Ni upendo kweli?

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,707
Nimelazimika kujiuliza maswali mengi zaidi leo alfajiri baada ya tukio la kusikitisha; usiku wa leo saa tano nikiwa nimelala niliamshwa ili kumkimbiza hsptl bint aliyekunywa betri acid baada ya aliyekuwa boyfriend wake kumuacha huku akidai bado "anampenda" hivyo kuamua kunywa acid hiyo iliyoutoa kikatili uhai wa binti huyo aliyekuwa anatarajiwa kujiunga na chuo.

Kwani kabla hajakata roho alfajiri ya leo alikuwa anatapika utumbo na vingine vingi, binti huyu alidai upendo ndo ulimpelekea kujitoa uhai kikatili kwani ndivyo alivyokuwa anasema katika masaa machache ya mwisho ya uhai wake na tunamzika leo saa saba.

Hivi upendo una ukatili huu au ni tafsiri yetu mbovu ya upendo? Hebu tueleze wewe unajua nini kuhusu UPENDO ili utusaidie kupunguza majanga haya au kuyamaliza kabisa, binafsi siamini kama upendo unaweza kumpelekea mtu kushindwa kujithamini na kuwathani wengine pia!

Tafadhali naomba maoni au tafsiri yako uwasaidie wengine na tatizo hili.

Msongo wa mawazo, kukosa mtu wa karibu wa kuongea naye na immaturity pia!

Duh!pole sana mpendwa!let her rest in peace!ya moyo wa mtu hakuna awezae jua!kwel inasikitisha lakin ndo upendo!dada inaonekana kampenda sana jamaa yake!

Duh!pole sana mpendwa!let her rest in peace!ya moyo wa mtu hakuna awezae jua!kwel inasikitisha lakin ndo upendo!dada inaonekana kampenda sana jamaa yake!

So unakubali "upendo"ndo ulivyo?Plz don't say yes!

Nimelazimika kujiuliza maswali mengi zaidi leo alfajiri baada ya tukio la kusikitisha;usiku wa leo saa tano nikiwa nimelala niliamshwa ili kumkimbiza hsptl bint aliyekunywa betri acid baada ya aliyekuwa boyfriend wake kumuacha huku akidai bado "anampenda" hivyo kuamua kunywa acid hiyo iliyoutoa kikatili uhai wa binti huyo aliyekuwa anatarajiwa kujiunga na chuo,kwani kabla hajakata roho alfajiri ya leo alikuwa anatapika utumbo na vingine vingi,binti huyu alidai upendo ndo ulimpelekea kujitoa uhai kikatili kwani ndivyo alivyokuwa anasema katika masaa machache ya mwisho ya uhai wake na tunamzika leo saa saba,hivi upendo una ukatili huu au ni tafsiri yetu mbovu ya upendo?Hebu tueleze wewe unajua nini kuhusu UPENDO ili utusaidie kupunguza majanga haya au kuyamaliza kabisa,binafsi siamini kama upendo unaweza kumpelekea mtu kushindwa kujithamini na kuwathani wengine pia!Tafadhali naomba maoni au tafsiri yako uwasaidie wengine na tatizo hili!
Very touchy and heart-moving!
Hapo ndo pa kufanyia utafiti kwa interested parties!

Kwa purpose ya LOVE kama sanaa, lazima kuna vitu fulani vya pekee ambavyo huyu kijana alikuwa anamwambia huyu dada enzi wakiwa katika mahusiano mema, vilivyomfanya huyu dada aone kuwa kumkosa huyu kijana haitowezekana kuishi tena..sasa vitu hivyo ndio vinatakiwa kujulikana hadharani!

Huyu kijana akamatwe apelekwe polisi, si kwa nia ya kumfunga, lakini asaidiane na polisi kueleza kwa taratibu alikuwa anamwambia maneno gani huyu binti, then yaandikwe , na itumiwe kama Mwongozo wa kudumu au precedence katika masomo ya mahusiano y kimapenzi!
Binafsi naitazama kesi hii kwa jicho la 3!

