Ni vikwazo gani Tanzania na baadhi ya nchi nyingine za Afrika zitawekewa baada kukataa chanjo ya Covid -19?

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Shirika la Afya duniani (WHO) limetangaza mpango wa muda kuhusu jinsi nchi zitakavyopewa chanjo za corona mwaka huu, huku Tanzania na Burundi zikiwa hazimo.

WHO limasema kuwa chanjo hizo ambazo ni dozi milioni 336 za AstraZeneca/Oxford na Pfizer-BioNTech, zitatolewa kwa muhula wa kwanza na wa pili ya mwaka 2021.

Kwa mujibu was WHO katika awamu hii, nchi zitapewa kwa sawa na 3.3% ya watu katika kila nchi katika mpango huu, kulingana na malengo ya shirikisho chanjo duniani GAVI ya utoaji wa chanjo kwa 3% ya wakazi wa dunia katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2021.

Katika orodha ya awali kuhusu mpangilio wa nchi zitakazopata chanjo katika eneo la Afrika Mshariki Tanzania na Burundi hazimo.

Nchi nyingine za Afrika ambazo hazimo katika orodha ya upokeaji wa chanjo ni pamoja na, Equatorial Guinea, Eritrea, Gabon, Lesotho, Madagascar na Ushelisheli

Shirika hilo la afya duniani linasema kuwa nchi ambazo hazimo katika orodha yake ya kupewa chanjo ya corona kwasababu "zilijinunulia chanjo zake zenyewe, hazikuomba chanjo, au hazijawekwa bado katika orodha ya nchi zitakazopewa chanjo ".

d586e4e5-5bd4-40f9-a7be-d596ccd80dc3.jpg
 
Kwani kukataa chanjo ni uhalifu?!
Kumbuka tuliingia mkataba wa kimataifa uliosimamiwa na WHO mana yake kuna vipengere vya makubaliano ya chanjo mbalimbali za magonjwa kama tumekataa maana yake tumevunja mkataba unafikiri what next?
 
Kumbuka tuliingia mkataba wa kimataifa uliosimamiwa na WHO mana yake kuna vipengere vya makubaliano ya chanjo mbalimbali za magonjwa kama tumekataa maana yake tumevunja mkataba unafikiri what next?
Serikali yetu inawaza local na sio globaly, hivyo inadhani kwakuwa inaweza kukiuka sheria/mkataba wowote humu ndani ya nchi kwa utashi wa rais, inadhani hilo liko hivyo pia kwenye mikataba ya kimataifa.
 
Nchi za viongozi wenye akili wanaojali raia wao zimenunua chanjo, ikiwa ni pamoja na Madagascar, na zingine kuomba msaada toka WHO kuwalinda watu wao lakini nchi mbili tu za watu wajinga na masikini wa kutupwa kati ya nchi 54 za Afrika eti hawahitaji chanjo wanazo za babu zao za kufukiza za kutosha.

Aibu sana kuwa na viongozi aina hii karne ya Sayansi na Teknolojia!
 
Dawa yao ni kawanyima ARV tu maana wengi wao wanaishi kwa kutegemea hizo dawa.

Ingawa uamuzi huo utawaathiri na Wananchi wengine wasiyo na hatia.
 
Kwani kukataa chanjo ni uhalifu?!
Nchi zinaingia mikataba ya kimataifa linapotokea Jambo kama Hilo lazima nchi zote ziwe kitu kimoja kumbuka watu wanasafiri nchi mbali mbali itakuwaje kwenye hizo nchi wamepambana wameliondoa gonjwa nyie na ujinga wenu bado mnalo mkisafiri mnawaambukiza wenzenu vinginevyo mbaki kwenu.
 
Chanjo siyo lazima. Lakini kwa maoni yangu, watakaohitaji wapate.
 
