Ni uhaini - as simple as that!

Ni uhaini - as simple as that!

Shwari,
Thanks for good narrative. Just to remind you, in 1964 we formed the union between the then Tanganyika and Zanzibar, both side signed the article of Union and URT constitution. I fully understand that there is contention on contents of article of union and the URT constitution. Miraculously,the Znz retained semi autonomy since 1964. In other words there is Znz and Tanzania[znz inclusive]. Tanganyikans never complained of relinguishing too much for the sake of unity.
The Znzbarian have been using the secession as a weapon when they want their demands meet. They started with soccer team, then National flag,national anthem, then consitution, Not namedTanzania, now borders etc etc. However, for any beneficial issue to them, like land, employment and other services they never identify themselves as Zanzibarian but Tanzania. Changes effected on monday is an example of hypocracy by our brothers.Let me testify the hypocracy theory of Znz. Oil is not a union matter, but land is !!! How could it be posible to extract oil from the sky!!!
So, if you understand the concern of majority in this forum, you should be well informed that we as Tanganyikans have no intention to stop the Znz decide their fate. It is imperative that they exercise the freedom with acumen,candid and transparently without bungling procedure. I would like them to have referendum on union, and I will honour their decision. There is no point of affronting each other or using muscles to hold them. The problem with Znz is on modus operandi, in this context I challenge the Leaders to express their grievance openly and with veracity instead of promoting the treason act with cheap and unpopular politics.
For Tanganyikans, Union is better as everybody is striving for in this new world. However we will not be losers simply because they are gone!
 
Mimi nilisema kuwa toka mwanzo kuwa haya mabadiliko ni lazima yalihusisha wakuu wa JMT. Kitu ambacho kinatugonga wenye akili finyu ni kuwa kama Zanzibar ni nchi moja kati ya nchi mbili ziNAZOunda JMT, ya pili ni ipi? Na mipaka yake iko wapi? Mimi ninavyojua ni kuwa Zanzibar ilikuwa ni moja ya nchi mbili ziLIZOunda JMT. Ni makosa kudai kuwa kusema kuwa Zanzibar ni nchi bila kuweka wazi nchi ya pili ni ipi na maana ya hilo neno nchi. Kama nchi ya pili inayounda JMT ni JMT basi Zanzibar wana haki ya kudai usawa na nchi mwenza mwenzao. Rais wa JMT hatakuwa na mamlaka yeyote ndani ya Zanzibar na wa Zanzibar ndani ya JMT. Maana yake tunakuwa na muungano wa nchi mbili zilizo sawa bila kuwa na authority inayoziunganisha. Muungano kama huu bila shaka utakuwa wa wasiwasi. Kilichotakiwa kuwekwa wazi ni kuwa Zanzibar si nchi ndani ya JMT bali ni sehemu iliyopewa haki za pekee za kuwa na uongozi wake na utawala katika baadhi ya mambo. Wanachofanya wenzetu ni kujaribu kuweka neno sovereign kinyemela mbele ya state. Yalikuwa ni makosa kujaribu kuwa-appease wazanzibari kwa kuwapa parity na JMT.

Hilo la kumpa madaraka Rais wa Zanzibar kugawa mipaka ya mikoa nchini mwake in consultation na Rais mwenza wa JMT bila kusema huyo mwenza ana uwezo gani wa kuzuia mabadiliko ambayo haafik nayo ni hatari vile vile. Ni usanii mtupu. Je Rais wa nchi ya Zanzibar akiamua kugawa mikoa na wilaya ili kuizidi mikoa iliyopo huko kwenye JMT na kwa namna hiyo kuwapa uwakilishi katika bunge -uwakilishi ambao ni debatable- uliozidi wa kutoka JMT. Wamarekani wana neno gerrymandering. Mamlaka haya hayakutakiwa kuwekwa kwenye mtu bali chombo. Wakati umefika wa kujadili mfumo wa Muungano kwa mapana yake badala ya kuruhusu watu wachache kuutafsiri wanavyotaka. Sisi sio wa kwanza kuwa na Muungano. Ni lazima tujifunze kwa wenzetu.

Kitu kingine ambacho ningependa kujua, ni jee katiba yetu na ya wenzetu zinazuia coalition governments? Kwamba vyama vinazuiwa kikatiba kushirikiana katika kutawala? Kwa maana nyingine, chama kinachoshinda uchaguzi wa urais, hakiruhusiwi kuwa na viongozi katika serikali yake kutoka vyama vya upinzani hata kama chama hicho kitakuwa hakijapata wabunge wakutosha kuweza kuunda serikali?

