Ni sawa wizara kutumia kodi ya wananchi kutumika kwenye mazishi ya Kanumba?

Nakubaliana na wewe kwa asilimia nyingi tu mkuu...kwanza tanzania hakuna filamu kuna maigizo
 
Ndugu zangu punguzeni asira, Msimtukane sana marehemu kwa makosa yake lakini kumbukeni ni watu wengi sana wanafanya mambo kama haya ila hayajulikani nahisi hata baadh ya watukanaji hapa ni wasinz tena wakutupwa kwani kumbukeni tu kwamba hakuna binadamu aliekamilika.Marehemu Kanumba alikuwa ni kipenzi cha watu hilo hakuna wakukataa lakini kitendo cha serikali ya wananchi maskini kama TZ kuchangia sh 15m hiyo ni dalili ya kuonesha kwamba hatuna viongoz wenye nia njema na nchi yetu kwa 7bu kikatiba huyu ni r
 
Vijana wa siku hizi bana.....

Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kushabikia serikali kutoa 15m kwa mbakaji wa watoto kisa tu eti ni maarufu? Wizara hiyo hiyo imeitelekeza timu ya taifa ya netball na kumchoresha mke wa Pinda kutembeza bakuli la ombaomba kuinusuru timu.....

Kwamba unaweza shabikia mama wa mhuni apewe 15m za kodi yetu wakati mama zetu wanatembea zaidi ya 10km kwenda kutafuta maji machafu vijijini huko?

Nalishangaa sana taifa langu hili....
Serikali legelege utaijua kwa matendo yake.

Hao wanaosapoti wengi hawajui matumizi ya hela tunazolipa kama kodi.

Hiyo chapaa inaweza kununua madawati 500, ambapo wanafunzi 1500 wangeacha kukalia mawe. Yangetosha madarasa 11 yenye wanafunzi 45 kila moja!

Wakati Nchimbi akiwa msibani anamwaga hayo mahela, Mwanry amemsaidia kujibu swali la wizara yake kwamba serikali haina hela na inaisaidia tbc kuweza kukopa hela za maintenance maana hawana hata za kureplace camera!

Chakujiuliza hapa ni money allocation and priority na umuhimu wake. Umaarufu wa Kanumba unaishia kwenye luninga ambazo ni watz wachache wanaozimiliki. Vijijini ambapo wengi tunafahamu kwamba ndio kuna idadi kubwa ya watu, hakuna kabisa umeme! Halafu watu hapa wanatetea matumizi ya hovyo kabisa ya kodi zao kwa reason ya umaarufu. Tunatakiwa kufikiria Tz zaidi ya Dar! Maisha ya watz wengi ni ya chini sana na hawapo dar. Kwahiyo tunapoijadili tz tuitazame kwa upana wake na sio kuishia mbezi mwisho.

Kijiji cha Motta, tarafa ya Kibakwe, jimbo la Kibakwe, wilaya ya Mpwapwa sio tu hakuna umeme bali hata gari halifiki! Hizo foleni huko dar wakiziona wanaweza kudhani ni nyoka!

Binafsi naona serikali haijafanya sawa na ni fikra finyu za viongozi wetu, ufupi wa mawazo kwa wenzetu na maamuzi ya kipuuzi kabisa!
 
Kitendo kilichofanyika ni cha busara,kubali ukatae Kanumba amewasaidia kwa njia moja ama nyingine vijana wengi kujiajiri kwa sababu ya kazi zake na pia amelitangaza soko la nchi yetu(la filamu) kwa kiasi kikubwa.usiwe mtu wa kupinga tu mambo ndugu yangu kama kusoma huwezi hata picha huoni,hawezi kuwa kama wewe kiukweli vinhinevyo uniambie ni nin ulishafanya kwa nchi yako chenye manufaa kimataifa

Ama kweli kuna watu wanaingia humu kupinga kila kitu. Kazi aliyoifanya Kanumba ni kubwa sana na atabaki kwenye kumbukumbu za walio wengi. R.I.P Kanumba.
 
Tuache kuwa EMOTIONAL DRIVEN kama wanawake, serikali IMEKOSEA. Kanumba was just an individual na alichofanya si jambo linalokubalika na kila mtu.
1. The so called FILAMU kwa sasa imekuwa ndio kitovu cha uhuni na uasherati mkubwa kama huu uliopelekea kifo chake (Sipongezi, zinaharibu akili zenu)
2. Huyu anayesema msiba wa Kanumba umewagusa wengi, hicho si kigezo. Magazeti ya SHIGONGO yanasomwa na karibu wanawake wooote waliofeli form 4 na wasio na mwelekeo, je hicho ni kigezo kuwa UWAZI na IJUMAA ndio magazeti bora hapa Tanzania? (Lipime wewe mwenyewe kama una akili timamu)
3. Allocation ya fedha za serikali ina taratibu zake. Ikiwa leo kafa Kanumba 15m, kesho (kwa mfano, Mwenyezi Mungu aepushie mbali) akafa Juma Kaseja, serikali isipotoa 15m tutawaelewa?

Nionavyo mimi: Kuwa msanii hakumlazimishi mtu awe MUHUNI. Ukisoma headlines za magazetu yenu haya ya UDAKU utaona jinsi yalivyopambwa na habari za Fulani na Fulani wamelala chumba kimoja Nairobi, Uwoya kafumaniwa na mume wa mtu, Sijui nani kabakwa, yaani ni full upuuzi. Ikiwa haya ndio mnayoyaita maendeleo leo hii tukiwa wabovu kiuchumi kama nchi, basi tuna safari ndefu.

Wasanii wafanye sanaa na sio uhuni. Umaarufu kunuka huo mnaojivunia kwa kuwa nje ya nyumba za baba zenu saa 8 usiku ndio matokeo yake haya. Mtoto wa miaka 18 ana mabwana 6 hadi anawaua wengine kwa presha halafu mniambie mimi nikiwa na akili zangu timamu bila pombe, ETI HAYO NI MAFANIKIO KWA TANZANIA, nyooo! Kwendeni zenu huko

Aisee! Umenena mkuu, umenena vyema. Umenena ukweli kabisa. Watu wanajisahau sana na kujikuta wakithamini hata upuzi. Wasanii wetu hawa wanaoonekana wa maana wanaifundisha nini jamii yetu kama siyo kuipotosha. Jamaa angekuwa makini kukahimiza katoto kale kaende shule badala ya kukimbizana nako chumbani kwa ajili ya wivu. Hapo tungeuona mchango wake. Naamini kabisa Kaseja ana mchango mkubwa kwa taifa kuliko Kanumba.
 
Nimehuzunika sana na kifo cha mpendwa wetu na kijana mwenzangu Steve Kanumba.BUT kunakitu hakijaniingia akilini pale waziri wa vijana na utamaduni alipotangaza kwamba wizara yake itatoa sh.milioni 15 kwa familia ya kanumba,nilimshuudia kwa macho yangu kupitia tv.Then nilisoma gazeti la mtanzania nikakutana na habari inayosma 'serikali itagharamia mazishi yote ya kanumba.'.nauliza je hii bajeti hiyo inatolewa kwenye fungu gani la bajeti ya serikali ukizingatia Kanumba ni raia wa kawaida kama mimi ? Na je huyo waziri alitoa rambirambi yake binafsi?

Hii nchi unafikiri tuna viongozi wanaofikiri,nchi maskini alafu ina entertain mambo ya kij***a,yaani mawazo ya kiongozi mmoja tu ndio yanafanywa na kulazimishwa kua ni mawazo ya taifa zima,na viongozi walio chini yake lazima wafanye maamuzi ya kujikomba ili kumridhisha mkulu
 
Kwa hiyo hata kubaka vibinti vidogo ni kuitangaza vema nchi yetu? Acheni hizo sio wivu ila ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Wamekufa wangapi waliofanya mazuri kwa nchi hii mbona hawajatendewa hivi? Au mnataka kutuambia kuwa ukiondoa baba wa Taifa anaefuata ni Kanumba?

Kanumba alimbaka nani? Yule binti alikuwa anajitangaza kila siku kwenye magazeti kwamba yeye si mtoto ni mtu mzima, Sheria pia inaruhusu binti wa miaka 14 kuolewa.

Kanumba ni zaidi ya wanasiasa wa nchi hii, umeona ule umati, kwa hakika umefuatia kwenye umati wa baba wa taifa.

Kubali ukatae, alistahili kuzikwa na serikali. Hiyo serikali inatumia mamilioni mangapi kwenye shughuli zisizo na tija kwa nchi hii?
RIP Kanumba
 
mama yake mzazi alisema jana kuwa mwanae amezaliwa mwaka 1995. Alikuwa akihojiwa na sauti ya Amerika (voa)

Huyo mama yake nae hajatulia, amejua lini kuwa mtoto wake kazaliwa 1995? Mtoto mwenyewe alishawahi kuhojiwa kwenye vyombo vingi vya habari ikiwemo kipindi cha Mkasi akasema yeye ni mtu mzima ana miaka 18. Leo mama anataka kuvuna mchicha kwenye shamba la bangi?
 
Kwa hiyo hata kubaka vibinti vidogo ni kuitangaza vema nchi yetu? Acheni hizo sio wivu ila ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Wamekufa wangapi waliofanya mazuri kwa nchi hii mbona hawajatendewa hivi? Au mnataka kutuambia kuwa ukiondoa baba wa Taifa anaefuata ni Kanumba?

Mkuu Kanumba was not an angel but he was not a devil either. Kwa mazuri yake, taifa limejulikana Dunia nzima. Hakuna asiye na mapungufu lakini heshima yake haipotei kwa mema aliyoyatendea Taifa.
Acha wivu mkuu hata vidole havilingani japo vipo kwenye mkono mmoja
 
Kwa hiyo hata kubaka vibinti vidogo ni kuitangaza vema nchi yetu? Acheni hizo sio wivu ila ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Wamekufa wangapi waliofanya mazuri kwa nchi hii mbona hawajatendewa hivi? Au mnataka kutuambia kuwa ukiondoa baba wa Taifa anaefuata ni Kanumba?

Amembaka nani yako? Ulishuhudia wakati anabakwa? Kumbe wapo wanaume wambea na wazushi kama wewe!!! Acha kumnena vibaya marehemu.
 
Nimehuzunika sana na kifo cha mpendwa wetu na kijana mwenzangu Steve Kanumba.BUT kunakitu hakijaniingia akilini pale waziri wa vijana na utamaduni alipotangaza kwamba wizara yake itatoa sh.milioni 15 kwa familia ya kanumba,nilimshuudia kwa macho yangu kupitia tv.Then nilisoma gazeti la mtanzania nikakutana na habari inayosma 'serikali itagharamia mazishi yote ya kanumba.'.nauliza je hii bajeti hiyo inatolewa kwenye fungu gani la bajeti ya serikali ukizingatia Kanumba ni raia wa kawaida kama mimi ? Na je huyo waziri alitoa rambirambi yake binafsi?

Kanumba alikuwa ni nembo ya taifa (Nation Icon) kwa sanaa za maigizo na filamu hivyo kumzika kwa fedha za umma sijaona tatizo.

kazi ya kanumba imeitangaza Tanzania kuliko fedha zitakazotumika kumzika ...kuanzia kwenye kodi ya kazi yake, ajira kwa vijana na kuifanya Tanzania ikajulikana kwa baadhi ya wageni kupitia kazi yake, nenda Kongo Brazaville, Kenya, Sudan , Ghana, Nigeria rudi hadi Kongo Kinshasa kanumba aliifikisha Tanzania huko kupitia sanaa.

Kazi ya kanumba iliburudisha na kuifunza jamii.
 
