Marekani yaidhinisha chanjo ya Chikungunya, Dengue Duniani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Maafisa wa afya nchini Marekani wameidhinisha kwa mara ya kwanza ulimwenguni chanjo dhidi ya homa ya Chikungunya.

Kulingana na mamlaka inayosimamia chakula na dawa (FDA) ya marekani, chanjo hiyo ambayo imepewa jina la Ixchiq iliyotengenezwa na kampuni ya Ulaya, Valneva, imeidhinishwa kutolewa kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi walioko katika hatari kubwa ya kuambukizwa.

Uidhinishwaji wa chanjo hiyo unatarajiwa kuharakisha usambazwaji wa dozi za chanjo hiyo katika nchi ambazo virusi hivyo vimeenea zaidi hasa Afrika, kusini mashariki mwa Asia na nchi za Amerika.

Chikungunya, husababisha homa na maumivu makali ya viungo.

Virusi vyake huenezwa na mbu na wataalam wa dawa wanavitaja kuwa “tishio la afya linaloongezeka duniani”.

DW
 
Tutafika tumechoka Sana, imagine jina la chanjo sijui natamkaje jina la ugonjwa/homa Kama dawa Sanga-Titi.
Naona haja ya kujitahidi kufurahia kila dakika ya uhai maana binadamu Ana muua binadamu mwenzake.
 
Maafisa wa afya nchini Marekani wameidhinisha kwa mara ya kwanza ulimwenguni chanjo dhidi ya homa ya Chikungunya.

Kulingana na mamlaka inayosimamia chakula na dawa (FDA) ya marekani, chanjo hiyo ambayo imepewa jina la Ixchiq iliyotengenezwa na kampuni ya Ulaya, Valneva, imeidhinishwa kutolewa kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi walioko katika hatari kubwa ya kuambukizwa.

Uidhinishwaji wa chanjo hiyo unatarajiwa kuharakisha usambazwaji wa dozi za chanjo hiyo katika nchi ambazo virusi hivyo vimeenea zaidi hasa Afrika, kusini mashariki mwa Asia na nchi za Amerika.

Chikungunya, husababisha homa na maumivu makali ya viungo.

Virusi vyake huenezwa na mbu na wataalam wa dawa wanavitaja kuwa “tishio la afya linaloongezeka duniani”.

DW
Sisi hatuna makuu. Tunasubiri kesho tu tuanze kuhamasishwa kudungwa. Tutawaona viongozi wetu wakizindua zoezi.
 
Back
Top Bottom