#COVID19 Ni ujinga na ukosefu wa maarifa unawasumbua waafrika na watanzania kuhusu chanjo ya COVID-19

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
NI UJINGA TU NA UKOSEFU WA MAARIFA NDIO UNAWASUMBUA WAAFRIKA NA WATANZANIA KUHUSU CHANJO YA COVID 19

Na: Shujaa

Ujue kinachofanya Africa kuwa bara maskini tofauti na mengine ya wazungu na Tanzania kuwa miongoni mwa Nchi maskini duniani pamoja na utajiri na rasilimali nyingi walizo nazo Sio kwasababu wazungu wao Wana kitu Cha ziada zaidi walichopewa na Mungu Bali kinachoitesa Africa au Tanzania NI kuwa na umati mkubwa wa watu wajinga ndani yake ambao hawajijui Kama ni wajinga na hawataki kufundishika kabisa na Wana mawazo duni Wakati wote

Samahani, nisieleweke vibaya, Ujinga Sio tusi Wala siwatukani ila Ujinga NI Hali ya kutokuwa na maarifa sahihi juu ya Jambo husika.Hata uwe Profesa bado kuna maeneo atakuwa mjinga mpaka afundishwe ili aondoe ujiinga.Tunasoma ili kuondoa ujinga.Mwalimu Nyerere alisema Moja ya magonjwa makubwa kwa Taifa letu NI UJINGA.

Hata maandiko ya MUNGU Katika ZABURI73:22 inaeleza kuwa tunakuwa NI wajinga pale ambapo hatujui Sana Neno(Maarifa).Ila inakuwa NI ujinga zaidi ikiwa unajiona Wewe Sio mjinga yaani unajiona Unajua kila kitu hivyo huna haja ya kujifunza na hii ni dalili ya kiburi.Uzuri uliopo kama Mjinga atakubali kujifunza na kupokea maarifa basi hataangamia kea kukosa maarifa


Sasa kwanza, moja ya Ujinga tulio nao watanzania ni Kufikiri sisi Tanzania ni kisiwa ambacho kipo pekee yake na kinaweza kujiendesha peke yake bill kutegemea ushirikiano na dunia Katika maeneo yote

Dunia leo ni Kijiji kinachounganishwa na vitu vingi pamoja.Huwezi kusema huwezi kushirikiana na mataifa ya wazungu, wakati vitu vingi tu unategemea kutoka kwao ili wewe uishi.Tanzania tuna Wafanyabiashara wengi wanaosafiri nje ya Nchi, Tuna viongozi wa dini wengi wanaohubiri INJILI Katika mataifa ya Nje na watu wengi ambao watahitaji kusafiri nje ya mipaka ya Tanzania ambapo kwa hali ya Sasa ya hatari juu ya janga la Corona ,ni kuwa hutaweza kusafiri au kuingia katika Nchi fulani bila kuwa Umepata Chanjo ya Corona Kama njia iliyowekwa kwa mataifa mengi ili kuzuia maambukizi Katika Nchi zao

Tafsiri yake ni Kwamba Kama tuna watumishi wa Mungu wa Kimataifa wanaohubiri Injili kwa kuzunguka duniani kote, ikiwa hawatakubali kuchanjwa,Ina maana wataishia kuhubiri ndani ya Nchi zao au makanisa Yao.Pia ikiwa tunawafanya biashara watakaokataa kupata Chanjo, inamaana hata bidhaa nyingi tunazozitegemea kusafirisha kutoka nje, hatutazipata tena na hali yetu ya maisha kiuchumi Kama Tanzania itakuwa ngumu zaidi.Kwa Sasa Fuatulia bidhaa nyingi zimepanda Bei ila sababu watakwambia ni Corona

Na huku tunapoelekea hata Hawa wanaokataa kupata Chanjo kwa madai yao ya kijinga kuwa wanataka kuuliwa na Chanjo ya wazungu, Itafika hatua hili swala halitakuwa hiyari Tena.Na kwa Hali na hatari ya Corona inavyozidi Itafika hatua hata hawa wanaokataa leo wataitafuta Chanjo wenyewe na gharama zao wenyewe.Time will tell

Sasa Wengine kwasababu ya Ujinga wao, wanaposikia nazungumzia kuwa hawataweza kuuza au kununua au Kusafiri na kuwa watalazimishwa kuchanjwa Kama hutapata Chanjo ya Covid, Tayari Wanaanza kufikiri kuwa eti huyu mtumishi hajui kuwa Kupigwa Chanjo ni alama ya mpinga Kristo ya 666 na hili ndilo linashabikiwa na watu wa ndani ya kanisa kwa namna isiyo ya kawaida na wanahamasishana ujinga kwasababu za kijinga, hata maandiko hawajui ila wanajifanya wajuaji na kufundishana Ujinga

