yahoo
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 3,527
- 1,405
Nimehuzunika sana na kifo cha mpendwa wetu na kijana mwenzangu Steve Kanumba.BUT kunakitu hakijaniingia akilini pale waziri wa vijana na utamaduni alipotangaza kwamba wizara yake itatoa sh.milioni 15 kwa familia ya kanumba,nilimshuudia kwa macho yangu kupitia tv.Then nilisoma gazeti la mtanzania nikakutana na habari inayosma 'serikali itagharamia mazishi yote ya kanumba.'.nauliza je hii bajeti hiyo inatolewa kwenye fungu gani la bajeti ya serikali ukizingatia Kanumba ni raia wa kawaida kama mimi ? Na je huyo waziri alitoa rambirambi yake binafsi?