Ni sawa wizara kutumia kodi ya wananchi kutumika kwenye mazishi ya Kanumba?

Kitendo kilichofanyika ni cha busara,kubali ukatae Kanumba amewasaidia kwa njia moja ama nyingine vijana wengi kujiajiri kwa sababu ya kazi zake na pia amelitangaza soko la nchi yetu(la filamu) kwa kiasi kikubwa.usiwe mtu wa kupinga tu mambo ndugu yangu kama kusoma huwezi hata picha huoni,hawezi kuwa kama wewe kiukweli vinhinevyo uniambie ni nin ulishafanya kwa nchi yako chenye manufaa kimataifa

yeh .. na alikuwa kipenzi cha wananchi...! ule umati uliojaa msibani kwake ni thibitisho tosha...

JF toka mdee atangaze anamtetea lulu naona mmegeuka kulipeleka kisiasa hili jambo....

R.I.P THE GREAT
 
Whether it was right or wrong lakini serikali inabidi kuwa makini kwenye haya mambo maana inaweza kutengeneza precedent mbaya. Kesho anaweza akafariki msanii mwingine maarufu halafu serikali isichangie chochote. Kwa haki kabisa watu watataka kujua mbona serikali ilichangia kwa yule lakini siyo huyu.

Word...issue imekuwa kubwa sana kutokana na zile pesa za JK, nadhani serikali ingesaidia kwa njia nyingine, nadhani hata ile ya viongozi wakuu wa kiserikali kushiriki tu ilikuwa ni heshima na support kubwa sana
 
Tusimshangae huyu waziri anafata akili za raisi wake.Juzi kati nilimsikia JK kwenye radio akimsifia kanumba mwishoni akasema "MAREHEMU ALIKUWA NA UMBILE ZURI''nikaduwaa nikasema kumbe ni siku hizi ni sawa mwamaume kumsifu uzuri mwanaume mwenzie!
 
Word...issue imekuwa kubwa sana kutokana na zile pesa za JK, nadhani serikali ingesaidia kwa njia nyingine, nadhani hata ile ya viongozi wakuu wa kiserikali kushiriki tu ilikuwa ni heshima na support kubwa sana

Nakubaliana na wewe serikali ingetafuta njia mbadala ya kuchangia. Kwa mfano, inaweza kujikita zaidi kwenye kuchangia kuendeleza vipaji vya wasanii na kutengeza sheria na policies zinazolinda hati miliki za wasanii na kuhakikisha kuwa zinakuwa enforced. Hapo serikali itakuwa inawawezesha wasanii ili waweze kujitegemea na ku-adsress matizo yao weneywe likiwemo la kundokewa na msanii mwenzao.

Kwa vile sekta ya usanii itakuwa tayari imeshawezeshwa vya kutosha, then yenyewe inaweza kugharamia gharama za kufariki kwa mwenzao. Lakini kutokana na serikali kuto-support hii sekta kwa kiwango cha juu, unakuta wasanii wengi ni wa kubangaiza tuu. Hawafaidiki na kazi zao. Matokeo yake, wanapoondokewa na mwenzao hawawezi hata kugharimia gharama za mazishi. Hili ni tatizo.

Kwa mfano sasa hivi watu wanataka kujua JK na wizara ya ulinzi wamechangia kiasi gani cha fedha kufuatia kifo cha Generali Kyaro aliyekuwa mkuu wa JWTZ na pia mpiganaji mkubwa sana kwenye vita vya Idd Amin. Hakuna mjadala wowote hapa kuwa generali Kyaro ametoa mchango mkubwa sana kwa taifa lakini hajawahi kupelekwa hata hapo India kwa matibabu kama wanavyopelekwa wanasiasa. Kuna umuhimu wa serikali kuwa consistency kwenye haya mambo ya misiba.
 
