Kitendo kilichofanyika ni cha busara,kubali ukatae Kanumba amewasaidia kwa njia moja ama nyingine vijana wengi kujiajiri kwa sababu ya kazi zake na pia amelitangaza soko la nchi yetu(la filamu) kwa kiasi kikubwa.usiwe mtu wa kupinga tu mambo ndugu yangu kama kusoma huwezi hata picha huoni,hawezi kuwa kama wewe kiukweli vinhinevyo uniambie ni nin ulishafanya kwa nchi yako chenye manufaa kimataifa
Sitaki kupuuzia mchango wa Kanumba katika sanaa yake (sanaa na si lazima taifa kwa ujumla). Ila linapo kuja swala la kodi tutambue kwamba kodi ni kwa manufaa ya wananchi wote. Kwa maana si kila huduma lazima imfaidishe kila mtu ila iwe na manufaa kwa taifa. Kwa maana nadhani tuna changanya umaarufu na mchango kwa taifa.
Linapo kuja swala la Kanumba si kwamba pesa zinge kosekana za kuendesha msiba wake. Wasanii wenyewe, ndugu, jamaa na marafiki wange weza pata pesa za kutosha kuendesha shughuli. Kwa hiyo si kwamba serikali imesaidia katika jambo ambalo otherwise linge kwama.
Pia kuna watu kibao ambao wana hitaji pesa kama hizo. Kuna watu hawana chakula, malazi, pesa za ada. Kweli waliona matumizi ya dharura ni kwenye msiba huu?
Piakuna member mmoja kwenye hii thread kasema kitu cha maana sana. Kwamba kuna precedence zingine tuna tengeneza zita leta matatizo. Sasa ina maana serikali itakua ina gharamia misiba yote ya namna hii? Wakifa wasanii wengine wenye kutoa mchango sawa sawa na Kanumba zita tumika pesa za serikali?
Mimi nadhani serikali imetumia ishu hii kisiasa sana. Sikuona haja ya JK kuahirisha safari kwende kuhudhuria msiba wa mtu mmoja wakati haku ahirisha safari wakati wa mgomo wa madaktari walipo kufa mamia ya watanzania. Pia sikuona haja ya viongozi wa kiserikali kujazana pale leaders club.
Anyway najua kuna wengine wata nipinga. Haya ni maoni yangu tu.
kumlinganisha kanumba na hao mabilionea ni sawa na kulinganisha sisimizi na tembo. hao hawakuhitaji msaada wa serikali yao. kanumba was a pioneer, but relatively poor. he deserved what was offered.Jamani mbona sijajibiwa swali langu?nauliza tena. Serikali ya marekani ilitoa sh.ngapi Michael Jackson au whitney houston walipokufa?
Kitendo kilichofanyika ni cha busara,kubali ukatae Kanumba amewasaidia kwa njia moja ama nyingine vijana wengi kujiajiri kwa sababu ya kazi zake na pia amelitangaza soko la nchi yetu(la filamu) kwa kiasi kikubwa.usiwe mtu wa kupinga tu mambo ndugu yangu kama kusoma huwezi hata picha huoni,hawezi kuwa kama wewe kiukweli vinhinevyo uniambie ni nin ulishafanya kwa nchi yako chenye manufaa kimataifa
Ukisikia wizara itatoa jua hapo hakuna ubinafsi! Wazazi wapewe pesa hizo na serikali; za nini? watanzania wangapi wanafiwa tena na watu wanaowategemea lakini serikali haiwasaidii. Ningeielewa serikali kama ingesema itasimamia kuhakikisha wazazi wake wanapata haki kutokana na mikataba yake na kazi zake.Nimehuzunika sana na kifo cha mpendwa wetu na kijana mwenzangu Steve Kanumba.BUT kunakitu hakijaniingia akilini pale waziri wa vijana na utamaduni alipotangaza kwamba wizara yake itatoa sh.milioni 15 kwa familia ya kanumba,nilimshuudia kwa macho yangu kupitia tv.Then nilisoma gazeti la mtanzania nikakutana na habari inayosma 'serikali itagharamia mazishi yote ya kanumba.'.nauliza je hii bajeti hiyo inatolewa kwenye fungu gani la bajeti ya serikali ukizingatia Kanumba ni raia wa kawaida kama mimi ? Na je huyo waziri alitoa rambirambi yake binafsi?
Hatuna vipaumbele basi. Kila kitu ni siasa.Vijana wa siku hizi bana.....
Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kushabikia serikali kutoa 15m kwa mbakaji wa watoto kisa tu eti ni maarufu? Wizara hiyo hiyo imeitelekeza timu ya taifa ya netball na kumchoresha mke wa Pinda kutembeza bakuli la ombaomba kuinusuru timu.....
Kwamba unaweza shabikia mama wa mhuni apewe 15m za kodi yetu wakati mama zetu wanatembea zaidi ya 10km kwenda kutafuta maji machafu vijijini huko?
Nalishangaa sana taifa langu hili....
Serikali legelege utaijua kwa matendo yake.
kumlinganisha kanumba na hao mabilionea ni sawa na kulinganisha sisimizi na tembo. hao hawakuhitaji msaada wa serikali yao. kanumba was a pioneer, but relatively poor. he deserved what was offered.
Yapi? Huo uzinzi na ulevi wake?Kanumba? Aaah' acha aende kijana wetu,ameifanyia makubwa sana nchi yetu!
kuna watu wanashabikia mambo ya kijinga ambayo yameanzia kwa jk nao wanayakubali. Hivi hii si ndo wizara ilifukuzwa nhc kwa kutolipa kodi? Ukienda dawasco na tanesco hawa ni wadaiwa sugu. Leo mnaniambia kuchezea kodi zetu kwa mambo ya mazisho ya mtu asiye na mchango wa kitaifa ni halali! Tusiwe wavivu wa kufikiri kiasi hicho, hivi huo ujinga wanaoufanya unatuingizia dola ngapi kwa mwaka? Serikali nzima imehamia kwenye msiba wa watu waliouana wakizini, na vyombo vya habari vingine hata wakati wa ajali ya meli hawakutangaza lakini leo wamepata airtime? Hawa viongozi mi najiuliza kwenye bajeti walizomia wameandika nini? Ni emergence ngapi za kitaifa zinatokea tunaambiwa hakuna hela? Hospitali ngapi leo hazina ultrasound,dawa,? Rais,makamu,pm,mawaziri vichwa vyao wote vimeoza. Wameshindwa kuwaletea wananchi maendeleo wameamua wawe wanawalisha wali kwenye misiba? Au ndo mwendelezo wa majibu mepesi kwenye maswali magumu? Ndo yale ya tacaids kutaka kodi za vinywaji zipande ili wao wapate za kununulia v8 na kusomesha watoto wao nje huku waathirika wakihangaika na lishe na complications za dawa?Tuacheni kutetea upumbavu,fedha zetu nyingi zimetumika pasipo kufuata matumizi yanayoeleweka. Fedha zenyewe za mkopo bado tunafanyia ujinga. Naomba wafadhili waendelee kujitoa ili tupate akili. Narudia HUU NI UPUNGUANI WA WALE WOTE WALIOTUMIA KODI ZETU KWENYE HUU MSIBA!.