Ni uhaini - as simple as that!

Ni uhaini - as simple as that!

..kwanza naona Waziri wa Sheria Mathias Chikawe kaamua kula "kobis". anadai mabadiliko haya hayana ramifications zozote zile kwa muungano.

..Zenj ina Raisi,cabinet,baraza la wawakilishi,wimbo wa taifa...kwa mtizamo wangu hayo yote yana-justify mabadiliko ya katiba waliyoyafanya wiki hii. wale wanaotaharuki leo hii ni sawa la watu wanaokumbuka shuka wakati jogoo anawika.

..zaidi, mabadiliko haya yana madhara gani kwa Mtanganyika? personally sioni faida wala hasara za waziwazi za muungano huu kwa wa-Tanganyika. uwepo, usiwepo, najionea sawa tu.

NB:

..Muungano ni unpopular in Zanzibar, and unfeasible to Tanganyikans. Zenj ni ndogo mno kuweza kuwa na muungano wenye usawa na unaeleweka na Tanganyika.

..tuwe majirani wema na wa-Zenj na kushirikiana nao kupitia EAC kama tunavyofanya kwa Burundi na Rwanda.
 
Mambo ambayo Zanzibar wanatakiwa kufanya sasa baada hatimaye "kufafanua" kuwa Zanzibar ni nchi "ndani ya Muungano"..

- Wanahitaji kuwa na Pasi zao za Kusafiria nje ya nchi lakini zitakuwa ni "ndani ya Muungano".
- Waziri wao wa Mambo ya Nje "ndani ya Muungano"
- Jeshi lao la ulinzi "ndani ya Muungano"

Haya yote yanawezekana kwa sababu tayari:

- Wana Rais wao "ndani ya Muungano"
- Bendera yao ya Taifa "ndani ya Muungano"
- Wimbo wao wa Taifa "ndani ya Muungano"
- Alama zao za Taifa "ndani ya Muungano"
 
Shwari, I have never read information suggesting ''bombing'' in JF. I ask you to revist MMKJ's article for clarity and better understanding of the debate. MMKJ had it that, since the union is based on mutual agreement,then any changes, modification or nullification should be reached bilaterally. The unilateral decision taken by SMZ to effect changes on constitution of Znz will have an impact on the union constitution.We all know that breaching of extant constitution is nothing but a treason. So, If there is a person who negate the theory of treason as propounded by MMKJ, that person should prove it wrong in this forum.
The Znz want to play double standard, nitty gritty!, that is she want secession while retaining the union status for certain gains.Tanganyikan are vexed with the union which has gotten some hypocracy. The gist as put forward by JF member is, znz should come forward with proposal of killing the union with certitude, from there, the two nations could have a new rapproachment.
We can dissolve the union amicably and maintain historical fraternity, but not through the bungled procedure. As far as I understand Tanganyikan are all weather, therefore the onerous to decide the fate of union through referendum lies to Znz.
I for one, would like to challenge the SMZ government leaders [some are JF members] with acumen clarify the SMZ position in Union with clear terms, not snookering the mainlanders. It is obvious that the ZNz topic has derailed us from the basic and important issue come october 30. We want to put the story behind and ponder the fate of our nation in five years to come with or without Zanzibarian.

Well let us talk about mutual understanding as you prophes. Between who the mutual understand wil be? of course it is Zanzibar and Tanganyika not Tanzania. It is over doubt that the Union is between Zanzibar and Tanganyika. It happens that Zanzibar are not hyprocratic as Tanganyika into cheating i itself in what is refered as Tanzania. Zanzibar constitution was there before the Union constitution and the Zanzibaris themselves constituted it. They have the due right to it without interference from the other member of Union (Tanganyika).
What you call mutual unerstanding always stands between willingly bodies and it should apply to this case. Tanganyika has no option but to negotiate with Zanzibar if it thinks the ammendment will effect it. However I dont see that there is any effect to Tanganyika but for Zanzibar and for better for that matter. Perhaps the Mwanakijijis are irked with this.
 
Mambo ambayo Zanzibar wanatakiwa kufanya sasa baada hatimaye "kufafanua" kuwa Zanzibar ni nchi "ndani ya Muungano"..