Kanumba? Aaah' acha aende kijana wetu,ameifanyia makubwa sana nchi yetu!
Yapi hayo makubwa embu tueleze,au kuwafanya akina Lulu na akina anti Ezekiel wafahamike hapa bongo?nahuko vijijini ambako ndiko kuna asilimia kubwa ya watu ,kipi wamenufaika na hizo filamu.Cha muhimu ni kumuombea jamaa apumzike mahala pema tu hayo mambo ya filamu ,filamu nyingi maudhui yake ni mabovu na za hovyo(sio filamu za marehemu tu bali zoooote),huwezi kuangalia sebuleni na watoto.Mimi nimeziona kwenye mabasi na hujaribu kutoziangalia,tukubali tu kila mtu na wakati wake na umaarufu wake,lakini la kusema kafanya makubwa kwa nchi hii haliniingii kichwani
 
Tuache kuwa EMOTIONAL DRIVEN kama wanawake, serikali IMEKOSEA. Kanumba was just an individual na alichofanya si jambo linalokubalika na kila mtu.
1. The so called FILAMU kwa sasa imekuwa ndio kitovu cha uhuni na uasherati mkubwa kama huu uliopelekea kifo chake (Sipongezi, zinaharibu akili zenu)
2. Huyu anayesema msiba wa Kanumba umewagusa wengi, hicho si kigezo. Magazeti ya SHIGONGO yanasomwa na karibu wanawake wooote waliofeli form 4 na wasio na mwelekeo, je hicho ni kigezo kuwa UWAZI na IJUMAA ndio magazeti bora hapa Tanzania? (Lipime wewe mwenyewe kama una akili timamu)
3. Allocation ya fedha za serikali ina taratibu zake. Ikiwa leo kafa Kanumba 15m, kesho (kwa mfano, Mwenyezi Mungu aepushie mbali) akafa Juma Kaseja, serikali isipotoa 15m tutawaelewa?

Nionavyo mimi: Kuwa msanii hakumlazimishi mtu awe MUHUNI. Ukisoma headlines za magazetu yenu haya ya UDAKU utaona jinsi yalivyopambwa na habari za Fulani na Fulani wamelala chumba kimoja Nairobi, Uwoya kafumaniwa na mume wa mtu, Sijui nani kabakwa, yaani ni full upuuzi. Ikiwa haya ndio mnayoyaita maendeleo leo hii tukiwa wabovu kiuchumi kama nchi, basi tuna safari ndefu.

Wasanii wafanye sanaa na sio uhuni. Umaarufu kunuka huo mnaojivunia kwa kuwa nje ya nyumba za baba zenu saa 8 usiku ndio matokeo yake haya. Mtoto wa miaka 18 ana mabwana 6 hadi anawaua wengine kwa presha halafu mniambie mimi nikiwa na akili zangu timamu bila pombe, ETI HAYO NI MAFANIKIO KWA TANZANIA, nyooo! Kwendeni zenu huko

Well said mkuu! Kwanza mara ngapi wapiganaji km askari walokwenda kagera na polisi wanaokufa in the line of duty hawapati fedha toka wizarani ktk mazishi yao! Wanaishia kusafirishwa bush tena wakati mwingine kwa kujichangia wao! Hivi hiyo mi hela ya mchezo huwa haipo! Mtu kabaka ka binti na kidhibiti kipo anapewa sifa kibaaao! Wajinga ndo waliwao.
 
Whether it was right or wrong lakini serikali inabidi kuwa makini kwenye haya mambo maana inaweza kutengeneza precedent mbaya. Kesho anaweza akafariki msanii mwingine maarufu halafu serikali isichangie chochote. Kwa haki kabisa watu watataka kujua mbona serikali ilichangia kwa yule lakini siyo huyu.

true story mzee, lazima government iwe na consistence. kesho akifa mwingine wasipotoa italeta matatizo.
 