Amandla.......
 
...

As President of Tanzania it is my duty to safeguard the integrity of the United Republic. But if the mass of the people of Zanzibar should, without external manipulation, and for some reason of their own, decide that the Union was prejudicial to their existence, I could not advocate bombing them into submission. To do so would not be to defend the Union. The Union would have ceased to exist when the consent of its constituent members was withdrawn. I would certainly be one of those working hard to prevent secession, or to reduce its disintegrating effects. But I could not support a war on the people whom I have sworn to serve - especially not if the secession is preceded by a rejection of Zanzibaris by Tanganyikans.

Natamani mtu mmoja angekuwa na fikra kama hizo.
 
Natamani mtu mmoja angekuwa na fikra kama hizo.
Mkuu lakini unajua kwamba hakuna mtu wala kiongozi yeyote wa Zanzibar aliyetaka au anayetaka kuuvunja Muungano?
Inaonyesha wazi ni hapa JF tu ndio watu wengi wanazungumzia kuuvunja Muungano kama haki ya Wazanzibar kufanya hivyo ikiwa wanataka kuondoka ktk Muungano. Na sidhani kama ndio hoja yetu sisi kwani kwani hakuna swala hili )la kuuvunja Muungano) mezani hivyo tunapojibishana hapa tunachanganya vitu kuwasikiliza hawa kina Shwari.

Viongozi wa Zanzibar wanataka madaraka zaidi na kwa bahati mbaya hakuna sehemu kubwa ya kuchukua madaraka hayo isipokuwa sehemu ndogo ya wananchi wa visiwa vya Zanzibar. Hivyo kinachofanyika ni kuunda serikali kubwa yenye ulaji kwa kila mtu wakisingizia mipaka ya Zanzibar na kadhalika. Wananchi wanafurahia kutia changa la macho mchana kweupeee.

Mimi nawaomba sana viongozi wa Zanzibar kama kweli wanasimamia mawazo ya wananchi wake waombe kuuvunja Muiungano kisha yatakayofuatia baada ya hapo wagawane madaraka wanavyopenda. Lakini hawawezi kutumia nafasi ya Muungano kuleta madai kama vile mtu asiyeridhika ndani ya ndoa lakini hataki kuomba talaka isipokuwa kila siku kuongeza madai ili mradi kumuudhi mwenza wake akiwa ndani ya ndoa. Na kwa maana hii ndio maana ya kifungu kinachosema hivi:- As President of Tanzania it is my duty to safeguard the integrity of the United Republic. kinasimamia kulinda kilichopo kama vile mtu anavyoweza kuilinda ndoa yake dhidi ya maudhi ikiwa hakuna mtu anayedai talaka. Mume au Mke atailinda ndoa kwa machafu yote hadi mmoja wao atakapo omba talaka yake ndipo swala linakuwa na uzito tofauti.

Hivyo, maelezo aliyonukuu mkuu wangu Shwari yanasimamia maudhui kama haya yanayotokea leo ndani ya Muungano. Na ni jukumu la JK kuulinda Muungano wetu hadi siku mmoja wetu kwa kauli yake atakapodai kujitenga kama walivyofanya Biafra.

Zanzibar hawajawahi kusema wanataka kuuvunja Muungano na Bara ikawakatalia kama wailivyokuwa Nigeria. Biafra hawakutaka kujua nafasi yao ktk Muungano kuunda Nigeria, wao walitaka kujitenga kabisa na sio kuweka masharti ya ku share uongozi au kujitangaza kwamba wao ni nchi ndani ya Jamhuri kwani walikuwa nchi ndani ya Jamhuri!.

Kama Zanzibar wanataka kuuvunja Muungano kama wale Biafra waseme wazi! Nina hakika hakuna Mbara atakayewazuia isipokuwa tutakachowaomba ni utaratibu wa kisheria. Wapige kura za maoni kwa wananchi wao, wawaeleze hasara zitakazotokana na kuuvunja Muungano na kama wengi bado wataafiki na kura za ndiyo zikachukua ushindi bila shjaka tutavunja Muungano.

Lakini hatuwezi kuvumilia upuuzi huu unaotokea leo wa madai ya viongozi waliodandia Mapinduzi ambayo hawajui kwanza huu Muungano ulikuwa na maana gani kwa wananchi wake. Sijasikia kiongozi hata mmoja akizungumzia hizo kero za wananchi. mambo muhimu yanayowagusa Wazanzibar zaidi ya hii mipaka na kugawana vyeo hali pato la nchi nzima ya Zanzibar kwa mwaka halipishani na manispaa ya Ilala (Kariakoo).
 
M
Mimi nawaomba sana viongozi wa Zanzibar kama kweli wanasimamia mawazo ya wananchi wake waombe kuuvunja Muiungano kisha yatakayofuatia baada ya hapo wagawane madaraka wanavyopenda. .

Hii inaitwa hekima; kwa sababu wakishatoka kwenye muungano wataanza kudai nini? watakuwa wamepata wanachotaka au watarudi kwenye status quo ya 1963 baada ya Mwingireza kuondoka, serikali kuwa chini ya kina Shamte (na Sultani kama figure head) nakabla ya mapinduzi? Kwa sababu haijawahi kuwepo serikali ambayo imefanya kazi ya "nchi ya zAnzibar" ukiondoa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Kila kitu kina mwanzo wake, wakiondoka ndani ya Muungano wataunda seikali yao mpya wanavyopenda wao ili mradi wananchi wake wanaridhika. Lakini najua wazi yatafuata ya Comoro kwani hawa watu maswahiba wangu sana tu, ni wabishi sijapata kuona watatiana vidole vya macho wala haitachukua miaka mingi. Kisha Bara itapigiwa SOS..
 
Hivi kero za Muungano zinaonekana Zanzibar peke yake? Mbona hatuzungumzii kero wanazopata raia wa JMT ambao sio wenyeji wa Zanzibar? Mbona hatuzungumzii kero inazopata JMT kutokana na Muungano?

Amandla.......Kwa sababu kero zote zinatokana na VIONGOZI WENYEWE.. Hivyo viongozi kwa kuelewa hivyo wanasingizia mipaka, nchi na kadhalika kiasi kwamba imeonekana Wazanzibar ndio Wajanja kumbe wanachokifanya ni kuongeza hesabu ya watawala wala kodi zao..
 
Kila kitu kina mwanzo wake, wakiondoka ndani ya Muungano wataunda seikali yao mpya wanavyopenda wao ili mradi wananchi wake wanaridhika. Lakini najua wazi yatafuata ya Comoro kwani hawa watu maswahiba wangu sana tu, ni wabishi sijapata kuona watatiana vidole vya macho wala haitachukua miaka mingi. Kisha Bara itapigiwa SOS..
Wakiwa ndani ya MUUNGANO wanapiga kura kuunda serikali ya UMOJA wa KITAIFA. Nje ya Muungano mambo yatakuwa magumu zaidi. Kutakuwa na serikali ya SHIRIKISHO.
 
Ni makosa kudai kuwa kusema kuwa Zanzibar ni nchi bila kuweka wazi nchi ya pili ni ipi na maana ya hilo neno nchi. ......................... Kilichotakiwa kuwekwa wazi ni kuwa Zanzibar si nchi ndani ya JMT bali ni sehemu iliyopewa haki za pekee za kuwa na uongozi wake na utawala katika baadhi ya mambo. Wanachofanya wenzetu ni kujaribu kuweka neno sovereign kinyemela mbele ya state.

FM, hata katiba ya JMT haisemi wazi kwamba JMT in 'severeign' (labda pengine walikosa neno la kiswahili!)!

Kama kuna tatizo basi lipo kwenye structure ya muungano wenyewe. Ni vema kuzingatia kuwa Tanganyika na Zanzibar ziliungana kwa baadhi ya mambo tu('mambo ya muungano) na sio kwa kila kitu. Hivyo serikali ya JMT mamlaka yake yapo kwenye mambo yote yasiyo ya muungano ya iliyokuwa Tanganyika na yale ya muungano kwa pande zote mbili. Kwa mambo yasiyo ya muungano kwa Zanzibar,SMZ ndiyo yenye mamlaka.

Hivyo kimantiki, isipokuwa kwa mambo ya muungano Zanzibar 'haikumezwa' ndani ya JMT kama ilivyo kwa Tanganyika. Binafsi naona ipo hoja kwa Zanzibar kudefine mipaka yake ili kwa mambo yasiyokuwa ya muungano ijulikane mamlaka yake yanaishia wapi.
 
Mi nawapendeni kitu kimoja ndugu zangu wa Tanganyika (japo hampendi kuitwa hivyo lakini mkataa asili huwa mtumwa) yaani nyinyi maneno meeeeengi vitendo hamna kitu.

Hebu iangalieni nchi yenu, Tanganyika, inanajisiwa, inaporwa, inaliwa na wajanja hawazidi sita kwa hisabu ya vidole, inatawaliwa na failed party kwa miongo karibu minne...bado humo mna wasomi wa viwango vikubwa, mabingwa wa kusema, wadadisi...wapiga soga kama walivyo humu JF n.k ...hakuna lolote lililokuwa system ipo pale pale na bado inauhakika wa kushinda kwa kishindo.

Hii ni aibu kuwa nchi zote za Afrika Mashariki zimejaribu kubadili system mpaka Kenya juzi tu wamepata katiba mpya, Watanganyika bado mmekaa tu mmefunga mikono, eti ni wapenda amani na utulivu (upumbavu na uzembe) wa kuleta mabadiliko.

Nawashangaza mnain'gan'gania Zanzibar wakati ni wazi kuwa hiyooo inaondoka pendeni msipende...badala ya ku'ngan'gania watawala wenu wabovu waondoke kwa kushindwa kupunguza, (si kuondosha), ujinga, maradhi na umasikini kwa miaka 40 sasa...mnatazama macho na kupiga soga tu, maneno tele, no actions.

Wazanzibar waungwana, weshalia sana na adha za CCM na muungano, weshasema sana...hakuna lililokuwa na wameamuwa vitendo sasa. Eeee...! ada ya mja hunena muungwana ni vitendo! ndivyo tutakavyoendelea kufanya kuanzia sasa.

Nimesikia Chikawe,juzi alimuamuru AG wa Zanzibar(tuna AG Zanzibar, Mbeya hakuna), aje Dar afafanuwe kilichotokea...jibu alilolipata...kamwachia naibu mwanasheria mkuu,Masaju ajitowe kimaso maso..."you can't boss us anymore...yale ni maamuzi BLW, kama yalivyokuwa siku hizo...what 's new there".

Hebu soma maelezo yeke kwenye vyombo vya habari Chikawe hajuwi anasema nini..mimi sijamuelewa hasa!kadhalika na DAG wake.

Ndugu zangu Watanganyika nakuombeni, acheni maneno, acheni bwabwaja..haziwasaidii...mtabaki mnaburutwa na CCM maisha yenu...fanyeni kama walivyofanya Wazanzibar, Wakenya...vitendo..japo kama hamuwezi kudai Tanganyika yenu basi daini...heshima yenu kwa kuwaondoa madhalimu (CCM) madarakani, nitawaona mumefanya la maana sana kuliko hizi bwabwaja za kila siku humu, shauri yenu...si tushangóa nanga!
 
Junius,
Endeleeni hivohivo kufanya mabadiliko mnayoyahitaji kwenye KATIBA yenu. Ili mradi hamuigusi KATIBA ya JMT. Chochote mtakachofanya kinachopingana na KATIBA ya JMT kinakuwa BATILI tangu mwanzo.
 
Mi nawapendeni kitu kimoja ndugu zangu wa Tanganyika (japo hampendi kuitwa hivyo lakini kwa kua mimi si mtumwa huwa sikatai asili yangu na kwetu Zanzibar) yaani nyinyi maneno meeeeengi vitendo hamna kitu...hebu iangalieni nchi yenu, Tanganyika, inanajisiwa, inaporwa, inaliwa na wajanja hawazidi sita kwa hisabu ya vidole, inatawaliwa na failed party kwa miongo karibu minne...bado humo mna wasomi wa viwango vikubwa, mabingwa wa kusema, wadadisi...wapiga soga kama walivyo humu JF n.k ...hakuna lolote lililokuwa system ipo pale pale na bado inauhakika wa kushinda kwa kishindo

Wazanzibar waungwana, weshalia sana na adha za CCM na muungano, weshasema sana...hakuna lililokuwa na wameamuwa vitendo sasa. Eeee...! ada ya mja hunena muungwana ni vitendo! ndivyo tutakavyoendelea kufanya kuanzia sasa.

Hii dhana kuwa wengine ni watumwa na nyie ni waungwana ndiyo itawapeleka pabaya. Hata siku moja hamwezi kumheshimu yule ambae mnamhesabu kuwa ni mtumwa. Ndiyo maana wengine tunasema tuvunje Muungano, tuimarishe mipaka baina ya nchi zetu, halafu tuone itakavyokuwa. Kwangu mimi kumhesabu mtu mwenye mawazo kama yako kuwa ni raia mwenzangu inanitia kichechefu. Vunjeni muunganoo na as far as I am concerned "good riddance"!

Amandla.....
 
Mi nawapendeni kitu kimoja ndugu zangu wa Tanganyika (japo hampendi kuitwa hivyo lakini mkataa asili huwa mtumwa) yaani nyinyi maneno meeeeengi vitendo hamna kitu.

Hebu iangalieni nchi yenu, Tanganyika, inanajisiwa, inaporwa, inaliwa na wajanja hawazidi sita kwa hisabu ya vidole, inatawaliwa na failed party kwa miongo karibu minne...bado humo mna wasomi wa viwango vikubwa, mabingwa wa kusema, wadadisi...wapiga soga kama walivyo humu JF n.k ...hakuna lolote lililokuwa system ipo pale pale na bado inauhakika wa kushinda kwa kishindo.

Hii ni aibu kuwa nchi zote za Afrika Mashariki zimejaribu kubadili system mpaka Kenya juzi tu wamepata katiba mpya, Watanganyika bado mmekaa tu mmefunga mikono, eti ni wapenda amani na utulivu (upumbavu na uzembe) wa kuleta mabadiliko.

Nawashangaza mnain'gan'gania Zanzibar wakati ni wazi kuwa hiyooo inaondoka pendeni msipende...badala ya ku'ngan'gania watawala wenu wabovu waondoke kwa kushindwa kupunguza, (si kuondosha), ujinga, maradhi na umasikini kwa miaka 40 sasa...mnatazama macho na kupiga soga tu, maneno tele, no actions.

Wazanzibar waungwana, weshalia sana na adha za CCM na muungano, weshasema sana...hakuna lililokuwa na wameamuwa vitendo sasa. Eeee...! ada ya mja hunena muungwana ni vitendo! ndivyo tutakavyoendelea kufanya kuanzia sasa.

Nimesikia Chikawe,juzi alimuamuru AG wa Zanzibar(tuna AG Zanzibar, Mbeya hakuna), aje Dar afafanuwe kilichotokea...jibu alilolipata...kamwachia naibu mwanasheria mkuu,Masaju ajitowe kimaso maso..."you can't boss us anymore...yale ni maamuzi BLW, kama yalivyokuwa siku hizo...what 's new there".

Hebu soma maelezo yeke kwenye vyombo vya habari Chikawe hajuwi anasema nini..mimi sijamuelewa hasa!kadhalika na DAG wake.

Ndugu zangu Watanganyika nakuombeni, acheni maneno, acheni bwabwaja..haziwasaidii...mtabaki mnaburutwa na CCM maisha yenu...fanyeni kama walivyofanya Wazanzibar, Wakenya...vitendo..japo kama hamuwezi kudai Tanganyika yenu basi daini...heshima yenu kwa kuwaondoa madhalimu (CCM) madarakani, nitawaona mumefanya la maana sana kuliko hizi bwabwaja za kila siku humu, shauri yenu...si tushangóa nanga!

Waarabu wamerudi Zenj kwa mlango wa nyuma,imewachukua miaka karibu 50 kwa mipango yao kufanikiwa.Tuhesabu miaka mingine miwili au mitau kabla Upemba na Uuunguja haujawasmbaratisha waungwana hawa.
 
Mwanakijiji umeshawahi kupitia web ya mzalendo.net?, kama bado hebu jaribu kuingia huko uone kinachoendelea. Wamekopi thread yako hii na inachambuliwa huko, eeh, hivi kumbe wenzetu wamefikia hatua hii!. Usoni tu ndugu rohoni wanaumia!
 
Mwana kijiji ndio nani ?jamaa anauka Uongo amekuwa na wafuwasi wake hapa analolisema hawakawii kutowa asante leo hii anajifanya profisa mchundo na kutafsi katiba ambayo haijuwi nini kimo ndani yake ,binafsi ningemuomba arudi tena na akufahamisheni jee alikosea katika kutowa tasmini zake au ndio miongoni mwaprofisa wa Jf hutafuta wale wasiokuwa na mbele wala nyuma na kuwahada kuwa wao wanaelewa ukweli wa Mungano ( unapoambiwa ujiambie )
 
Mkuu,
Taratibu basi bila jazba, hebu rudia kusoma ulichoandika uone kama ndivyo ulivyokusudia kuufikisha ujumbe. Ujumbe haueleweki, au ndivyo ulivyokusudia?
 