- Wanahitaji kuwa na Pasi zao za Kusafiria nje ya nchi lakini zitakuwa ni "ndani ya Muungano".
- Waziri wao wa Mambo ya Nje "ndani ya Muungano"
- Jeshi lao la ulinzi "ndani ya Muungano"

Haya yote yanawezekana kwa sababu tayari:

- Wana Rais wao "ndani ya Muungano"
- Bendera yao ya Taifa "ndani ya Muungano"
- Wimbo wao wa Taifa "ndani ya Muungano"
- Alama zao za Taifa "ndani ya Muungano"

Mzee Mwakijiji tafadhali usiwe ndumila kuwili. Kumbuka wapi Muungano ulikotokea na ulipo sasa. Kama Muungano ulipita katika mabadiliko mengi ambayo yalitowa faida kwa upande mmoja basi kubali kuwa na upande mwengine una zamu yake kunufaika.

Nashindwa kukuelewa kipi unachokilalamikia iwapo hapo kabla mabadiliko yalifanywa na ukayafurahia lakini sasa unataka Muungano udumae usiwe na mabadiliko? Zanzibar waachie wadai na waweke wanachoona kinawafaa hili la kusema kuwa baada ya hili watadai hili au lile lisiwe kigezo cha kuwakosoa Wazanzibari. Sasa waache wafanye mabadiliko na ukifika wakati wakisema hatutaki Muungano basi itakuwa hivyo kwani si wameungana kwa hiyari yao?
 
Mambo ambayo Zanzibar wanatakiwa kufanya sasa baada hatimaye "kufafanua" kuwa Zanzibar ni nchi "ndani ya Muungano"..

- Wanahitaji kuwa na Pasi zao za Kusafiria nje ya nchi lakini zitakuwa ni "ndani ya Muungano".
- Waziri wao wa Mambo ya Nje "ndani ya Muungano"
- Jeshi lao la ulinzi "ndani ya Muungano"

Haya yote yanawezekana kwa sababu tayari:

- Wana Rais wao "ndani ya Muungano"
- Bendera yao ya Taifa "ndani ya Muungano"
- Wimbo wao wa Taifa "ndani ya Muungano"
- Alama zao za Taifa "ndani ya Muungano"

Kwa sasa ni vigumu kumuaminisha mtu kuwa Rais wa muungano ana shughuli ya kufanya zanzibar .Muungano uliobaki sasa ni wa karatasi tu tunazozitambua sisi watu wa bara, hatudanganyiki na maneno matamu yaliyotumika kutoa ufafanuzi.Baada ya uchaguzi hatua za dhati zitumike aidha kurekebisha mgongano huu wa kikatiba au tuachane na Zanzibar tugange yajayo .
 
Hii inaitwa hekima; kwa sababu wakishatoka kwenye muungano wataanza kudai nini? watakuwa wamepata wanachotaka au watarudi kwenye status quo ya 1963 baada ya Mwingireza kuondoka, serikali kuwa chini ya kina Shamte (na Sultani kama figure head) nakabla ya mapinduzi? Kwa sababu haijawahi kuwepo serikali ambayo imefanya kazi ya "nchi ya zAnzibar" ukiondoa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hili la kujifanya Godfather litawasumbua sana. Umesahau kuwa Zanzibar iliishi ipendavyo hadi pale Abedi Karume alipouliwa? Mbona kulikuwa na mengi yaliyoyakifanywa yenye kutowa mfano kwa Tanganyika? Mnajidanganya kuwa zanzibar ikiwa huru tena(uhuru walioupoteza 1977) haitoweza kusurvive. Kama suala la kujaribu fanyeni lakini najuwa ni tabu kwani sifa yenu ya ubabe itashuka.
 
Kila kitu kina mwanzo wake, wakiondoka ndani ya Muungano wataunda seikali yao mpya wanavyopenda wao ili mradi wananchi wake wanaridhika. Lakini najua wazi yatafuata ya Comoro kwani hawa watu maswahiba wangu sana tu, ni wabishi sijapata kuona watatiana vidole vya macho wala haitachukua miaka mingi. Kisha Bara itapigiwa SOS..

Hapo umekosea sana mwenzangu. Kama Tanganyika (Tanzania Bara) inaendelea kuwepo basi Zanzibar itendelea kuwepo kwani kama mauwaji,ufisadi na kuangamiza nchi kuko zaidi Bara kuliko Zanzibar. HATA HIVYO ZANZIBAR NI YA WAZANZIBARI WAUWANE WACHINJANE NI NCHI YAO na kuitawala hatutawabadilisha Wazanzibari bali watakapokuwa huru ndio watakuwa responsible na nchi yao.
 