Kama huwezi kuthamini mchango wa Kanumba katika nchi hii,basi hujui maana ya kutoa mchango wa Taifa Lako. Katika umri mdogo Kanumba ametoa mchango mkubwa kukuza ajira, ku-intertain, kueleimisha jamii, na kuitangaza vyema nchi yetu. Kumbuka waliko itoa Bongo Movies, kutoka maaigizo hadi kufikia kuwa Industry inayowaweka watu kibao mjini. Sisemi kuwa Industry imekomaa, lakini ilipofika inatia moyo. Mchango wa Kanumba ni mkubwa kuliko mchango wa wanasiasa wengi tu, ambao wanaiba fedha zetu na mwisho wa siku wanazikwa mazishi ya kitaifa. After all hizo unazoita fedha za walipa kodi si pamoja na Kanumba na Familia yake? Halafu watu kama ninyi ndo unaweza kukuta hata hiyo kodi hamlipi na hamna mchango wowote kwa Taifa hili. Hovyo sana wewe.

hakuna mtu asiyelipakodi a cku hzi labda kama hanunui kitu chochote!
 
Jamani mbona sijajibiwa swali langu?nauliza tena. Serikali ya marekani ilitoa sh.ngapi Michael Jackson au whitney houston walipokufa?

Wala usiende mbali huko. Kwani serikali ilitoa kiasi gani Mr. Ebbo alipofariki? Au yeye hakuchangia kwenye sanaa Tanzania? Au kwa vile Mr Ebbo alikuwa anapatikana "Uswazi"? Tena nakumbuka serikali ilikuwa inamtumia Mr Ebbo kwenye kampeni zake za ubinafsaji iliyomfanya mpaka kutunga ule wimbo uitwao"Ubinaf-sishaji". Kwa serikali hii siyo mchango kwa taifa?
 
Nimehuzunika sana na kifo cha mpendwa wetu na kijana mwenzangu Steve Kanumba.BUT kunakitu hakijaniingia akilini pale waziri wa vijana na utamaduni alipotangaza kwamba wizara yake itatoa sh.milioni 15 kwa familia ya kanumba,nilimshuudia kwa macho yangu kupitia tv.Then nilisoma gazeti la mtanzania nikakutana na habari inayosma 'serikali itagharamia mazishi yote ya kanumba.'.nauliza je hii bajeti hiyo inatolewa kwenye fungu gani la bajeti ya serikali ukizingatia Kanumba ni raia wa kawaida kama mimi ? Na je huyo waziri alitoa rambirambi yake binafsi?
Freemason members whether dead or live are very influential. There is no surprise why the government spends that much on kanumba's funeral.
 
hilo la bajeti ndo muhim, mkapa hakuwa kiongozi mzuri sana ila aliheshimu bajeti ndomaana mfumuko wa bei haukuwa mkubwa kama hivi...
Serikali ya huyu .... Haifwati bajeti, hapo ni hela flani za maendeleo zimetolewa kwa ujinga huo. Kuna shughuli kadhaa za maendeleo zitasimama kugharamia mazishi hayo...Tanzania sio Dar pekee huko mikoani sijui Kanumba anamchango gani hadi apewe heshima kubwa hivyo!!!
Sio wivu wakuu, tunajaribu kufunguana macho kuokoa taifa letu na ujinga aliouleta mkuu wetu, kusifiana bila mantiki...
Kwa nchi makini haraka baada ya msiba waziri awajibishwe kwa kukiuka bajeti ya wizara..
Nenda kamwambie yule mama aliyetoka kuchota maji kilomita kadhaa kwamba waziri wako amekuwakilisha uchangia msiba wa Kanumba ndo tutajua wangapi wanawivu...
 
Tuache kuwa EMOTIONAL DRIVEN kama wanawake, serikali IMEKOSEA. Kanumba was just an individual na alichofanya si jambo linalokubalika na kila mtu.
1. The so called FILAMU kwa sasa imekuwa ndio kitovu cha uhuni na uasherati mkubwa kama huu uliopelekea kifo chake (Sipongezi, zinaharibu akili zenu)
2. Huyu anayesema msiba wa Kanumba umewagusa wengi, hicho si kigezo. Magazeti ya SHIGONGO yanasomwa na karibu wanawake wooote waliofeli form 4 na wasio na mwelekeo, je hicho ni kigezo kuwa UWAZI na IJUMAA ndio magazeti bora hapa Tanzania? (Lipime wewe mwenyewe kama una akili timamu)
3. Allocation ya fedha za serikali ina taratibu zake. Ikiwa leo kafa Kanumba 15m, kesho (kwa mfano, Mwenyezi Mungu aepushie mbali) akafa Juma Kaseja, serikali isipotoa 15m tutawaelewa?