Mnachoshindwa Kuelewa Ni Kuwa Tanzania Kuna Chanjo Nyingiii Tuu ambazo Tumekuwa Tukizitumia Toka Zamani, na Bado Tunaendelea Kuzitumia Hizo Chanjo. Na Hayo Makampuni Yaliyo Tajwa ndio Ambayo Wanatengeneza Hizo Chanjo pamoja na Dawa za Binadamu Nyibgi tuuuu, Hivyo kama Kweli Wana Nia Mbaya Na Sisi Tanzania Kama Inavyo daiwa na Baadhi Ya Watu basi Ili Tuwe Salama Ni Kufanya haya

1. Tukatae Chanjo Zote Zinazoingizwa Tanzania Kuanzia Chanjo Wanazopewa Watoto zetu wakizaliwa, Chanjo Za Hepatitis ect

2. Tukatae Dawa Zote za HIV kama ARV ambazo Zimethibitishwa pia na WHO na Zinatoka Hizo Nchi Ambazo Hao waliotengeneza Chanjo za COVID wanapo huko.

3. Tusi Import Dawa Yoyote ilee Toka nje ya Tanzania Na Tuanze Kutengeneza Dawa zetu Wenyewe.

4. Kwasababu Hawa Watu wana Nia Mbaya Na Tanzania, Tuache Kuagiza Vifaa vyovyote vile vya mahospitalini kwasababu wanaweza kutuwekea Vitu Vibaya Kwenye Hivyo Vifaa vya Mahospitalini Kuanzia Gloves, Syringes, Needles na Vifaa Vingine vyotee tuanze kutengeneza Vya Kwetu Ili Tuwe Salama kwasababu TUNASIKIA hawa Wazungu Hawatupendi Sisi kama Wanatupenda Wangetekeneza Vifaa vya Kuzuia watu Kufa

5. Tuache Kutumia Wataalamu wowote kutoka Nje ya Tanzania, Hata wataalamu Wetu wasiende Nje ya Nchi Kusoma Kitu chochote kuhusu Afya Ya Mtu Wanaweza Kufundishwa Vitu ambavyo Mwisho wa Siku wakija Hapaaa wanasabisha Watu wasizaee

Tusitishie Tishie Tuuu kwenye Chanjo Tufanye kwelii, Sisi Ni Nchi Tajiri Sanaa, Tunakila Kitu ndio Maana Hawa Watu weupe wanatuonea Wivuu

Tusitishie Tishie Tuuu....

Kama Tuna Ubavu Tufanye Hayo, sio Kwenye Chanjo Tuuu. Hatuna Hela Za Kununua Tunaanza Kuleta Sababu Za Kitoto kwamba chanjo sio Salamaa Sio salamaa wakati 99% ya Matibabu Tanzania Tunawategemea Wazungu.
 
Nchi za viongozi wenye akili wanaojali raia wao zimenunua chanjo, ikiwa ni pamoja na Madagascar, na zingine kuomba msaada toka WHO kuwalinda watu wao lakini nchi mbili tu za watu wajinga na masikini wa kutupwa kati ya nchi 54 za Afrika eti hawahitaji chanjo wanazo za babu zao za kufukiza za kutosha. Aibu sana kuwa na viongozi aina hii karne ya Sayansi na Teknolojia!
Duh

Mbona uko outdated...!
 
Nchi zinaingia mikataba ya kimataifa linapotokea Jambo kama Hilo lazima nchi zote ziwe kitu kimoja kumbuka watu wanasafiri nchi mbali mbali itakuwaje kwenye hizo nchi wamepambana wameliondoa gonjwa nyie na ujinga wenu bado mnalo mkisafiri mnawaambukiza wenzenu vinginevyo mbaki kwenu.
Kwani kusafiri ni lazima bwashee?

Dunia iko kiganjani.
 
Hakuna chochote mabeberu watatufanyia maana hawana shida nasi. Lakini muda si mrefu tutajionea madhara ya kujutenga na ulimwengu. Mabeberu watatoa ushauri "travel advisory" kwa watu wao juu ya hatari ya kutembelea nchi yetu. Utalii utakuwa unapaa kwa wengine na kwetu mahotel yataendelea kugeuzwa hostel za wanafunzi wa veta.
 
Nchi za viongozi wenye akili wanaojali raia wao zimenunua chanjo, ikiwa ni pamoja na Madagascar, na zingine kuomba msaada toka WHO kuwalinda watu wao lakini nchi mbili tu za watu wajinga na masikini wa kutupwa kati ya nchi 54 za Afrika eti hawahitaji chanjo wanazo za babu zao za kufukiza za kutosha.

Aibu sana kuwa na viongozi aina hii karne ya Sayansi na Teknolojia!
Beberu jinga wewe
 
Back
Top Bottom