Ukiona mama au baba analala chumba kingine kwa kisingizio kwamba mtoto mchanga analia sana usiku ujue ndio mwanzo wa kuvunjika ndoa. Mtikila akimaliza harakati za uchaguzi mkuu atakwanda mahakamani kudai nchi inayoitwa "Tanganyika" ambao by implication imeshakuwepo kwa kuwepo nchi inaitwa "Zanzibar". Talk about the chicken coming home to roost!
 
Mwana kijiji ndio nani ?jamaa anauka Uongo amekuwa na wafuwasi wake hapa analolisema hawakawii kutowa asante leo hii anajifanya profisa mchundo na kutafsi katiba ambayo haijuwi nini kimo ndani yake ,binafsi ningemuomba arudi tena na akufahamisheni jee alikosea katika kutowa tasmini zake au ndio miongoni mwaprofisa wa Jf hutafuta wale wasiokuwa na mbele wala nyuma na kuwahada kuwa wao wanaelewa ukweli wa Mungano ( unapoambiwa ujiambie )

Watu wanaomwonea kijicho Mzee Mwanakijiji nawashangaa. Unaongelea asante anazopewa bila kuangalia anazotoa! Yeye karibu wote wanaochangia thread zake anawashukuru hata kama wanatofautiana nae. Amepewa Thanks karibu 8000 wakati yeye amezimwaga karibu 13,000!v Humu ndani kuna watu wenye mamia ya thanks lakini wenyewe aghalabu kushukuru.

Huyu jamaa pamoja na kuwa anapewa sapoti kubwa sana lakini vile hupingwa sana. Tofauti na wengi wetu sijaona dalili ya kinyongo kutoka kwake. Yeye bado anaendelea kutoa mchango wake, ukubalike au usikubalike. Badala ya kumvisha vilemba vya ukoka vya uprofisa mchundo bora ungemfahamisha wapi amekosea. Au na wewe unamuogopa?

Amandla..........
 
Viongozi wa Zanzibar wanataka madaraka zaidi na kwa bahati mbaya hakuna sehemu kubwa ya kuchukua madaraka hayo isipokuwa sehemu ndogo ya wananchi wa visiwa vya Zanzibar. Hivyo kinachofanyika ni kuunda serikali kubwa yenye ulaji kwa kila mtu wakisingizia mipaka ya Zanzibar na kadhalika. Wananchi wanafurahia kutia changa la macho mchana kweupeee. My take: makamu wawili wa rais!!
Mimi nawaomba sana viongozi wa Zanzibar kama kweli wanasimamia mawazo ya wananchi wake waombe kuuvunja Muiungano kisha yatakayofuatia baada ya hapo wagawane madaraka wanavyopenda. Lakini hawawezi kutumia nafasi ya Muungano kuleta madai kama vile mtu asiyeridhika ndani ya ndoa lakini hataki kuomba talaka isipokuwa kila siku kuongeza madai ili mradi kumuudhi mwenza wake akiwa ndani ya ndoa.

Zanzibar hawajawahi kusema wanataka kuuvunja Muungano na Bara ikawakatalia kama wailivyokuwa Nigeria. Biafra hawakutaka kujua nafasi yao ktk Muungano kuunda Nigeria, wao walitaka kujitenga kabisa na sio kuweka masharti ya ku share uongozi au kujitangaza kwamba wao ni nchi ndani ya Jamhuri kwani walikuwa nchi ndani ya Jamhuri!.

Kama Zanzibar wanataka kuuvunja Muungano kama wale Biafra waseme wazi! Nina hakika hakuna Mbara atakayewazuia isipokuwa tutakachowaomba ni utaratibu wa kisheria. Wapige kura za maoni kwa wananchi wao, wawaeleze hasara zitakazotokana na kuuvunja Muungano na kama wengi bado wataafiki na kura za ndiyo zikachukua ushindi bila shjaka tutavunja Muungano.

Lakini hatuwezi kuvumilia upuuzi huu unaotokea leo wa madai ya viongozi waliodandia Mapinduzi ambayo hawajui kwanza huu Muungano ulikuwa na maana gani kwa wananchi wake. Sijasikia kiongozi hata mmoja akizungumzia hizo kero za wananchi. mambo muhimu yanayowagusa Wazanzibar zaidi ya hii mipaka na kugawana vyeo hali pato la nchi nzima ya Zanzibar kwa mwaka halipishani na manispaa ya Ilala (Kariakoo).

Mkuu, kula tano kwanza halafu popote ulipo pata kikombe cha chai, mimi ninapata sasa hivi kwa heshima yako.
 
Back
Top Bottom