Mwanakijiji said:
Mambo ambayo Zanzibar wanatakiwa kufanya sasa baada hatimaye "kufafanua" kuwa Zanzibar ni nchi "ndani ya Muungano"..

- Wanahitaji kuwa na Pasi zao za Kusafiria nje ya nchi lakini zitakuwa ni "ndani ya Muungano".
- Waziri wao wa Mambo ya Nje "ndani ya Muungano"
- Jeshi lao la ulinzi "ndani ya Muungano"

Haya yote yanawezekana kwa sababu tayari:

- Wana Rais wao "ndani ya Muungano"
- Bendera yao ya Taifa "ndani ya Muungano"
- Wimbo wao wa Taifa "ndani ya Muungano"
- Alama zao za Taifa "ndani ya Muungano"

Mwanakijiji,

..let them have all that.

..kwani inatuzuia nini sisi wa-Tanganyika kuwa navyo?

..kuna mambo mengi ya msingi yanayoihusu Tanganyika[watu milioni 37] tunapaswa kuyajadili hayo kuliko kusumbuka na masuala ya ndani ya wa-Zenj wasiozidi hata milion 2.
 
Hii dhana kuwa wengine ni watumwa na nyie ni waungwana ndiyo itawapeleka pabaya. Hata siku moja hamwezi kumheshimu yule ambae mnamhesabu kuwa ni mtumwa. Ndiyo maana wengine tunasema tuvunje Muungano, tuimarishe mipaka baina ya nchi zetu, halafu tuone itakavyokuwa. Kwangu mimi kumhesabu mtu mwenye mawazo kama yako kuwa ni raia mwenzangu inanitia kichechefu. Vunjeni muunganoo na as far as I am concerned "good riddance"!

Amandla.....

Unapotosha maana! Anachofanya Junius ni kukupeni Challenge na hiyo yote ni misemo ya lugha na kama nyie hamko hivyo basi hiyo misemo haikuguseni.

La kujiuliza jee mnaukubali Utanganyika? na pili Muungwana anakubali kwao na yeye mbali ya dharau mnayoiwekea Zanzibar bado anafahari kuwa Mzanzibari. Ama kwa wewe kuwa Muungwana ni kukubali kuwa Mtanganyika basi!
 
Junius,
Mkuu wangu pengine wewe unatazama vitu kwa uasilia wa uzawa kuhalalisha matendo ya Viongozi wa Zanzibar. Labda nikupe mfano mzuri sana unaolingana na kile kilichotokea Zanzibar. Pengine unafikiri kwamba Bara hatufahamu au hatuna akili isipokuwa maneno mengi yasiyokuwa na vitendo..

Huo muafaka wenu pamoja na hizo kura za maoni ni sawa na CUF wamekubali kuwa mke wa pili wa CCM Bara, baada ya mke mkubwa Baraza la Mapinduzi kuafiki kushare mume mmoja. before this CUF was independent lakini sasa hivi mnategemea CCM bara watakubaliana nanyi ktk maswala yapi kama mume wa pande zote mbili.

Na kibaya zaidi ni kwamba nyie sii watoto halali wa CCM, mnaingia ktk nyumba ya baba wa kambo pasipo kupenda kutokana na ashiki za mama yenu CUF. Sasa CCM bara itawaridhisha wake wote na kila mnavyozidi kudai vitu ndivyo CCM bara wanajiona wao ni waume wa shoka yaani wanaweza ku handle wake wawili..Lakini tatizo ni kwamba nyie watoto wa huyu mama CUF kawaahidi maisha bora kwa kutazama mfuko wa CCM bara na sio ubunifu wa mipango inayowawezesha nyie kujipinda kivyenu, kupewa nyumba yenu ya kuishi haina maana mna uhuru zaidi.

Haya madai ya viongozi wenu ati wameungana ni kamba tu wanakufungeni kwani kuungana kwa hawa wake wawili ili iwe nini?...wake hawa wote wanamtegemea mume huyo huyo CCM bara sasa mnachodai hasa ni kitu gani ktk haki na Uhuru wa Wazanzibar?.. Na ndio maana viongozi wenu hawadai talaka isipokuwa wanadai kila mmoja wao apewe hiki ama kile na kibaya zaidi kwa umoja wao wote hakuna madai yoyote yanayohusiana na watoto wao yaani nyie Wanzanzibar..