Tatizo liko kwenye mfumo mzima wa serikali yetu, usimamizi mbaya wa pesa za wananchi ndo ulotufikisha hapa leo. Hasa maadili ya uongozi, heshima ya viongozi wetu. Hata rais anaonekana hana heshima yake mpaka anawekwa kwenye matangazo ya biashara radioni(eti dunia yako)? Hata kama Kanumba angekua maarufu kiasi gani, serikali haikupaswa kufanya upumbavu kama huo. Nadhani ni kutapatapa kwa ccm na ndo mwisho wake, inajaribu kufurukuta kwa kila tukio hata panya akifa ni inshu kwao, tutaona mengi! kwani vifo hav
 
Ama kweli kuna watu wanaingia humu kupinga kila kitu. Kazi aliyoifanya Kanumba ni kubwa sana na atabaki kwenye kumbukumbu za walio wengi. R.I.P Kanumba.

Tunapinga matumIzi holela! SK ni marehemu hizo mil 15 zingenunulia dawa tungeokoa maisha zaidi
 
Kanumba alikuwa ni nembo ya taifa (Nation Icon) kwa sanaa za maigizo na filamu hivyo kumzika kwa fedha za umma sijaona tatizo.

kazi ya kanumba imeitangaza Tanzania kuliko fedha zitakazotumika kumzika ...kuanzia kwenye kodi ya kazi yake, ajira kwa vijana na kuifanya Tanzania ikajulikana kwa baadhi ya wageni kupitia kazi yake, nenda Kongo Brazaville, Kenya, Sudan , Ghana, Nigeria rudi hadi Kongo Kinshasa kanumba aliifikisha Tanzania huko kupitia sanaa.

Kazi ya kanumba iliburudisha na kuifunza jamii.

Andika kitu cha maana Walau Mara 1 kwa mwaka!!! Ongezea Kazi za SK hata malaika Mbinguni ziliwaburudisha
 
Tusimshangae huyu waziri anafata akili za raisi wake.Juzi kati nilimsikia JK kwenye radio akimsifia kanumba mwishoni akasema "MAREHEMU ALIKUWA NA UMBILE ZURI''nikaduwaa nikasema kumbe ni siku hizi ni sawa mwamaume kumsifu uzuri mwanaume mwenzie!

Lahaula!!Unamaanisha au unatania tu mkuu?tumekwisha aisee,kama Rais kasema hivyo basi David Cameron 1-wa Tz 0!!
 
Kanumba alimbaka nani? Yule binti alikuwa anajitangaza kila siku kwenye magazeti kwamba yeye si mtoto ni mtu mzima, Sheria pia inaruhusu binti wa miaka 14 kuolewa.

Kanumba ni zaidi ya wanasiasa wa nchi hii, umeona ule umati, kwa hakika umefuatia kwenye umati wa baba wa taifa.

Kubali ukatae, alistahili kuzikwa na serikali. Hiyo serikali inatumia mamilioni mangapi kwenye shughuli zisizo na tija kwa nchi hii?
RIP Kanumba

Kuhusu umati usikudanganye, watu wenye njaa, wasio na kazi wakiambiwa kuwa hapa kutakuwa na pilau na juice watatoka popote pale kuja kula.Na ukitilia maanani watamuona msaanii fulani.
Kikubwa kinachoongelewa hapa ni Matumizi ya hela ya kodi yetu kutoka kwenye Wizara.

Mawaziri wetu wanaendeshwa na sifa kama mkuu wao...hakuna vipaumbele..kuna mambo mengi wangefanya kumuenzi marehemu lakini itaishia hapo tu..
 
Duuu aisee kweli kua uyaone, yaani sijawahi kuona nchi yenye watu wenye mawazo mgando km TZ!! Yaani msanii tu serikali inamgharamia mazishi yake du! Hivi wasanii km Michael Jackson, Luck Dube, whitney Houston, Bob Marley, Maria Makeba n.k, Serikali za nchi zao ziligharamia mazishi yao?

Tungeenda kuagia kati ya maeneo haya
w.house,mjengon dom au uwanja wa taifa na tungeshusha bendela nusu mlingot pia watu ingekuwa siku ya mapumziko
nakila mwaka tungeeazimisha!
 
Back
Top Bottom