Ni uoga au ni uwezo duni wa waandishi wetu wa habari?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,239
113,612
Kwa mara nyingine tena, Rais wetu huyu Chifu Hangaya amefanya mahojiano na chombo cha habari.

Nimeangalia vipande vipande kadhaa vya mahojiano hayo na sijaona swali lolote lile lililo gumu aliloulizwa huyu chifu wetu.

Anaulizwa vi softballs tu. Naye anatoa majibu mepesi mepesi tu. Sijui mara anaingia mitandaoni, mara anacheza na wajukuu, mara sijui kusikiliza Taarab, yaani mambo mepesi mepesi tu.

Alisema[ga] Le Mutuz, viongozi wetu ni akisi yetu sisi wenyewe wananchi.

Nchi hii ina changamoto kibao. Ina viongozi waongo. Tena waongo wasio hata na haya.

Waandishi wa habari wanapata fursa ya kumhoji Rais aliyeshiriki kudanganya, hawamuulizi kwa nini yeye na wenzake huwa wanatudanganya.

Ni kwenye vijamhuri vya midizi tu kama Tanzania ambako viongozi waandamizi wa kiserikali chao wanawadanganya watu wao kuwa Rais wao ni mzima ilhali si mzima. Ni mgonjwa mahututi au ni marehemu tayari.

Halafu hakuna anayejali [ukinitoa mimi] kuwa kuwa amedanganywa na hakuna anayejali kuona kuwa kunakuwepo na uwajibikaji.

Hangaya ni bora wamuulize maswali hayohayo soft, wakimuuliza magumu anajichanganya sana. Wewe angalia tu hata zile hotuba za kusoma, ni lazima utaona anakoseakosea sana na lazima kuwa na maneno controversial.

Hivyo mimi nashauri waendelee kuuliza hahohayo maswali ya kawaida
 
Nimeshangaa yani kama alikosa maswali kabisa angemuuliza anaonaje au kuzungumzia vitu na bidhaa na huduma kupanda bei kila kukicha?

Basi hata mwandishi alishindwa kuigilizia maswali ya Kikeke akamuuliza? Waandishi wanahangaika kujipendekeza hadi wanasahau kuuliza maswali ya msingi!

Yani watu wameona kujipendekeza kunalipa sana ...na ni kweli wanaogopa kufukuzwa kazi kwa kuuliza maswali magumu
 
Ama wanaogopa kuuliza au nao hawana uwezo wa kuuliza hayo maswali magumu au yawezekana ikawa ni hivyo vyote viwili: yaani waoga na hawana uwezo.
 
Hangaya ni bora wamuulize maswali hayohayo soft, wakimuuliza magumu anajichanganya sana. Wewe angalia tu hata zile hotuba za kusoma, ni lazima utaona anakoseakosea sana na lazima kuwa na maneno controversial.
Hivyo mimi nashauri waendelee kuuliza hahohayo maswali ya kawaida
kwamba wamemuona akili yake ndogo puliziii mkuu naomba na mm niulizwe swali gumu ili nijijua akili yangu inafananaje?.
 
It's a both combination,uoga,uduni wa knowledge,unafiki na wachumia tumbo,hawa wanaojiita ni journalists wa Sasa hakuna hata mmoja anaye wafikia waandishi wale wakati nchi ina heshima na adabu(tutambue walifanya kazi chini ya mfumo wa chama kimoja)kumbuka safari ya President Mwinyi kule Brazil kwenye ile coffee meeting jinsi walivyokula fedha yangu,kumbuka yule waziri aliyeuza twiga wangu kwa bei cheee wakati yeye akijimilikisha dola kibao,ila yote haya niliyajua kutokana na investigative journalism ya journalists makini.
 
CCM kupitia dola huhakikisha Rais hapewi suala lolote la kumtatiza - Mwandishi mtata au mwenye maswali magumu hawezi kupata nafasi ya kufika kwenye hafla hiyo achilia mbali kupata nafasi ya kuuza swali.
Kutawala nchi ya Tanganyika ni rahisi mno ndugu zangu, na urahisi huu umeshafanywa na CCM yenyewe.
 
Wanao muuliza akili ndogo anae ulizwa nae ndio wale wale. Sasa eti baba levo nae mtangazaji unategemea huyu jamaa anauelewa wowote kuhusu mfumuko wa bei? Au steve nyerere anaweza akauliza swali kuhusu kukua kwa uchumi? Hii nchi ivunjwe tuanze upya
 
Back
Top Bottom