Hivi kweli wewe na akili yako malalamiko yako siku zote ilikuwa ujue Zanzibar ni nchi au sio nchi ndani ya Muungano?..Hilo tu. na kichekesho kikubwa ni kwamba mnachukulia Muungano wa nchi nyingine ili kutafsiri Muungano wa Tanzania hali Muungano wetu ni unique , tofauti kabisa na miungano mingine kwani tumeua nchi mbili kuunda moja wakati huohuo tukiepuka Zanzibar kumezwa na Tanganyika ndio maana ikawepo serikali ya Zanzibar tukaua serikali ya Bara. Lakini kama tutaunda serikali tatu na kwa kufuata mifano ya mfumo wa nchi nyinginezo Zanzibar itamezwa vibaya sana.

Mnachoshindwa kuelewa ni kwamba muundo huu tuliokuwa nao umetokana na kuepuka kuunda serikali tatu za Muungano kwani haziwezi kuleta uuwiano wa aina yeyote ile. Bara ni nchi kubwa sana ina watu wasiopungua millioni 40 hali Visiwani isojaa kiganjani hawafiki hata millioni 2. Sasa kumbuka tu kwamba siku zote kuundwa kwa serikali tatu kunaondoa utaratibu wote wa kupokezana Uongozi ktk ngazi ya Jamhuri. Hapo ndipo itakuwa mwisho wa kuona Mzanzibar ndani ya uongozi wa nchi hii. Kisha mtalianzisha upya maanake hamtakubali kuwekwa pembeni kabisa, next thing, yatakuwa madai ya kuvunja Muungano, huu sii ujanja ila ni Uhaini kwa msemo wa Mwanakijiji.
 
Mnyasa. Kwa hiyo......?

Amandla.......

kwa hiyo??

Hoja yangu taifa halijengwi kama mwamba au bahari ambavyo havihami, mzanzibari wa leo ndiye atakayezaa Mnamibia wa Kesho, Kabla ya wale waliopo zanzibar leo kuwepo ile nchi ilikuwa ni tupu.

Mipaka inayoliliwa leo na Wanzanzibar iliwekwa na wakoloni, cha ajabu ile iliyowekwa na Karume na Nyerere ndiyo tunayohoji uhalali wake, mbona hatujiulizi mndengereko Ally Hassani Mwinyi alifikaje Zanzibar, kwao ni Mkuranga au Unguja??
 
Kuna kitu wazanzibar hawajakitambua na sidhani kuwa wanajua kwanini hawakijui. Hoja hapa si kuzuia wznz kuamua mustakabali wao. Jambo la muhimu ni kuwa wafanye hivyo bila unafiki [hypocracy]. Wana Rais wao "ndani ya Muungano"Bendera yao ya Taifa "ndani ya Muungano",Wimbo wao wa Taifa "ndani ya Muungano",Alama zao za Taifa "ndani ya Muungano" . Mwaka huu wameenda mbali eti wanadai kwanini znz haijatoa mkuu wa majeshi [bungeni] kana kwamba wakuu wa majeshi wanapigiwa kura. Wakipewa uwaziri bara hilo ni muungano, wakitaka kuingiza bidhaa kupitia badari huru znz kukwepa kodi hilo ni muungano, wakipewa ajira mamia kwa maelefu huku bara hilo ni muungano, wakigombea ubunge mkuranga hilo ni muungano, wakilipwa mishahara na kodi za bara hilo ni muungano. Huu unafiki [hypocracy] ndio MMKJ ameuweka katika lugha nzuri '' uhaini'' au treason.[ Treason= betray of one's sovereign or country. Treachery or disloyalty].
Ndio maana tunasema viongozi wenu watamke kuwa mnataka muungano au mumeshauvunja. Watanganyika hawapendi unafiki katika hili.
 