Nionavyo mimi: Kuwa msanii hakumlazimishi mtu awe MUHUNI. Ukisoma headlines za magazetu yenu haya ya UDAKU utaona jinsi yalivyopambwa na habari za Fulani na Fulani wamelala chumba kimoja Nairobi, Uwoya kafumaniwa na mume wa mtu, Sijui nani kabakwa, yaani ni full upuuzi. Ikiwa haya ndio mnayoyaita maendeleo leo hii tukiwa wabovu kiuchumi kama nchi, basi tuna safari ndefu.

Wasanii wafanye sanaa na sio uhuni. Umaarufu kunuka huo mnaojivunia kwa kuwa nje ya nyumba za baba zenu saa 8 usiku ndio matokeo yake haya. Mtoto wa miaka 18 ana mabwana 6 hadi anawaua wengine kwa presha halafu mniambie mimi nikiwa na akili zangu timamu bila pombe, ETI HAYO NI MAFANIKIO KWA TANZANIA, nyooo! Kwendeni zenu huko
Asante sana mzee kwa kunisemea.
 
Kitendo kilichofanyika ni cha busara,kubali ukatae Kanumba amewasaidia kwa njia moja ama nyingine vijana wengi kujiajiri kwa sababu ya kazi zake na pia amelitangaza soko la nchi yetu(la filamu) kwa kiasi kikubwa.usiwe mtu wa kupinga tu mambo ndugu yangu kama kusoma huwezi hata picha huoni,hawezi kuwa kama wewe kiukweli vinhinevyo uniambie ni nin ulishafanya kwa nchi yako chenye manufaa kimataifa

Hivi umemuelewa mtoa mada, usipoelewa mada vizuri katika JF unaruhusiwa kupita tu! Mtoa mada anataka ajuzwe hizo gharama za kugharamia msiba wa Kanumba zinazotoka wizarani zilikuwa kwenye fungu lipi au bajeti ipi? Mashaka yetu ni kwamba hapa kuna misuse of government funds. Nilitaka nikuweke sawa ili next time uchangie hoja na si kushambulia mtoa hoja.
 
Issue sio Kanumba kafanya nini. Issue ni watumishi wa serikali wanatoa wapi hayo madaraka ya kuamua kodi yetu itumike wanavyopenda wao. Je kesho akifa mtoto wa waziri naye akaamua atoe ubani wa mamilioni mtamzuiaje? Na je hizo hela wanazotoa ni nani anahakikisha kweli zinafika huko wanakosema zinafika? Nchi yetu hamna madawa hospitalini, watoto bado wanakaa chini mashuleni hamna madawati, lakini bado mnaona ni sawa serikali kugharamia mazishi ya muigizaji wa filamu zisizokuwa na maadili. Ujuha wa hali ya ju!!!!!!!!!
 
Kwa hiyo hata kubaka vibinti vidogo ni kuitangaza vema nchi yetu? Acheni hizo sio wivu ila ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Wamekufa wangapi waliofanya mazuri kwa nchi hii mbona hawajatendewa hivi? Au mnataka kutuambia kuwa ukiondoa baba wa Taifa anaefuata ni Kanumba?

Point unayo ila unaelekea kushindana na mapenzi binafsi ya watanzania. Mi nakuunga mkono kuwa serikali sio kampuni ambayo imetenga fedha maalum kwa ajili ya Public Relation (Social responsibility). ukiona fedha zimetoka ujue bajeti ya wizara fulani imepewa pesa nyingi kupita kiasi, tunajua Ikulu wanalofungu ambalo haliguswi hata kwenye Bajeti kuu ila Wizara ya Nchimbi kiukweli imechoka hiyo pesa bora wangeenda kuwakopesha vijana wamachinga wapanue mitaji yao ya elfu ishirini.
 