Kuna mwana saikolojia mmoja aliwahi kusema, kitendo cha kujiua hua kinajengwa na mawazo ya mtu mwenyewe, yaani kama mtu anapenda kuongelea hili jambo pale tu anapoghafirika au udhiwa na mtu yoyote mfano hupenda kusema " ikitokea hivi mi ntajiua" basi hili hujengeka kwenye akili yake na pale jambo kubwa linampomtokea basi hali ile inamjia na kuchukua uamuzi huo.
Yeye alishauri kwamba mtu yoyte aipende kuwazia hilo tendo la kujiua kama ndo solution yake ya mwisho na unapo sikia kua mwanao au ndugu yako yoyote anapenda kusema hayo maeneo basi fanya kila namna ili aache.

ujinga kujiua kwa ajili ya mtu umemfahamia ukubwani, simpi pole na namlaani huyo dada kwa uamuzi aliouchukua
sijampenda.

Ni pepo la mapenzi dawa ilikuwa kumuwahisha kwenye maombezi.kwa Jina la Yesu jina lipitalo majina yote lingetoka.

Nadhani huyo dada hakujipenda yeye pamoja na nafsi yake kwa kiasi kikubwa, na badala yake akampenda mshikaji ake sana, let her 'RIP', But what i can say is better to Love youself more than others can do for you, or you cn do for them,

Am very extremely sorry to hear about that love accident, ndivyo mapenzi yalivyo jaman 2yaheshimu mausiano, yanaua watu

I wish falling in love had traffic light, so every one would suggest to go, slow down or just stop to avoid heart accident.

hapana sio upendo bali ni msongo wa mawazo na maamuzi yasio sahihi ndo vilivyosababisha uamuz usio wa maana pole kwa mumpoteza

Niliwahi pia kushuhudia mtu alitaka kujitoa uhai. Upendo ukigeuka unahisi dunia sio yako. Kama hujawahi kupenda kwa moyo wako wote ni ngumu kulielewa hili suala.

inasikitisha,hata nimpende vipi mwanamme,akiniacha,siwezi kuutoa uhai wangu hata siku moja.huko mbeleni hatujui kuko vipi,leo nijitoe uhai kisa mwanamme,yeye baada ya muda ana move on na maisha yake.mtoa uhai,anawaachia huzuni wazazi wake

Kuna watu wanapenda hadi wanawehuka, nahisi huyu alikuwa ni mmoja wao na akili yake ilitenguliwa na mapenzi ndo maana akajiua!

Dah, Binafsi umenikumbusha kifo cha kaka yangu ambaye alijiua kwa Acid kwa sababu hizo hizo.

Very touchy and heart-moving!

Hapo ndo pa kufanyia utafiti kwa interested parties!

Kwa purpose ya LOVE kama sanaa, lazima kuna vitu fulani vya pekee ambavyo huyu kijana alikuwa anamwambia huyu dada enzi wakiwa katika mahusiano mema, vilivyomfanya huyu dada aone kuwa kumkosa huyu kijana haitowezekana kuishi tena..sasa vitu hivyo ndio vinatakiwa kujulikana hadharani!

Huyu kijana akamatwe apelekwe polisi, si kwa nia ya kumfunga, lakini asaidiane na polisi kueleza kwa taratibu alikuwa anamwambia maneno gani huyu binti, then yaandikwe , na itumiwe kama Mwongozo wa kudumu au precedence katika masomo ya mahusiano y kimapenzi!

Binafsi naitazama kesi hii kwa jicho la 3!

Unaweza ukawa sahihi but UPENDO umekua ukisingiziwa mambo kama haya,mtazamo wako ni upi?

Kuna mwana saikolojia mmoja aliwahi kusema, kitendo cha kujiua hua kinajengwa na mawazo ya mtu mwenyewe, yaani kama mtu anapenda kuongelea hili jambo pale tu anapoghafirika au udhiwa na mtu yoyote mfano hupenda kusema " ikitokea hivi mi ntajiua" basi hili hujengeka kwenye akili yake na pale jambo kubwa linampomtokea basi hali ile inamjia na kuchukua uamuzi huo.

Yeye alishauri kwamba mtu yoyte aipende kuwazia hilo tendo la kujiua kama ndo solution yake ya mwisho na unapo sikia kua mwanao au ndugu yako yoyote anapenda kusema hayo maeneo basi fanya kila namna ili aache.

Kwa mujibu wako upendo hausiki hapo!!

Back
Top Bottom