Mwana kijiji ndio nani ?jamaa anauka Uongo amekuwa na wafuwasi wake hapa analolisema hawakawii kutowa asante leo hii anajifanya profisa mchundo na kutafsi katiba ambayo haijuwi nini kimo ndani yake ,binafsi ningemuomba arudi tena na akufahamisheni jee alikosea katika kutowa tasmini zake au ndio miongoni mwaprofisa wa Jf hutafuta wale wasiokuwa na mbele wala nyuma na kuwahada kuwa wao wanaelewa ukweli wa Mungano ( unapoambiwa ujiambie )

Spear, wewe kweli mkuki wa kuchimbia mihogo!!
Mtu kama wewe ni kati ya wale wasio na mchango wowote katika kuboresha mawazo au hata kuyapinga kwa ubishani wa kimantiki iletayo afya.
Mada hii ya MMKJJ imevuta hisia kali bordering on alarm on the part of many Tanzanians and Tanganyikans in particular.
Inawezekana kabisa kwamba wewe you are so thick skinned kufikia hali ya kutoelewa kinachoendelea.
Ukiishiwa mawazo mkuki wako kachimbie mihogo, si kumchoma the messenger wa mada.Kama message imekufikia toa maoni yako.Jaribio lako la kumdiscredit MMKJJ ni la kitoto
 
NA siku hizi ukienda mahakamani ni sawa unaenda kuiabisha mahakama kwa huo uamuzi itakayoutoa dhidi ya kesi yoyote against utawala ama walawala wlioko madarakani.
 
Hili la kujifanya Godfather litawasumbua sana. Umesahau kuwa Zanzibar iliishi ipendavyo hadi pale Abedi Karume alipouliwa? Mbona kulikuwa na mengi yaliyoyakifanywa yenye kutowa mfano kwa Tanganyika? Mnajidanganya kuwa zanzibar ikiwa huru tena(uhuru walioupoteza 1977) haitoweza kusurvive. Kama suala la kujaribu fanyeni lakini najuwa ni tabu kwani sifa yenu ya ubabe itashuka.

Unapotosha maana! Anachofanya Junius ni kukupeni Challenge na hiyo yote ni misemo ya lugha na kama nyie hamko hivyo basi hiyo misemo haikuguseni.

La kujiuliza jee mnaukubali Utanganyika? na pili Muungwana anakubali kwao na yeye mbali ya dharau mnayoiwekea Zanzibar bado anafahari kuwa Mzanzibari. Ama kwa wewe kuwa Muungwana ni kukubali kuwa Mtanganyika basi!

Wewe na Junius hamna tofauti. Mwenzako anatamani utumwa wewe una enzi utawala wa kikoloni na wakisultani! Nyinyi ndio wanafik. Semeni wazi kuwa tunataka tuvunje Muungano ili turudishe hali ya neema ilivyokuwa kabla ya Mapinduzi. Huo uzanzibari mnaojisifia ni ule wa mtwana na muungwana.

Sisi machogo tunajisifia nchi yetu, Tanzania. Awali ya hapo bila shaka Tanganyika. Tunaonyesha mapenzi yetu kwa vitendo. Linganisha wazanzibari (kwa asilimia) wangapi wamehamia Bara na machogo wangapi wako Zanzibar. Mnajidanganya na kujibalaghua kuwa machogo wanawaonea kijicho wakati ukweli ni kuwa wengi wetu could not care less kama mkiwemo ama mkiondoka. Hao viongozi wenu wakishaachia ngazi wote wanakimbilia bara ambako mnadai wamejaa watu waovu! Nyinyi ni hypocrites na tunawajua. Mkiondoka na mkianza kuchinjana mtatulaumu kwa kukubali kuvunja Muungano!

Amandla......
 
Kuna kitu wazanzibar hawajakitambua na sidhani kuwa wanajua kwanini hawakijui. Hoja hapa si kuzuia wznz kuamua mustakabali wao. Jambo la muhimu ni kuwa wafanye hivyo bila unafiki [hypocracy]. Wana Rais wao "ndani ya Muungano"Bendera yao ya Taifa "ndani ya Muungano",Wimbo wao wa Taifa "ndani ya Muungano",Alama zao za Taifa "ndani ya Muungano" . Mwaka huu wameenda mbali eti wanadai kwanini znz haijatoa mkuu wa majeshi [bungeni] kana kwamba wakuu wa majeshi wanapigiwa kura. Wakipewa uwaziri bara hilo ni muungano, wakitaka kuingiza bidhaa kupitia badari huru znz kukwepa kodi hilo ni muungano, wakipewa ajira mamia kwa maelefu huku bara hilo ni muungano, wakigombea ubunge mkuranga hilo ni muungano, wakilipwa mishahara na kodi za bara hilo ni muungano. Huu unafiki [hypocracy] ndio MMKJ ameuweka katika lugha nzuri '' uhaini'' au treason.[ Treason= betray of one's sovereign or country. Treachery or disloyalty].
Ndio maana tunasema viongozi wenu watamke kuwa mnataka muungano au mumeshauvunja. Watanganyika hawapendi unafiki katika hili.

My sentiments exactly. Wakifika hapo wanasita maana wanajijua kuwa hawawezi ku'survive' nje ya Muungano! Wanachotaka ni wafukuzwe ili mambo yatakapowaendea mrama wapate wa kumlaumu. Wanafik wakubwa hawa.

Amandla........
 
Haaa... haaa ... heee.. heee.. Kama ni kweli... haya ndio matokeo ya kumchagua msanii na kumpa urais. Mpaka aje aondoke na kwetu Morogoro kutakuwa ni jamhuri ya watu wa Morogoro.
Nimesoma meseji za wengi humu ila yako tu ndo nimeiona umeandika pumba, yaelekea hata hujui mada iliyopo na pia hata ulichoandika huenda pia hukijui. Hufai humu JF
Suala lililoka hapa si ubabe bali kuangalia uhalisia wa mambo, Ile kusema tu JK kwa sababu ni Rais atumie force haisaidii. atakuwa anaongoza miili ya watu na si nyoyo za watu kitu ambacho ndo lengo.
Natamani waZenj wangejitenga, wamekuwa maadui wao kwa wao kwa zaidi ya miaka 10, lakini adui wao alikuwa mbara ambaye alikuwa anatumia sera ya divide and rule. Zenj inawatu around 1mil, naamini kama watajitenga ni rahisi kwao kuendelea na kufika mbali kiuchumi kuliko kuchanganyikana na manyang'au ya huku bara kwani yenyewe yamekaa kunenepisha matumbo yao tu kwa kutuibia.
 
Junius,
Mkuu wangu pengine wewe unatazama vitu kwa uasilia wa uzawa kuhalalisha matendo ya Viongozi wa Zanzibar. Labda nikupe mfano mzuri sana unaolingana na kile kilichotokea Zanzibar. Pengine unafikiri kwamba Bara hatufahamu au hatuna akili isipokuwa maneno mengi yasiyokuwa na vitendo..

Huo muafaka wenu pamoja na hizo kura za maoni ni sawa na CUF wamekubali kuwa mke wa pili wa CCM Bara, baada ya mke mkubwa Baraza la Mapinduzi kuafiki kushare mume mmoja. before this CUF was independent lakini sasa hivi mnategemea CCM bara watakubaliana nanyi ktk maswala yapi kama mume wa pande zote mbili.

Na kibaya zaidi ni kwamba nyie sii watoto halali wa CCM, mnaingia ktk nyumba ya baba wa kambo pasipo kupenda kutokana na ashiki za mama yenu CUF. Sasa CCM bara itawaridhisha wake wote na kila mnavyozidi kudai vitu ndivyo CCM bara wanajiona wao ni waume wa shoka yaani wanaweza ku handle wake wawili..Lakini tatizo ni kwamba nyie watoto wa huyu mama CUF kawaahidi maisha bora kwa kutazama mfuko wa CCM bara na sio ubunifu wa mipango inayowawezesha nyie kujipinda kivyenu, kupewa nyumba yenu ya kuishi haina maana mna uhuru zaidi.

Haya madai ya viongozi wenu ati wameungana ni kamba tu wanakufungeni kwani kuungana kwa hawa wake wawili ili iwe nini?...wake hawa wote wanamtegemea mume huyo huyo CCM bara sasa mnachodai hasa ni kitu gani ktk haki na Uhuru wa Wazanzibar?.. Na ndio maana viongozi wenu hawadai talaka isipokuwa wanadai kila mmoja wao apewe hiki ama kile na kibaya zaidi kwa umoja wao wote hakuna madai yoyote yanayohusiana na watoto wao yaani nyie Wanzanzibar..

