazoea miaka nenda rudi,

4. Vifaa Duni, kuanzia Cameras, Technologia hadi Bajeti

5. Vipaji hakuna, wanachukuana wale wale kwa kujuana, kuna Wasomi wa Chuo cha Sanaa wanabaniwa kila sekta wanapitishwa wauza Sura

My Take;
Apatikane mdau/wadau mzuri awekeze kwenye hicho kiwanda, awekeze kwa Wasomi waliobobea kwenye kila taaluma ya Filamu, Sanaa yetu ikifika mbali hata hao Watalii watakuja wenyewe, kwanza tuna maeneo mengi sana na mazuri ya kufanyia shootings.
 
Nchi yetu ina historia za Watu waliofanyia makubwa Taifa hili, kutwa tunaangalia movies za wenzetu wakiwaenzi mababu na mabibi zao kupitia Movies ili Historia inabakie na hata iwe rahisi kwa Watoto kujifunza Shuleni,

Kiwanda chetu cha Filamu kimeshindwa kufanya hayo, tunaletewa huyu kamfumania yule, yule Mtoto wake alikua huyu ila hakujua, sijui Mama wa Kambo nini yaani ujinga ujinga tu.
 
Tasnia hailipi najua wengi watabisha lingine tatizo bajeti DSTv, azam na Startime wamalipa china ya Million moja kwa Movie moja.
 
Wengi wao hawana ufahamu juu ya mambo mbalimbali ya dunia(issues), pia wengi hawasoni vitabu na machapisho ya waandishi nguli, elimu ndogo hapa ni mchanganyiko wa elimu ya darasani na Ile ya kutembea maeneo tofauti ndani na nje ya nchi... Visa vyao ni mapenzi tu.

Hawafuatlii ishu nyeti kama za rushwa, wizi wa kimtandao, ukwepaji wa Kodi, uharibifu wa mazingira, wizi wa magari, usafirishaji na biashara ya binadamu, matatizo ya ajira...

Mwisho waigizaji wengi wa bongo movu Sio waigizaji, labda Kuna biashara wanazifanya kupitia mwavuli wa kuigiza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom