Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,999
- 1,187
Wanalazimisha jungu likubalikeHii habari tumeshaijadili hapa sana, mpaka Sitta akasimama bungeni kukanusha....sasa wewe sijui umeileta kwa mantic gani hapa!
Wanalazimisha jungu likubalikeHii habari tumeshaijadili hapa sana, mpaka Sitta akasimama bungeni kukanusha....sasa wewe sijui umeileta kwa mantic gani hapa!
Upuuzi mtupu, MOD tuondolee hii kitu hapa, majungu pelekeni kwenye vikao vya mafisadi
nadhani hamjui juu ya hayo myasemayo, kuna mamlaka zinazo husika kuidhinisha hizo pesa na kama ni kweli hao ndio wezi na so spika, acheni kupika majungu, leteni ushahidi ; kwangu hizo ni porojop tu,
Mtui nakuunga mkono kwamba haya tunayosuhudia hapa ni majungu. Mwandishi hajafanya uchambuzi wa kutosha kubainisha mtiririko wa matukio. Na kubwa zaidi, ufisadi unaotaka kuanikwa hapa mbona ni kiwango kidogo sana ukilinganisha na EPA, Richmond, Kagoda, Kiwira etc.. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!!!
Ni kiwango kipi cha ufisadi tunapaswa kuvumilia?Nikidhani kuwa hakuna ufisadi mdogo wala mkubwa.... wote ni mbaya tu na unapaswa kupigwa vita.
Nami naunga mkono ni majungu tu haya tumeshasikia sana juu ya hili na nafikiri we are fed up with stories without any direction. we need to discuss serious issues sio majungu tu ya watu hapa. I said yesterday that some contributors in this forum are not to be trusted and they are biased towards certain groups in the ruling party.
mimi najua Bwana bwassa anatumikia kina nani? anaangalia gharama za kujenga au ku furnish nyumba ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano??/ je alikuwa na mpangpo wa kujiuzia nyumba hiyo kama alivyofanya yule ndugu yangu wa Umeme pale ubungo? au alikuwa anataka kuibinafsisha kama Rais mstaafu alivyofanya Kiwira na nyumba kadha za Serikali? Bwassa acha hizo labda useme wewe umenunuliwa kwa shilingi ngapi tu. Mkapa alitumia fedha nyingi kukarabati Ikulu wala hatukusema maana aliimwachia mwenzie wala hakuichukua, hivyo hivyo hakuna tatizo kubwa kwa bwana six kukarabati nyumba ya spika. uspika wenyewe unaisha mwakani, na washirika wa bwassa mmepania kutokumrudisha bungeni na uspika atausikia kwenye bomba tu.Wakuu,
Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu kwa makini, lakini ukweli ni kwamba ufisadi ni ufisadi tu, hauna udogo! Msisahau pia nyumba ambayo Spika Sitta, tumeambiwa, amepangiwa ya USD 8,000 (TSh. Milioni 10) za walipa kodi kwa mwezi na kuipuuza nyumba yake aliyopewa zamani, akisema siyo hadhi yake; samani za Tsh. Milioni 250 kwa hiyo nyumba mpya ya kupanga; gari la kifahari analolitaka la aina ya Mercedes Benz la TSh. Milioni 300 linalonunuliwa na Ofisi ya Bunge na kuliona la sasa halifai! Hoja hizi Spika alishindwa kuzijibu Bungeni na badala yake akaomba ulinzi wa askari zaidi wa usalama, vimulimuli na mapikipiki, kama vile yeye ni Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu!
LAKINI tatizo la mzee huyu la fitina na usaliti wa kisiasa, halikuanza leo! Katika miaka ya mwanzoni ya 1990, akiwa Waziri wa Sheria (na baadaye akaondolewa, baada ya kushindwa Ubunge wa Urambo), alishiriki "kiujanjaujanja" katika hoja ya kutaka kuleta Serikali ya Tanganyika katika mfumo wa Muungano, ili uwe wa Serikali Tatu badala ya Mbili.
Katika kitabu chake, UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA. Uk. wa 20 hadi Uk. 27, Mwalimu Nyerere alimsema vibaya sana Sitta, kwa kupeleka mbele ya Halmashauri Kuu ya CCM, Dodoma, "TAARIFA YA SERIKALI JUU YA AZIMIO LA BUNGE KUHUSU HAJA YA KUUNDA SERIKALI YA TANGANYIKA NDANI YA MUUNDO WA MUUNGANO". Mwalimu Nyerere alisema, kuhusu taarifa hiyo, katika kijitabu hicho: "Taarifa yenyewe ni ndefu, maana ina maelezo mengi ya mapambo tu, au ya kiinimacho(Uk. 20)...Baadaye, baada ya kikao, nilimtafuta Ndugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki (Uk. 27)...". Huyo ndiyo Spika Sitta, mbele ya macho na fikra za Mwalimu Nyerere! Hivi ni mpiganaji kweli wa vita dhidi ya "Ufisadi", au ni msaliti tu wa Chama chake? Wana-CCM na msio wana-CCM na ni Watanzania tu wenye nia njema, pimeni!