Unayefundisha Kupiga Chanjo ya Covid NI Moja Kati ya masharti ya Mpinga Kristo na kuwa NI alama ya chapa ya 666! Hivi Unajua majira ya Mpinga Kristo au ya chapa ya 666 yanaanza lini?Kwa kuwa una Ujinga ndani yako na umekubali kudanganyika na mafundisho ya mashetani yanayokutia hofu, sitakujibu hata Hiyo hoja yenu Wala sio Lengo langu la makala hii

Lakini kukuonyesha Wewe unayepinga kupata Chanjo kuwa ni mjinga kwa madai ya kuogopa kupata alama ya 666 ya Mpinga Kristo, Nikuulize Je Unajua hata hii mifumo ya kifedha (Electronic Transaction) tunavyotumia duniani kote, NI maandalizi ya Mpinga Kristo?Je Unajua hata matumizi ya alama za vidole(Fingerprint) tunazotumia kujisajili kwenye mifumo mbalimbali ni Moja ya maandalizi ya Mpinga Kristo?Je Unajua hata sarafu ya Euro ya Uingereza ina alama ya 666?Je tuache kuvitumia Hivyo vyote vyenye chapa ya 666 au tuache kufanya Mambo yote yaliyokuwa Katika mifimo hii ya kifedha kwasababu ni sehemu ya maandalizi ya Mpinga Kristo?

Ebu acha Ujinga ulio nao na unaomezeshwa na waalimu wa uongo!Kaa chini ujifunze kama unataka kweli kujua majira ya Mpinga Kristo na Kipi kitafanyika na haya mandalizi yanatu affect Nini Kama watu wa kanisa? Ila Sio kukurupukia Mambo na kuyahusisha na Mpinga Kristo na kuyapa Nguvu kana kwamba Kanisa lipo kwenye dhiki kuu.Wakati kanisa bado lingalipo duniani HAKUNA milango ya kuzimu itakayoliweza kanisa au hakutakuwa kazi za Mpinga Kristo zitakazokuwa na Nguvu dhidi ya kanisa mpaka kanisa linyakuliwe.Hivyo achana kusikiliza haya mafundisho ya mashetani

Ikiwa hutaki kuchanjwa kwa hiyari yako Hakuna anayekuzuia ila usihusianishe maswala haya ya Chanjo na maswala ya Mpinga Kristo na kujitia hofu, achana na hayo mafundisho ya kuzimu yanayozagaa

🔜Ila mwisho, nilitaka kusema, Corona haitaisha leo Wala kesho maana ni miongoni mwa magonjwa ya kuambukizwa ambayo yametabiriwa kuwepo nyakati hizi za mwisho yenye Lengo la kutufanya sisi kanisa tujue mwisho upo karibu ili tuzidi kujitakasa zaidi na kuifanya dunia imtafute Mungu zaidi

Hivyo kwa Msingi huo, Usifikiri utakaa miaka yote Katika Nchi yako bila kusafiri Nchi za nje ambapo itakupasa tu kupata Chanjo ili usafiri na hata ukisema utakaa bado hata huku Itafika wakati hii Chanjo itakuwa ni lazima Sio kwasababu ya Hivi vitu mnavyohusianisha na Mnyama(Mpinga Kristo) ila itakuwa na ulazima kwasababu Tanzania NI sehemu ya dunia , Hivyo italazimika kufanya hivyo kwa kuhakikisha usalama wa afya ya kila mwananchi Katika dunia.Ukiona hutataka hilo Basi katafute sayari yako au sayari yenu ya kuishi huko ambayo hamtashirikiana na wengine wenye mitizamo Kama yenu.

Mwisho kabisa nitoe Rai yangu kuwa niiombe Serikali yetu na Viongozi wa dini wenye ufahamu sahihi kutoa zaidi Elimu kwa watanzania wote kuhusu Chanjo hii, iliyogubikwa na taarifa nyingi za uongo zinazowatia hofu na uoga watanzania kutoka ulimwenguni kote maana pia wengi wao wanaonyesha NI wajinga wasio na maarifa juu ya Chanjo hii, yamkini watapatikana watu baadhi , watakaokubali kufundishika na kuelewa umuhimu wa Chanjo hii, maana wengi bado wapo gizani Kama SI njia panda.Mungu awabariki

Shujaa

0712054498/0759420202

stmwaisembac@gmail.com
 
Andiko lako refu, jibu ni fupi tu, wasiwasi ndo akili kubwa.

Soma naenderthals extinction!!

Wazungu ni wanyama hatari!?

Soma makaburi ya red indians canada, haina hataweek.

Soma ya wajerumani na wanubi wa namibia.

Wide knowledge ndo jibu kwa andiko lako.

Ujinga ndo inaweza Aminisha watu ulichiandika.

Naomba ishia hapo
 
Back
Top Bottom