tuache kuwa emotional driven kama wanawake, serikali imekosea. Kanumba was just an individual na alichofanya si jambo linalokubalika na kila mtu.
1. The so called filamu kwa sasa imekuwa ndio kitovu cha uhuni na uasherati mkubwa kama huu uliopelekea kifo chake (sipongezi, zinaharibu akili zenu)
2. Huyu anayesema msiba wa kanumba umewagusa wengi, hicho si kigezo. Magazeti ya shigongo yanasomwa na karibu wanawake wooote waliofeli form 4 na wasio na mwelekeo, je hicho ni kigezo kuwa uwazi na ijumaa ndio magazeti bora hapa tanzania? (lipime wewe mwenyewe kama una akili timamu)
3. Allocation ya fedha za serikali ina taratibu zake. Ikiwa leo kafa kanumba 15m, kesho (kwa mfano, mwenyezi mungu aepushie mbali) akafa juma kaseja, serikali isipotoa 15m tutawaelewa?

Nionavyo mimi: Kuwa msanii hakumlazimishi mtu awe muhuni. Ukisoma headlines za magazetu yenu haya ya udaku utaona jinsi yalivyopambwa na habari za fulani na fulani wamelala chumba kimoja nairobi, uwoya kafumaniwa na mume wa mtu, sijui nani kabakwa, yaani ni full upuuzi. Ikiwa haya ndio mnayoyaita maendeleo leo hii tukiwa wabovu kiuchumi kama nchi, basi tuna safari ndefu.

Wasanii wafanye sanaa na sio uhuni. Umaarufu kunuka huo mnaojivunia kwa kuwa nje ya nyumba za baba zenu saa 8 usiku ndio matokeo yake haya. Mtoto wa miaka 18 ana mabwana 6 hadi anawaua wengine kwa presha halafu mniambie mimi nikiwa na akili zangu timamu bila pombe, eti hayo ni mafanikio kwa tanzania, nyooo! Kwendeni zenu huko

naipenda jf,umedadavua vyema.thanks.
 
Tuache kuwa EMOTIONAL DRIVEN kama wanawake, serikali IMEKOSEA. Kanumba was just an individual na alichofanya si jambo linalokubalika na kila mtu.
1. The so called FILAMU kwa sasa imekuwa ndio kitovu cha uhuni na uasherati mkubwa kama huu uliopelekea kifo chake (Sipongezi, zinaharibu akili zenu)
2. Huyu anayesema msiba wa Kanumba umewagusa wengi, hicho si kigezo. Magazeti ya SHIGONGO yanasomwa na karibu wanawake wooote waliofeli form 4 na wasio na mwelekeo, je hicho ni kigezo kuwa UWAZI na IJUMAA ndio magazeti bora hapa Tanzania? (Lipime wewe mwenyewe kama una akili timamu)
3. Allocation ya fedha za serikali ina taratibu zake. Ikiwa leo kafa Kanumba 15m, kesho (kwa mfano, Mwenyezi Mungu aepushie mbali) akafa Juma Kaseja, serikali isipotoa 15m tutawaelewa?

Nionavyo mimi: Kuwa msanii hakumlazimishi mtu awe MUHUNI. Ukisoma headlines za magazetu yenu haya ya UDAKU utaona jinsi yalivyopambwa na habari za Fulani na Fulani wamelala chumba kimoja Nairobi, Uwoya kafumaniwa na mume wa mtu, Sijui nani kabakwa, yaani ni full upuuzi. Ikiwa haya ndio mnayoyaita maendeleo leo hii tukiwa wabovu kiuchumi kama nchi, basi tuna safari ndefu.

Wasanii wafanye sanaa na sio uhuni. Umaarufu kunuka huo mnaojivunia kwa kuwa nje ya nyumba za baba zenu saa 8 usiku ndio matokeo yake haya. Mtoto wa miaka 18 ana mabwana 6 hadi anawaua wengine kwa presha halafu mniambie mimi nikiwa na akili zangu timamu bila pombe, ETI HAYO NI MAFANIKIO KWA TANZANIA, nyooo! Kwendeni zenu huko

Hayo mengine simo ila hili la mstari mwekundu ndio msingi wa hoja nzima. Nakuunga mkono.
 
Back
Top Bottom