Bwassa
Ama kweli, ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni! Kama unadhani vigogo wa EPA ni mafisadi peke yao, basi ulikuwa hujamfahamu Spika wa Bunge SAMUEL JOHN TEGEZA SITTA ! Ukimsikiliza anapoongea unaweza kuamini kwamba kiongozi huyo wa Bunge ni msafi kutokana na umahiri wake wa kujivalisha sifa kemkem Mr Misifa. Unakumbuka hivi karibuni alivyomtukana Naibu Spika eti hawezi kusimamia mambo nyeti mpaka awepo yeye mwenye Bunge? ! Kisa nini? Kupenda sifa na kumdhalilisha mwenzake mbele ya umma, halafu bado anaendelea kuliita Bunge eti ni chombo cha kidemokrasia!
Tumebaini kwamba Sitta amekuwa akijimiminia sifa nyingi ili kulinda ufisadi anaoufanya usigundulike katika jamii yetu. Ngoja nikupe tone tu la madhambi yake kwa umma ili uone ni hatua gani utachukua, na ili na yeye ajipime kwa nafasi yake. Angalia uchafu huu:-
- Anatumia vibaya fedha za umma. Amekuwa akitumia msaidizi wake kuchota mapesa kwa kisingizio kuwa ni masurufu ya safari za ndani na nje ya nchi. Kila safari ya siku moja ndani ya nchi huchukua shilingi Milioni tano (5,000,000/=), na kila safari ya siku moja nje ya nchi huchukua shilingi Milioni Kumi na Tano (15,000,0000/=). Ameshindwa kufanya marejesho ya masurufu (imprest) hayo, licha ya kupeleka risiti kadhaa za kughushi/za uongo kwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Bunge. Mpaka sasa anadaiwa jumla ya shilingi Milioni sitini (60,000,000/=) za masurufu.
- SITTA hupeleka risiti za uongo kwa Mhasibu Mkuu, zikionesha madai kutoka Oysterbay Pharmacy ya Shilingi Milioni Mbili ( 2,000,000/= ) aliyotumia kwa tiba kila wiki.
- Amekuwa akilazimisha hawara yake wa Hospitali ya Aga Khan naye alipwe posho kama wabunge anapokwenda naye Dodoma. Kwa mfano, hawara huyo alilipwa per diem kuanzia tarehe 13/12/2007 hadi tarehe 31/01/2008 ( Siku 50). Huo ni Ufisadi mkubwa!
- Anaye kimada wake mwingine anayekwenda kwa jina la ASIA ambaye anaishi nyumba Na. 111 karibu na Mahakama ya Ardhi Upanga na amezaa naye. Huko mtaani kwao kimada huyo hujiita mama SITTA, na ni dada yake aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa iliyokuwa Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC). Mwanamke huyo muda wote hutumia gari la Ofisi ya Bunge STK 232 Toyota RAV 4.
- Pia anaye kimada mwingine (jina limehifadhiwa) ambaye anaishi kinondoni ( Livingstone), mtaa wa Honolulu katika nyumba ya kupanga inayomilikiwa na dada yake Kawawa. Nyumba hiyo inatazamana na Nyumba Na. KH.MK/No. 337 katika mtaa huo huo. Kimada huyo hutumia gari ya kiofisi ya Spika mwenyewe STK 3002.
- Vimada wote hao hupata huduma za maji na umeme kwa gharama za Ofisi ya Bunge. Kuna kipindi mke halali wa Spika, aliwahi kulalamikia hali hiyo. Kuna siku maji yalikatika nyumbani, mke wa Spika akaomba apelekewe bowser la maji na Ofisi ya Bunge. Ohooo! Watekelezaji wakapeleka maji kimakosa kwa kimada. Mama Sitta akashtukia dili.
- Kuna taarifa kwamba mnamo Mwezi Oktoba 2007, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iligundua mapungufu makubwa katika matumizi ya fedha yaliyofanywa na Spika SITTA. nimedokezwa kuwa Spika aliwanyamazisha wajumbe wa kamati hiyo, ambapo aliwatishia kutowapatia posho na safari za nje kama wangeyafumua mapungufu yake hadharani! Hapo inaonesha kuwa wajumbe hao walipewa rushwa!!
- Kama JK anataka viongozi wa kisiasa na wa serikali watenganishe biashara na uongozi wa ku sacrifice kimojawapo, hilo litakuwa gumu kwa sababu Sitta alipokuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha cha Uwekezaji nchini (TIC) alitumia nafasi hiyo kuingia ubia na wafanyabiashara wengi wa Kigeni. Je, Wizara ya Maliasili na Utalii inatambua kuwa Spika ana hisa kwenye kampuni moja ya Kichina inayosafirisha nagogo licha ya marufuku yaliyowekwa?!
- Nililokupa hapo ni tone tu.
mimi najua Bwana bwassa anatumikia kina nani? anaangalia gharama za kujenga au ku furnish nyumba ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano??/ je alikuwa na mpangpo wa kujiuzia nyumba hiyo kama alivyofanya yule ndugu yangu wa Umeme pale ubungo? au alikuwa anataka kuibinafsisha kama Rais mstaafu alivyofanya Kiwira na nyumba kadha za Serikali? Bwassa acha hizo labda useme wewe umenunuliwa kwa shilingi ngapi tu. Mkapa alitumia fedha nyingi kukarabati Ikulu wala hatukusema maana aliimwachia mwenzie wala hakuichukua, hivyo hivyo hakuna tatizo kubwa kwa bwana six kukarabati nyumba ya spika. uspika wenyewe unaisha mwakani, na washirika wa bwassa mmepania kutokumrudisha bungeni na uspika atausikia kwenye bomba tu.