Hivi kweli wewe na akili yako malalamiko yako siku zote ilikuwa ujue Zanzibar ni nchi au sio nchi ndani ya Muungano?..Hilo tu. na kichekesho kikubwa ni kwamba mnachukulia Muungano wa nchi nyingine ili kutafsiri Muungano wa Tanzania hali Muungano wetu ni unique , tofauti kabisa na miungano mingine kwani tumeua nchi mbili kuunda moja wakati huohuo tukiepuka Zanzibar kumezwa na Tanganyika ndio maana ikawepo serikali ya Zanzibar tukaua serikali ya Bara. Lakini kama tutaunda serikali tatu na kwa kufuata mifano ya mfumo wa nchi nyinginezo Zanzibar itamezwa vibaya sana.

Mnachoshindwa kuelewa ni kwamba muundo huu tuliokuwa nao umetokana na kuepuka kuunda serikali tatu za Muungano kwani haziwezi kuleta uuwiano wa aina yeyote ile. Bara ni nchi kubwa sana ina watu wasiopungua millioni 40 hali Visiwani isojaa kiganjani hawafiki hata millioni 2. Sasa kumbuka tu kwamba siku zote kuundwa kwa serikali tatu kunaondoa utaratibu wote wa kupokezana Uongozi ktk ngazi ya Jamhuri. Hapo ndipo itakuwa mwisho wa kuona Mzanzibar ndani ya uongozi wa nchi hii. Kisha mtalianzisha upya maanake hamtakubali kuwekwa pembeni kabisa, next thing, yatakuwa madai ya kuvunja Muungano, huu sii ujanja ila ni Uhaini kwa msemo wa Mwanakijiji.

Swahiba,
The best comment!!
1. Walichofanya hawa wahuni ni Uhaini
2. Good Timing: wanajua Kikwete anataka support ya kura zao, na support ya CCM Zanzibar, Kikwete (a weak president) naye amewafanyia timing, italipuka tu hiyo baada ya uchaguzi.
3. Zanzibaris are tired of stability; they are used to 'chaos". If they were clever enough they would rather fight for economic emancipation, and more autonomy to implent some of the issues. Kama ulivyosema hapo juu; ungeongeza tu kuwa akina Seif na hao wengine wanataka kuwa "big fish in a small pond".
4, Nafikiri hii comment yako ungeiweka vile vile kwenye open media outlet, kwenye magazeti ya Tanzania ingependeza sana.

Congrats
 
Mambo ambayo Zanzibar wanatakiwa kufanya sasa baada hatimaye "kufafanua" kuwa Zanzibar ni nchi "ndani ya Muungano"..

- Wanahitaji kuwa na Pasi zao za Kusafiria nje ya nchi lakini zitakuwa ni "ndani ya Muungano".
- Waziri wao wa Mambo ya Nje "ndani ya Muungano"
- Jeshi lao la ulinzi "ndani ya Muungano"

Haya yote yanawezekana kwa sababu tayari:

- Wana Rais wao "ndani ya Muungano"
- Bendera yao ya Taifa "ndani ya Muungano"
- Wimbo wao wa Taifa "ndani ya Muungano"
- Alama zao za Taifa "ndani ya Muungano"

Mwanakijiji,
Labda kabla ya kuweka comments hapa hebu tupe data ya ile population composition of Zanzibar. Sijawahi kufika huko (na sijawahi hata kufikiri kwenda huko). Nasikia kuna waarabu, Waajemi, halafu Weusi. Na katika hawa kuna mixtures. Ninachokumbuka ni kuwa wengi wa hawa walienda kule kutoka barani africa (bara) kupitia biashara ya utumwa. They settled there. Inawezekana ni kweli kabisa wachache sana ndiyo wanapiga kelele na kuwa na mpango wa kuvunja muungano. Mie sielewi kabisa, Mwafrika mweusi atamani avunje muungano na mwafrika mwenzie ili ajiunge na Waarabu, it doesn't add up.
Stats please! Statistics zinaweza kutusaidia.
 
Hili suala ni la kikatiba zaidi "tena ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Na kwa vile siyo ndani ya katiba ya Zanzibar, basi inabidi wahusika wanaofikilia kujiengua kwenye utaratibu huu, basi wafuate taratibu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si vinginevyo kama inavyoelekea kufanywa kwa kubadilisha Katiba ya Zanzibar na kuita Zanzibar ni nchi halali nje ya Jamhuri ya Muungano. Na hapo ndipo suala la "Uhaini" linakuja, kwa vile Katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa imekiukwa... Tuwe makini sote katika suala hili kadri linavyokwenda mbele.
 
Back
Top Bottom